Warioba Anataka Nini Hasa?

nani kakwambia warioba ndo anawatingisha, hivi hamjajua kwamba mmeshatoka madarakani,fungukeni macho muone yaliyotokea hebu niambie kampuni ya strabag imeyeyukia wapi
 

mwana -------- ni aibu kwa babaye........hv hata kama hujafikisha miaka 25 huwezi Ku reason zaid ya hapo? basi jenga hoja yako kwa kuengemea mgogoro uliopo wa kikatiba kati ya zanz na JMT.....!!!

hata kutushawishi kwa hoja ya jeshi ka yule kanjanja umeshindwa kweli........?????? hlo gazeti lazima lipate hasara sana Leo.....nan wa kusoma udaku wak??
 
Mbona chadema walifanya mikutano ya hadhara karibu nchi nzima kueleza wanachama wao na wapenzi wao nini wanachotakiwa kusema.hilo warioba hakuona..?

Tatizo ni kuwa Chadema walitoa elimu ya uraia na kuwaacha wananchi wakajieleze wenyewe lakini CCM iliwapa hadi madesa, jamaa wakaingia nayo kwenye chumba cha mtihani. Wasahihishaji wakakuta kuna mfanano usiokuwa wa kawaida katika maelezo yani hadi nukta. Sasa ikabidi Mzee awafutiei matokeo!
 
W. J. Malecela mimi nakushauri rudi tu kule Amerika ulikokuwa unapakuliwa msosi.
Hii si sehemu ya kuja ku-advertise magazeti yenu ya wauza sembe.
Invisible peleka hii kitu kule kwenye matangazo
 
Last edited by a moderator:

Mtu anadesa mpaka nukta, CCM ni janga kuu
 

Kumbuka kuwa Jakaya Mrisho Kikwete kakuta kuna kero za Muungano na kafanya jihadi (kajitahidi sana) kutatua hizo kero.

Mimi sitofautiani na Kikwete. Mpira uko kwenu muucheze mchezavyo Zanzibar ni lazima iwe na mamlaka kamili. Imeanza kwa kutambulika rasmi kuwa ni nchi, sasa bado kuwa na Uhuru kamili wa kujiamulia mambo yake, siyo mpaka yakaamuliwe Dodoma.

Tunataka tuione OIC inarudi Zanzibar haraka iwezekanavyo.
 
Kuna siku niliandika hapa kuwa sikio linatabia ya kusikia kile linachotaka kusikia,tofauti na hapo halitokisia lisichotaka. CCM toka awali kabisa sikio lao halikutaka kusikia "kubadili muundo wa Muungano". Tume hii hii ya Jaji Warioba kama ingekuja na maoni ya kuwa "wengi wamependekeza" Muungano wa serikali mbili kama ulivyo,leo dhihaka,matusi,kejeli na dharau dhidi ya Warioba na Tume visingekuwepo.
An Ear of CCM was not and never will it be ready to correctly hear the so called "serikali 3". Ukiwasikiliza wajumbe almost 99.99% hawajibu hoja za msingi kabisa zilizomo ndani ya Rasimu,they personally attack warioba na Tume. Ikiwa CCM inasema Rasimu haswa ibara inayogusa Muundo wa Muungano si maoni ya wananchi,na ikiwa wajumbe karibu wote wanasema "wananchi wake" wamemtuma kuunga Serikali mbili,suala la Serikali ngapi/Muungano wa aina gani lirudishwe kwa wananchi lipigiwe kura then mchakato uendelee. Kuendelea kujadili Rasimu ambayo wengi (CCM) wanasema ni ya uongo,means tayari hatua hii imevurugika...we can not step ahead.
 

Kwa maneno mengine unaunga mkono serikali tatu.... Maana tuwe na Nchi inaitwa Zanzibar na nyingine Tanganyika
 
Tatizo la maccm wanamjadili Warioba badala ya kujadili issues ambazo tume imeziibua, mfano kwamba katiba ya muungano inasema Tanzania ni nchi moja ambayo ilikuwa formed baada ya kuunganisha iliyokuwa jamhuri ya Tanganyika na iliyokuwa jamhuri ya Zanzibar lakini mabadilko ya katiba ya Zanzbar ya 2010 yanaitambua Zanzibar kama nchi ambayo imjitwalia baadhi ya madaraka ya serikali ya muungano. JK alishindwa kuilinda katiba ya muungano na akaacha Zanzibar ivunje katiba kwa mabadiliko hayo ya 2010. Kwa bunge lenye wabunge makini tungekuwa tumemsahau JK zamani kwani angekuwa ameondolewa kwa kushindwa kuilinda katiba (Mwenye clip ya hotuba ya baba wa taifa ya Kilimanjaro Hotel kuhusu katiba aiweke).

Anachofanya Warioba ni funika kombe mwanaharamu apite kwani it is too late as ili muungano uwe wa serikali 2 maccm waiadibishe Zanzibar irudishe katiba yake kabla ya mabadiliko ya katiba yao 2010 jambo ambalo ni gumu as inabidi liamuliwe na kura ya maoni ya Wazanzibari.

Msaliti wa muungano ni yupi, aliyekubali Zanzibar ijitwalie madaraka ya serikali ya muungano au anayetaka kurekebisha hali iliyopo pasipo kumshitaki raisi ambaye ameshindwa kuilinda katiba? Anachofanya Warioba na kueleza sababu za tume kupendekeza mfumo wa serikali 3 ni sahihi kwani maccm mnamshambulia pasipo hoja na matusi, unataka anyamaze kimya, CCM siyo mama yake na ikibidi atatoka.

Muungano kama ndoa haupaswi kulindwa na vifaru na madege yaliyo oneshwa kwenye sherehe za muungano, kama hakutakuwa na hiari na maridhaiano hautalazimishwa kwa nguvu yoyote, utakufa tu. Maccm kaeni na mjibu hoja za nguvu na mwache kutumia nguvu kujibu hoja.
 
Napenda argument zako, kwa kuwa zina uhalisia sana, unaandika unachokiamini.
 
Mheshimiwa angalia hizo rangi nyekundu yaani ndicho ulichoambulia pamoja na kutumia kodi zetu kusoma ulaya, tumia tu lugha ya kiswahili tutakuelewa sio kuvurunda sarufi ya lugha ya watu :blabla:
 
Mheshimiwa angalia hizo rangi nyekundu yaani ndicho ulichoambulia pamoja na kutumia kodi zetu kusoma ulaya, tumia tu lugha ya kiswahili tutakuelewa sio kuvurunda sarufi ya lugha ya watu :blabla:

Umeona eeeh!
 
Kwa maneno mengine unaunga mkono serikali tatu.... Maana tuwe na Nchi inaitwa Zanzibar na nyingine Tanganyika

Kama ni tatu zitawapa Uhuru kamili wakujiamulia mambo yao ya msingi au kama ni mbili haijalishi, mradi tusiwabane na kuwalazimisha tuyatakayo sisi. Mfano kama Serikali yetu imeamua haina dini basi tusiwalazimishe na wao kuwa Serikali yao isiwe na dini.
 
Naona unawashawishi wenzako mmngoe meno na kucha mzee wetu. Mmezoea kutuburuza tangu enzi za babako mmerithi nyie mnataka kuendelea. Anauchungu na maagizo yetu tuliyomtuma ambayo mmeamua kuingiza kapuni. Ni kweli hayupo peke yake ila tupo Watanzania wengi saaaaaaana nyuma yake hicho ndio kinampa nguvu.
 
Mheshimiwa angalia hizo rangi nyekundu yaani ndicho ulichoambulia pamoja na kutumia kodi zetu kusoma ulaya, tumia tu lugha ya kiswahili tutakuelewa sio kuvurunda sarufi ya lugha ya watu :blabla:

- Sijakuelewa mkuu sana eti tatizo lipo wapi na hayo maneno ya English? hebu fafanua kidogo?

Le Mutuz System
 

- Sio kweli hawakilishi wananchi wengi angekuwa kusingekuwa na utata na ripoti yake, poleni sana!1

Le Mutuz System
 
Ni kweli lina noah fulani hivi lina machata ya kumwaga na huwa linapiga mziki kama limbukeni fulani

- ha! ha! si ungefungua thread ya members wa JF na magari yao nani anatembelea gari gani na nani anapiga muziki kwenye gari, le mburulazzz kazi yako ni kutembea mitaani kusikiliza magari ya members wa JF ha1 ha! ha!

Le Mutuz system
 
Mmezoea kuabuse katiba ndio maana mnakuwa na hofu kiasi hiki mkijua kila atakaeingia atakiuka kama CCM ilivyozoea.
 

Deni la Taifa linakaribita 40 Trillion hujaiona hiyo thread?
 

Dada Faiza,ili huo uhuru kamili uwepo,bila kupindisha maneno ni serikali 3..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…