Waraka wangu kwa Mkombozi wetu.

DMCT

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
2,281
2,000
Waraka wangu wa kwanza kutoka katika fikra zangu Finyu.

Glory to God, nawaombea wote uzima maana snipers wa siku hizi ni wataalamu wa kupindua risasi hata kama zimepigwa juu.

Mtikisiko na hofu kuu umetawala ndani ya nafsi za mamilioni ya Watanga nyikani walioamini mkombozi, jemedari,(niweke na kizungu Comrade), walie amini ametukuka kwa uweza wa Mungu kuja kuwakomboa Watanga hawa, huyu mtu aliinuka na kujinadi, kwa mazoezi ya viungo, na kuzungumza kwa shamrashamra lukuki, hali iliyo fanya kuzungumzwa katika kikundi changu pendwa pindi nikila ugali wangu na maharage yaliyo pecha pale Kwa ndugu zangu Kagoma ambapo nilikua nikirudi shule baba yangu ananiuliza kwa uchungu, "mwanangu umetoka shule au mgodini..?" Kutokana na vumbi jekundu lililosababishwa na miundombinu mibovu hasa barabara. Nilikaa kubishana sana na wenzangu kwamba sasa tunaacha kuTanga kwa maana mkombozi amekuja, nilipata imani sana na Mkombozi wa wanyonge.

Nayapenda maisha yangu, na nawaogopa sana "Watu wasiojulikana" Nasikia ni wataalamu sana wa kuchunguza mwili kwa vitendo. Pamoja na hayo, naomba niwasilishe niliyoyaona kama Mtanga nyikani katika huu usukumaji ligulurudumu wa Mkombozi wangu kwa Watanga nyikani wenzangu;

1. Demo class ni darasa la demo yaani majaribio, kwa mtazamo wangu finyu, hii demo class inatakiwa iwepo ili imfundishe anaye ongoza kwa kuwa wale "wakosa kosoaji" Wanaokosa baada ya kumkosoa mkombozi anayejitangaza, wasikosee bali wamkomboe katika utawala wake kwani atayajua matatizo ya wanyonge wake kupitia hawa "Wakosa wakosoaji"(wapinzani). Lakini hiki kitu hakipo na kwa sasa na kinaonekana kama kosa la jinai. Bora hata umchape mimba mwanafunzi, na sio kukosoa.

2. Nimesoma civics naomba ni apply hapa kidogo, kuna sifa ya mkombozi wa wanyonge ambapo yeye anafanya kweli " Anawanyonga". Sifa ya huyu Mkombozi anatakiwa akubali kuwa ni binadamu na anakosa na hivyo akubali kukosolewa.. Sasa ndugu yangu mnyonge mwenzangu ni kwamba wewe ni malaika (hata shetani malaika alikosa) huwezi kukosolewa na hivo tunyongwe kwa kukosoa, eti mkombozi wangu?

3. Unasisitiza tufanye kazi tusijadili siasa, tunakubali ndio, lakini kazini kutakalika ikiwa bosi wangu anabifu na bosi wake ambae wewe ndie bosi wake, nipigwe makofi, nipigwe roba ya kikekokeko, nitakuwa mfanisi kweli katika utendaji? Mkombozi!!!!

4. Nalifurahia sana kwa bashasha kuu niliunga mkono hoja juu ya huyu mdudu ulimuita "ELIMU BURE" kumbe sikuelewa vizuri, ukweli ni kwamba watoto wanatoka bure, wanaangukiwa na kuta za madarasa ya mwaka 1972 ambayo yalipata mgogoro na cement na pima maji mwaka 2005 mpaka sasa yanachekana na nyufa zinazo kasirika mwisho kutamani kuchukua roho za watoto wa wanyonge ambao wewe ndio mkombozi wao. Nafikiri watoto pia wanaogopa kukaa kwa madawati uliyopeleka maana walizoea kukaa chini na ndio maana Watu wakisema hakuna madawati unataka hawa watu "wasiojulikana" Wakawafanyie uchunguzi wa miili yao.

Sisiembuuu tuambiane nanyie mna waraka kama wangu?

Ahsanteni..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom