Warioba ‘amnanga’ aliyetoa maoni kwa waraka wa CCM

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amewakosoa wajumbe wa mabaraza ya Katiba wanaokuja kwenye mikutano na matamko ama nyaraka za vyama, badala ya maoni ya wananchi waliowachagua

Jaji alitoa kauli hiyo hiyo nzito wakati akifungua mkutano wa baraza la katiba katika Halmashauri ya Musoma vijijini muda mfupi baada ya kundi la tatu kuwasilisha maoni yake.

Kauli ya Jaji Wariona ilikuja mara baada ya mjumbe Tobias Maugo kuchangia maoni kwenye rasimu ya Katiba akitumia waraka unaodaiwa kusambazwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanachama wake kikiwataka washinikize kupitishwa kwa mapendekezo ya chama hicho

Mjumbe huyo alikuwa akiusoma waraka huo neno kwa neno kana kwamba ilikuwa maoni yake mwenyewe.

“Mjumbe unasoma waraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao sisi Tume tayari tunao mikononi mwetu. Hatukuzuia kusoma tena lakini nilitaka tu kukwambia kuwa kama una maoni mengine, uyasema kwa kuwa waraka huo tunao tayari.’’

Waraka wa CCM kwa wanachama wake umeanza kuleta tafrani ambapo juzi mkoani Iringa Mjumbe wa Tume ya Katiba alimzuia mmoja wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya kutumia waraka huo kutoa maoni yake.

Alhaj Said El-Maamry ambaye kitaalamu ni mwanasheria, alimzuia Hussein Kiswil aliyekuwa akichangia mapendekezo kwenye rasimu hiyo, baada ya kubaini kuwa, alichokuwa anazungumza kilitokana na maelekezo ya CCM.

Hata hivyo hatua hiyo ilizua tafrani katika mkutano huo, baada ya mjumbe huyo wa Baraza la Katiba wilaya, kutoridhika na msimamo huo wa mjumbe wa tume na kupendekeza afukuzwe kwenye mchakato huo, kwa kile alichoeleza kuwa anapingana na maelekezo ya kuwaacha watu watoe maoni yao kwa uhuru.

Kiswil alidai kuwa mjumbe huyo hastahili kuendelea na kazi ya kusimamia mabaraza hayo kwa kuwa yeye pamoja na wajumbe wenzake kadhaa, hawana imani naye.

“Siku ya jana (juzi) tukiwa ndani ya ukumbi huu mlitueleza kuwa kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake katika kuchangia rasimu ya katiba hii, mimi nilichaguliwa kuingia katika kundi na kupewa jukumu la kuchambua muundo Muungano” alisema Kiswil na kuongeza;

“Nilipoanza kuchangia mimi aliingia Mjumbe wa tume El-Maamry na kusikiliza, nilipomaliza kabla hata ya kuruhusiwa na mwenyekiti alianza kuzungumza akisema maoni niliyotoa mimi ni maelekezo ya chama cha Mapinduzi na aliongeza kuwa ana taarifa za kuwapo kwa kiongozi mkubwa wa kisiasa aliyekuja Iringa kutoa semina… Nilitaka anithibitishie kama hayo aliyoyasema ni ya kweli.”

Kitendo cha CCM kuusambaza waraka huo kwa wanachama wake kinaelezwa kuwa ni kinyume na kanuni na utaratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inataka watu watoe maoni yao wenyewe.

Tayari baadhi ya wajumbe wa Mabaraza ya Katika ngazi ya wilaya waliopata waraka huo wameripotiwa kuanza kuutumia kujenga hoja katika mijadala inayoendelea maeneo mbalimbali nchini.
 
Warioba akubaliane na dhana ya garbage in garbage out! Kinacho mtesa sasa ni denial! Alisha ambiwa na yeye akakiri kuwa kulikuwa na udhaifu mkubwa wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya kata na baadae wilaya.

Udhaifu ule ndio huu unaotumika sasa kufanya mafyongo! Awe mpole tu chadema itaonyesha njia kwenye mabaraza yake.
 
kumbe warioba alijua pa kuja kuwashikia magamba ha aha aha aha!!! sasa mwenyekiti wa tume naye kajipanga kusikiliza maoni ya mjumbe muhusika sio maoni ya ccm. safi sana tume endeleeni kusimamia upatikanaji wa katiba ya Tanzania sio katiba ya ma ccm
 
Nakumbuka 2010, Makamba aliwazuia wagombea wa CCM kushiriki katika midahalo. Kinana amesambaza waraka kupinga serikali tatu. Inavyoelekea huko CCM hakuna demokrasia na viongozi wao wengi ni mbumbumbu
 
Kama CCM mlishangia kwamba Jaji Warioba ni mwana itikadi mwenzenu baada tu ya kupewa kuingoza hii tume hii nyeti ya katiba -- basi waliingia chaka; yule mzee anafuata misimamo wa watanzania wote; poleni sana CCM kutumia hela nyingi kuhonga ili mpate wajumbe wengi kwenye mabalaza haya!! sasa mnaona mambo yanavyowageuka?

So far so good Mzee Warioba, watumikie watanzania watakukumbuka vizazi na vizazi.
 
Unasema waraka unadhaniwa kuwa wa CCM,kama unadhaniwa ukweli uko wapi mbona unaleta mambo ya kudhani.
 
Kama CCM mlishangia kwamba Jaji Warioba ni mwana itikadi mwenzenu baada tu ya kupewa kuingoza hii tume hii nyeti ya katiba -- basi waliingia chaka; yule mzee anafuata misimamo wa watanzania wote; poleni sana CCM kutumia hela nyingi kuhonga ili mpate wajumbe wengi kwenye mabalaza haya!! sasa mnaona mambo yanavyowageuka?

So far so good Mzee Warioba, watumikie watanzania watakukumbuka vizazi na vizazi.
Hayo mawazo yako ni sawa na bure kama ccm wangetaka kuweka mtu wao kwenye tume ya katoba wangemweka hata mukamu lakini hayo mambo hawana.
 
sishangai kwani hata kwenye ilani yao ya uchaguzi 2010 hakukuwa hata na sentensi moja kuhusu hii katiba mpya, tunashangaa sijui hili la katiba mpya wameli-copy wapi na sina uhakika kama waliku kweli wamejiandaa na hizi changamoto thats why wanahaha kurubuni mabaraza haya.
 
kumbe warioba alijua pa kuja kuwashikia magamba ha aha aha aha!!! sasa mwenyekiti wa tume naye kajipanga kusikiliza maoni ya mjumbe muhusika sio maoni ya ccm. safi sana tume endeleeni kusimamia upatikanaji wa katiba ya Tanzania sio katiba ya ma ccm

Yule mzee anamitego ya kiutu uzima
 
Unasema waraka unadhaniwa kuwa wa ccm,kama unadhaniwa ukweli uko wapi mbona unaleta mambo ya kudhani.

CCM UMEBEMENDA MABARAZA YA KATIBA, UMEBEMENDA HADI WANACHAMA WAKO, hebu cheki namna yao ya kufikiri....KATIBA YA NCHI IANZE THEN SERA ZA VYAMA.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amewakosoa wajumbe wa mabaraza ya Katiba wanaokuja kwenye mikutano na matamko ama nyaraka za vyama, badala ya maoni ya wananchi waliowachagua

Jaji alitoa kauli hiyo hiyo nzito wakati akifungua mkutano wa baraza la katiba katika Halmashauri ya Musoma vijijini muda mfupi baada ya kundi la tatu kuwasilisha maoni yake.

Kauli ya Jaji Wariona ilikuja mara baada ya mjumbe Tobias Maugo kuchangia maoni kwenye rasimu ya Katiba akitumia waraka unaodaiwa kusambazwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanachama wake kikiwataka washinikize kupitishwa kwa mapendekezo ya chama hicho

Mjumbe huyo alikuwa akiusoma waraka huo neno kwa neno kana kwamba ilikuwa maoni yake mwenyewe.

“Mjumbe unasoma waraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao sisi Tume tayari tunao mikononi mwetu. Hatukuzuia kusoma tena lakini nilitaka tu kukwambia kuwa kama una maoni mengine, uyasema kwa kuwa waraka huo tunao tayari.’’

Waraka wa CCM kwa wanachama wake umeanza kuleta tafrani ambapo juzi mkoani Iringa Mjumbe wa Tume ya Katiba alimzuia mmoja wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya kutumia waraka huo kutoa maoni yake.

Alhaj Said El-Maamry ambaye kitaalamu ni mwanasheria, alimzuia Hussein Kiswil aliyekuwa akichangia mapendekezo kwenye rasimu hiyo, baada ya kubaini kuwa, alichokuwa anazungumza kilitokana na maelekezo ya CCM.

Hata hivyo hatua hiyo ilizua tafrani katika mkutano huo, baada ya mjumbe huyo wa Baraza la Katiba wilaya, kutoridhika na msimamo huo wa mjumbe wa tume na kupendekeza afukuzwe kwenye mchakato huo, kwa kile alichoeleza kuwa anapingana na maelekezo ya kuwaacha watu watoe maoni yao kwa uhuru.

Kiswil alidai kuwa mjumbe huyo hastahili kuendelea na kazi ya kusimamia mabaraza hayo kwa kuwa yeye pamoja na wajumbe wenzake kadhaa, hawana imani naye.

“Siku ya jana (juzi) tukiwa ndani ya ukumbi huu mlitueleza kuwa kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake katika kuchangia rasimu ya katiba hii, mimi nilichaguliwa kuingia katika kundi na kupewa jukumu la kuchambua muundo Muungano” alisema Kiswil na kuongeza;

“Nilipoanza kuchangia mimi aliingia Mjumbe wa tume El-Maamry na kusikiliza, nilipomaliza kabla hata ya kuruhusiwa na mwenyekiti alianza kuzungumza akisema maoni niliyotoa mimi ni maelekezo ya chama cha Mapinduzi na aliongeza kuwa ana taarifa za kuwapo kwa kiongozi mkubwa wa kisiasa aliyekuja Iringa kutoa semina… Nilitaka anithibitishie kama hayo aliyoyasema ni ya kweli.”

Kitendo cha CCM kuusambaza waraka huo kwa wanachama wake kinaelezwa kuwa ni kinyume na kanuni na utaratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inataka watu watoe maoni yao wenyewe.

Tayari baadhi ya wajumbe wa Mabaraza ya Katika ngazi ya wilaya waliopata waraka huo wameripotiwa kuanza kuutumia kujenga hoja katika mijadala inayoendelea maeneo mbalimbali nchini.

hii tume ina kazi kubwa sana ya kurudisha credibility ambayo ishaipoteza.
Natumai busara za Warioba za kuleta maoni ya wananchi kwenye constitution zitatumika ipasavyo kuliko kutimizwa matakwa ya aliyemchagua.
 
Hatimaye MAGAMBA wazidi kupata wakati mgumu , the end will come to justify the beginning. Jaji warioba :laser:MURIKA MWIZI MEEEEN.
 
Tangu awali Jaji Warioba alitahadharishwa kuwa ccm 'wamehack' zoezi la uteuzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba lakini akaamua kufumba macho na kusonga mbele.
Sasa huu waraka wa ccm unaosambazwa umezidi kumuweka pabaya kwakuwa wanachama wa ccm ambao ni wajumbe wa mabaraza wanatoa mawazo ya ccm na wala si mawazo ya wananchi waliowachagua! Sasa hapo ndipo tutamuweka kwenye mizania na kupata ukweli kama yeye anafanya kazi kwa maslahi ya ccm ama kwa maslahi ya wananchi wote!
 
Warioba akubaliane na dhana ya garbage in garbage out! Kinacho mtesa sasa ni denial! Alisha ambiwa na yeye akakiri kuwa kulikuwa na udhaifu mkubwa wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya kata na baadae wilaya.

Udhaifu ule ndio huu unaotumika sasa kufanya mafyongo! Awe mpole tu chadema itaonyesha njia kwenye mabaraza yake.

Hahahahahaaa sasa ndio kinaanza kueleweka na ni dalili kuwa tutapata katiba nzuri kama wataendelea kuwa bana na hizo nyaraka zao
 
Mabaraza ya katiba yamelalamikiwa kuhodhiwa na CCM warioba aliweka pamba masikioni. Sasa hivi ndo analeta unafiki wake!

Viongozi wetu wamezoea kuzomewa na kundi la watu tena hadharani hata ukionywa vipi kabla ya kuzomewa huwezi kuamini kuwa ni onyo. Acha waendelee kuwa tomaso. Ila haya yote yana muda wake.
 
Unasema waraka unadhaniwa kuwa wa ccm,kama unadhaniwa ukweli uko wapi mbona unaleta mambo ya kudhani.

WARIOBA hakuna hasicho kijua kuhusu CCM na walaka wao, mimi namshangaa sana sababu alisema hataki kumuona mtu akishawishiwa na MTU MWINGINE ama TAASISI yoyote KILA MTU ATOE MAONI YAKE MWENYEWE, sasa huu si ni USHAHIDI WA KUTOSHA achukue hatua sasa kama yeye KIDUME, na serikali 3 zote za nini? HAPA KIBOKO alikuwa MWALIMU WAO marehemu JK orijino mwana wa NYERERE, Aliposema tuchukue maoni kuhusu mfumo wa VYAMA VINGI, WANAFIKI wakashawishi watu wapige kura za HAPANA yeye akasema NDIO, angalia hapa tulipo, hivi ingekuaje chini ya CHAMA KIMOJA
 
Tatizo watanganyika karibia wote mnapenda muungano kuliko tanganyika yenu ndio maana ccm wanayawakilisha mawazo yenu watanganyika kupitia waraka walio utoa.
 
Back
Top Bottom