Warioba awajibu CCM

Warioba awajibu CCM

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameeleza sababu za Tume hiyo kupendekeza Serikali tatu, huku akisisitiza kuwa suala hilo lilikuwepo tangu siku nyingi. Kauli hiyo inaonekana kama kukijibu Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimependekeza kuwepo kwa Serikali mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari Warioba aliongeza,

"Mikutano na Mabaraza ya Katiba siyo ya kupiga kura bali ni kujadili na kutoa hoja ambazo zitakuwa na msingi kwa masilahi ya taifa na siyo kutetea masilahi ya kundi au watu fulani,"

CCM

Tangu rasimu hiyo ilipotolewa mapema Juni mwaka huu, chama hicho kilionyesha kutokuridhishwa na rasimu hiyo na kuahidi kuipeleka kwa wanachama wake.

Katika kuonyesha kutokuridhshwa huko, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaeleza wajumbe wa Mabaraza ya Katiba jijini Dar es Salaam juzi azma ya chama hicho kuwa na rasimu mbadala.

Nape ambaye aliitumia siku nzima ya Alhamisi kuzungumza na wajumbe hao wa mabaraza, alisema wameandaa rasimu yao ambayo imeandikwa vitu wanavyohitaji na wanachama wote wanapaswa kuvisimamia.

==Mwananchi==
 
Sina uelewa na kauli ya Mh Warioba anapozuia wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wasikubali kushawishiwa na taasisi au watu fulani. Je hawa wajumbe watakwenda na mawazo ya nani au ni ya kwao wenyewe? Je sisi tusiokuwa wajumbe wa hayo mabaraza mawazo yetu yataewasilishwa na nani? Nafikiri mfumo mzima una walakini. Turuhusuni na sisi tusiokuwa kwenye mabaraza yoyote tutoe mawazo yetu. Wote mnajua Mabaraza haya yalivyoingiliwa na makundi rasmi na yasiyo rasmi, wengi waliotaka kuingia walienguliwa.
 
Mkuu Getstart bado unayo nafasi ya kutoa maoni yako kupitia mabaraza yasiyo chini ya Tume ya mabadiliko ya katiba, kama vile mabaraza ya wafanyabiashara, madhehebu ya dini, vyama vya siasa n.k. Usikate tamaa.
 
Last edited by a moderator:

Alipoambiwa kulikuwa na uchakachuaji kwenye mabaraza haku-take action. Jana anasema watu wasishawishiwe. Uzee nao is not an investment.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mkuu Getstart bado unayo nafasi ya kutoa maoni yako kupitia mabaraza yasiyo chini ya Tume ya mabadiliko ya katiba, kama vile mabaraza ya wafanyabiashara, madhehebu ya dini, vyama vya siasa n.k. Usikate tamaa.
Hii inawezekana tu kama uko kwenye mabaraza hayo. Kumbuka kwa mujibu wa maelekezo ya Tume mabaraza hayo yanaundwa na watu wenye mawazo yanayofanana, kwa maana ingine ni vikundi vya wananachama wa aina fulani. Kuna watu hawako huko na wanatakiwa kutoa ,maoni yao, kwa nini tusiruhusiwe kuwasilisha maoni yetu kwenye Tume. Tunafungwa na Mabaraza ambayo nina hakika yatatoa maoni yenye mitazamo ya kimakundi yao na maslahi yao.
 
Tusidanganyane! Duniani kote Katiba haiwezikuandikwa kwa kalamu inayotumia wino wa kawaida. Katiba wanayoitaka wananchi wengi inaandikwa kwa damu za binadam. Lazima damu imwagike ule wino ndio katiba mpya. Ni nchi chache sana zinaandika kwa kalamu ya kawaida. Tannganyika ni moja ya nchi iliyobahatika mwaka 1961 kuandika katiba bila ya kutumia damu. Kwa sasa ni ngumu sana kwa watawala kukubali mabadiliko makubwa kama hayo yanayotaka kufanyika. For any how tukija kwenye voting majority watakuwa watu kwa chama tawala na msitegemee mabadiliko yoyote ya msingi. Lakini hata CUF au CHADEMA wakichukua nchi hawatakubaliana na hii rasmu mpya ya katib. Watapenda kuwa na Speaker wao, Jaji mkuu wao, Wakuu wa mikoa wa kwao, mawaziri watakao fuata Itikadi za vyama vyao. Kwa sasa naona CCM wako sahihi sana. Katika mazingira haya ya ushindani wa kisiasa ukimpa adui wako ahueni atakushinda tu. for any delicate CCM watakuwa hawana chao. Itabaki history. Vinginevyo CCM ikubali kuachia nchi bila kumwaga damu kama wao walivyopewa bila kumwaga damu. Zanzibar tayari walimwaga damu ikaandika katiba mpya.
 
Hoja inayo umiza kichwa kwenye rasimu ni kuhusu serekali 3,kuna watanganyika wanahofu na tanganyika yao kurudi.
 
Back
Top Bottom