Waraka

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
Wana-JF,naombeni nafasi yenu 'nishee' nanyi Waraka ufuatao.Kiukweli,Waraka huu ulimrudisha mpwa wangu Ashura kwenye mstari na sasa anapaa kuelekea kwenye mafanikio.Sasa yuko Kidato cha Pili na anaongoza darasani. Namshukuru sana Mungu kwa kuniongoza katika uandishi wa Waraka huu. Waraka wenyewe ni huu hapa:
WARAKA WA KWANZA WA PETRO KWA ASHURA

​
Mjomba Ashura,naomba nikusalimu.Baada ya salamu naomba nikuambie mambo yafuatayo ambayo mimi nayaona na kuamini kuwa yana manufaa kwako:


Mjomba Ashura,mimi ni mjomba wako kwa maana ya kuwa kaka wa mama yako Scolastica Eusebius Mselewa(nilizaliwa mwishoni baada yake).Hakuna ubishi kuwa wewe waniita mjomba nami nakuita Ashura,mpwa wangu.Baba yako Haji Mokiwa ni rafiki yangu sana kwakuwa tumekuwa katika kipindi kimoja.Tulishiriki pamoja kwenye michezo mbalimbali kwenye makuzi yetu hasa mpira wa miguu.Alikuwa mchezaji mzuri sana…mshambuliaji.Mimi sikuwa mchezaji mzuri kama yeye ila nilikuwa mshabiki pia ‘kocha' mzuri na wakupigiwa mfano.Hadi leo niko hivyo.Namudu vyema mchezo wa ‘draft' lakini nabaki kuwa mshabiki mkubwa wa mpira wa miguu,mchezo uliochezwa na baba yako.


Mjomba Ashura,katika familia aliyotokea mama yako ambayo mimi nahusika nayo,Mama yetu,Marehemu Costantina Michael Mhagama,na baba yetu Marehemu Eusebius Petro Mselewa,tulizaliwa watoto kumi na wawili(12).Majina yao ni kama ifuatavyo:Severia,Johnbosco,Stella,Aurelian,Immaku​lata,Birgita,Stella,Johnbosco,Deograsias,Immakulat​a,Scolastika(mama yako) na mimi Petro(mjomba wako na mwandishi wa waraka huu).Waweza kuona kuwa kuna majina yamerudiwa.Hivyo ndivyo ilivyokuwa baada ya waliotangulia kufariki dunia.Kati ya watoto hao 12,watatu walifariki utotoni.Hao ni Johnbosco,Stella na Immakulata(wa kwanza kuandikwa hapo juu).Tisa tuliobaki tulifanikiwa kufikia utu uzima na kuingia shule.Watatu:Aurelian,Birgita na Stella walifariki dunia mwaka 2000,2001 na 1998(kama walivyotajwa).Mungu azilaze roho za marehemu wote wa familia yetu hii mahali pema peponi.Amina.


Mjomba Ashura,kati ya watoto wa babu na bibi yako waliotajwa hapo juu,tisa waliingia shule na kusoma.Ni wale waliofikia umri wa utu uzima baadaye.Kati yao,mimi tu nilifanikiwa kuendelea na masomo ya Sekondari baada ya kumaliza elimu yangu ya Shule ya Msingi mwaka 1997 katika Shule ya Msingi Visiga(shule unayosomea).Nilichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Ruvu.Hapo nilisoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne,yaani kuanzia mwaka 1998 hadi 2001.Nikaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita mwaka 2002 hadi 2004 katika Shule ya Wavulana ya Songea.Baada ya hapo nikajiunga na Chuo Kukuu cha Dar es Salaam mwaka 2005 kusomea Shahada(Degree) ya Kwanza ya Sheria.Nilimaliza mwaka 2009.Kwasasa,nimeajiriwa kama Afisa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Hivyo ndivyo ilivyo kwa upande wangu.






Mjomba Ashura,wakati mimi nilipokuwa nakua na kusoma wewe ulikuwa bado ni mtoto mdogo.Maisha yangu ya nyumbani na Shuleni yalikuwa magumu sana…ya umaskini mkubwa.Nilivumilia mno.Kwakuwa mama yako ndiye tuliyekua pamoja,yeye anafahamu vyema jinsi tulivyoishi.Anajua vyema sana.Ukipata nafasi muulize.Usikose.


Mjomba Ashura,tangu mwanzo wa makuzi yenu,wewe na Fatuma(mtoto wa dada Immakulata),nimekuwa nikijihusisha na maisha yenu kwa namna moja au nyingine.Nimekuwa nikijihusisha na kuwatunza,kuwafunza,kuwachunga,kuwalinda,kuwatetea​,kuwalea,kuwakemea na zaidi ‘kuwalazimisha' kuhudhuria masomo yenu ya Shule ya Msingi.Sasa mpo darasa la sita.Kujihusisha kwangu kulikuwa hakutegemei uwepo wa wazazi wenu au la.Nilikuwa nafanya hivi nikiamini kuwa watoto wa dada na kaka zangu ni wangu.Naweza kuwa ninaamini katika ujinga.Kweli.Lakini,hata kama imani yangu ni ujinga yatosha kusaidia wanajamii wenzangu.Hata mimi nilisaidiwa.Kama hufahamu,mimi nilisomeshwa na Padre Mathias Mambo(sasa ni Marehemu) kuanzia kidato cha pili hadi cha sita.Nilisaidiwa nami najaribu kukusaidia.


Mjomba Ashura,tangu uanze kukaa Mailimoja-Kibaha kwa mama yako mkubwa,Immakulata,umekuwa na tabia ya kutohudhuria Shule.Nilipopata ripoti hiyo,nilikuita uje Visiga-Kibaha(nyumbani) ili niweze kuzungumza nawe.Ukaja.Tukazungumza.Nilijaribu kukuadhibu na kuondoa vikwazo ambavyo wewe ulisema ndivyo vikukwamishavyo kuhudhuria shule.Hatahivyo,bado waendelea na tabia hiyo ya utoro.Nikawaombe wakuambie kuwa ipo siku nitakuja huko ili unieleze sababu hasa ya kutokwenda Shule.Ukijiamini kabisa,umekaririwa ukisema:"na huyo mjomba Petro aje tu…nitamwambia kuwa sitaki Shule…kwani lazima?".Maneno yako hayo ndiyo yaliyonifanya mimi niandike waraka huu.


Mjomba Ashura,sasa naomba fursa nitafsiri maneno yako.Naanza na "na huyo Mjomba Petro aje tu".Maneno haya yaonyesha kukiri kwako mambo makubwa mawili.Kwanza,wakiri kuwa mimi najihusisha na maisha yako hasa ya kimasomo.Pili,wakiri kuwa mimi hutumia hata nguvu kuhakikisha unabaki kwenye mstari mnyoofu wa maisha.Lakini pia maneno hayo yaweza kutafsiriwa kama yaonyesha kiburi na dharau kwangu.Asante kwa hilo.Kuhusu maneno "nitamwambia kuwa sitaki Shule",wamaanisha uamuzi wako dhabiti wa kutotaka Shule.Nikiwa kama Mwanasheria,naheshimu sana uamuzi wako huo kama ndio wa mwisho na wa manufaa kwako.Ingawa ndio kwanza una miaka 13,nitakubaliana nawe.Ila,sitakuja wala kuonana nawe ili uniambie kuwa hutaki Shule.Nakuomba utumie busara zako kukaa mbali nami.Nitajitahidi pia.Naogopa kufanya tukio lisilovutia kwakuwa sitakuwa tayari kukusikia Mjomba wangu ambaye mama yako na ndugu zako wengine wajua madhara ya kukosa elimu ukitamka maneno hayo yanayoudhi na kupenya kwenye masikio yangu.Sitavumilia.


Mjomba Ashura,kuhusu maneno-swali "kwani lazima?",naomba nikujibu kama ifuatavyo.Elimu si lazima.Mimi ni mfuasi wa imani kuwa elimu ni kipaji…si jambo la kulazimishwa.Mbona wajomba zako Johnbosco na Deogratias;mama zako Severia,Immakulata na Scolastica hawana elimu ya kutosha zaidi ya ile ya darasa la saba? Si wanaiishi tu? Kwani kimeharibika nini? Ole wako kama una maswali hayo niliyotangulia kuyauliza kwenye akili yako.Hawa waliishi kwenye kipindi tofauti.Kulikuwa hakuna Shule za kutosha na hata pesa za kulipia gharama za masomo yao.Wako waliokusudia kuikosa kama wewe na wale ambao hawakukusudia.Wote sasa watamani hata kurudi darasani tena.Wangekuwa wewe wangehudhuria masomo kwa bidii….wasingekuwa watoro tena.Waulize wakuambie….Hawakuwa na Mjomba kama mimi ambaye yuko tayari kulipia gharama za masomo yenu.Hawakuwa na kimbelembele kama mimi.Sisi hatukukuzwa karibu ya mjomba,shangazi,mama mkubwa,mdogo,baba mkubwa wala mdogo.Sisi na wazazi wetu tu.Tofauti na sasa.Una wengi wanaokuzunguka na ‘kukukera'.Ndugu kibao.


Mjomba Ashura,nimalize kwa kusema uamuzi uliochukua au unaotaka kuuchukua ni wa hatari sana kwa maisha yako.Hautaweza kuishi mbali na Mjomba Petro.Yeye ni msaada mkubwa sana kwenu na kwako.Utammiss sana! Ukae ukijua kuwa kwa muda wote huo Mjomba Petro alikuwa hakubughudhi ila alikuwa akikujenga kimaisha.Tafadhali usibomoe uhusiano huo mwema na wa kindugu.




Ndimi Mjomba wako kwa maisha yako,

Petro Eusebius Mselewa



0713 111171
 
Dah, mrefu... ngoja ntarudi...
 
opps, nimekubip hiyo namba yangu inaishia ho.

Unaweka namba ya ukweli hapa? Dah ya nini sasa sie?
 
Aisee pole sana kwa changamoto za malezi; nazielewa ila naona umegive up mapema sana. Ungempeleka boarding ambapo wako strict na kwa kukosa company ya mitaani angesoma tu. She is just too young to give up on her!
 
Aisee pole sana kwa changamoto za malezi; nazielewa ila naona umegive up mapema sana. Ungempeleka boarding ambapo wako strict na kwa kukosa company ya mitaani angesoma tu. She is just too young to give up on her!

Boarding?? Ipi hiyo dada Kaunga?

Alafu hujasoma pale mwanzo vizuri..ameandika "Kiukweli,Waraka huu ulimrudisha mpwa wangu Ashura kwenye mstari na sasa anapaa kuelekea kwenye mafanikio.Sasa yuko Kidato cha Pili na anaongoza darasani."
 
Last edited by a moderator:
opps, nimekubip hiyo namba yangu inaishia ho.

Unaweka namba ya ukweli hapa? Dah ya nini sasa sie?

In case una mpwa wako unataka atumiwe barua:glasses-nerdy:
 

....ni kweli siyo kila Kosa ni lazima mtoto aonywe Kwa viboko...Waraka huu wa Kwanza, wa Petro Sura ya Kwanza na Mistari (verse) yake 10 hakika imenifundisha Kitu...

...bravo Mjomba Petro
 
Boarding?? Ipi hiyo dada Kaunga?

Alafu hujasoma pale mwanzo vizuri..ameandika "Kiukweli,Waraka huu ulimrudisha mpwa wangu Ashura kwenye mstari na sasa anapaa kuelekea kwenye mafanikio.Sasa yuko Kidato cha Pili na anaongoza darasani."

Aisee nilimiss au nilisahau ya hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
opps, nimekubip hiyo namba yangu inaishia ho.

Unaweka namba ya ukweli hapa? Dah ya nini sasa sie?

Mkuu Kongosho,waraka huu nimeuweka hapa kama ulivyojitokeza kwenye Blogs mbalimbali na gazetini.Samahani kama umekwazika kuiona nambari yangu
 
Last edited by a moderator:
Mjomba mzuri sana wewe......wajomba na maanti mpoooo
Ulezi si wa Baba na Mama tu
Bravoo Mjomba
 

Hongera mwanasheria! ila neno mjomba da umelitumia kimakosa sehemu nyingi
 
PETRO E mselewa aisee kumbe ni mbox tu???? Sijui kama unamjua mtu anayeitwa Maps na Mwanja???
 
Last edited by a moderator:
PETRO E mselewa aisee kumbe ni mbox tu???? Sijui kama unamjua mtu anayeitwa Maps na Mwanja???
Nawajua Mkuu,MAPS(Man Affecting Peoples) ameshafariki.Mwanja sina taarifa zake kamilifu.Hao watu ni hatari,hasa Marehemu MAPS.Ulimaliza pale lini Mkuu>
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…