Siku ya leo imenipa mwanga mkubwa juu ya chama hiki baada ya kusoma tamko la chama ACT – Wazalendo juu ya maamuzi ya bodi ya wakurugenzi wa MCC kusitisha mahusiano na Tanzania. Kusema kweli imenishangaza sana chama kinachojinasibisha kama chama cha UJAMAA kimekiuka nguzo zake kuu kwa sababu tu ya mtazamo na maamuzi ya viongozi wake.
Kwanza lablda niseme hivi UJAMAA ni imani, imani ya kwamba Undugu na Umoja wetu ndio nguzo yetu ya maendeleo na kwamba hakuna mgeni anayeweza kutuletea maendeleo isipokuwa sisi wenyewe. Hii ni imani ambayo ndio haswa chimbuko la kudai UHURU wetu tusitawaliwe kiuchumi. Hatukuomba UHURU kwa sababu tulikuwa tumefungwa katika minyororo ama tulitengwa katika kupata haki za kibinadamu - Hapana. na haya ndio Castrol amekataa hadi jana akimwambia Obama kwamba - Hatuhitaji zawadi toka kwa MKOLONI. Maneno haya yanatokana na Imani sii swala la maskini jeuri!
Hivyo, hata sisi hatukuomba UHURU wa bendera, uhuru ambao kwamba mnajitawala wenyewe lakini bado mnatawaliwa Kiuchumi. Lengo kuu la Ujamaa ni kuondokana na kutawaliwa kiuchumi na ndio maana katika harakati za kujitawala kiuchumi ikazaliwa itikadi ya UJAMAA na KUJITEGEMEA inayokinzana na dhana ya kutawaliwa Kiuchumi na wakoloni, fikra hizo zikahamasisha wananchi wenyewe wachukue jukumu la kutaka kuendesha uchumi wa nchi zao kwa sababu wakoloni walikuja kukoloni nchi zetu sio kwa sababu walihitaji ardhi zaidi za kuishi wao, bali makoloni ya kuwekeza katika kukuza uchumi wa cnhi zao. Usipozingatia haya nawe ni msomi basi ndio katika maneno yale ya Nyerere alosema kwamba sio kila msomi ana akili wala sio kila mwenye akili ni msomi wengine ni wapuuzi tu!..WAPUUZI yaani IGNORANT! kama wale wanaohubiri Kuran na Biblia kumbe wanayoyafanya yao ni katika yale yaloharamishwa!
Sasa leo napo wasoma chama cha ACT –Wazalendo, chama ambacho kwamba nilidhani kweli ni WAJAMAA wamenipa mshtuko mkubwa sana kuona wapo tayari kukiuka principal zao kwa vipande vya rupia kutegemea misaada ambayo ndio msingi mkuu wa kutawaliwa kiuchumi. Sii Marekani, Jumuiya ya nchi za Ulaya wala Canada zinazoweza kutoa misaada pasipo kutazama kwanza interest zao na sidhani kama kuna mmoja wa viongozi wa ACT anafahamu interest za Marekani ama hiyo taasisi ya MCC zaidi ya kwamba wanatusaidia! Wanachokifahamu ni vitu gani wanavyotusaidia pasipo kujua, wao wananufaika na vitu gani toka kwetu? Hilo moja!
Pili, sidhani kama viongozi wa ACT wanafahamu undani wa itikadi hii inapofikia wao kutetea mashirika makubwa yanayoendesha uchumi wa nchi hizi kuwa msingi wa kujinufaisha wao kimaendeleo. Ujamaa (Socialism) kwa mapana yake ni falsafa inayopinga mapokezi ya mashirika makubwa kutawala uchumi wa nchi dhidi ya walio wengi. Nchi zetu bado zikipigana kuupata Uhuru wa kiuchumi, wakati nchi za magharibi ambazo tayari wamejitawala kiuchumi vyama vyao vya kijamaa vimejikita kupambana na wakoloni wa ndani ambayo ndio haya mashirka makubwa kutawala uchumi wa nchi zao yakiwaacha wananchi walio wengi maskini. Kwa hiyo ukoloni haukuwa nje tu hadi ndani mwao kuna Ukoloni. Leo unapotetea nchi kama marekani inayotujmia taasisi kama MCC kututawala kiuchumi wakatuletea makampuni kama Halliburton na Symbion nchini mnadhani hatutakuwa na matatizo ya kisiasa kwa kusimika vibaraka wake ili wanufaike kwa mafuta na gas!
Hivi kweli kwa akili zenu mnafikiri Marekani wanajali nani atakuwa rais wa Zanzibar kupitia kura za wananchi? Basi kama wangekuwa wazuri hivyo wa demokrasia wangekubali matokeo ya Misri, Palestina au hata Iraq katika uchaguzi mkuu ulopita! Kwa nini Marekani hao hao walikuwa against vyama vilivyoshinda na katika uchaguzi halali kabisa! It all comes to their Interest! Na Tanzania kwa utajiri tulokuwa nao lazima watatuchafua kama walivyoweza kuzibomoa nchi nyingine toka Russia, Somalia, Iraq, Libya, Sudan na sasa Syria! Utajiri wa Mafuta na gas tulokuwa nao kama hatutatumia AKILI zetu basi itakuwa laana kwetu.
Kama mnakumbuka Ufaransa waliiwekea vikwazo Rwanda miaka 14 ilopita baada ya uchaguzi wa Kagame ati anakiuka haki za binadamu na wala sio kwa sababu Kagame alikuwa dikteta mbaya sana kuliko kina Yahya Jammeh wa Gambia ama Obiang Mbasogo wa Equatorial Guinea ambao wamekubatiwa na Ufaransa miaka yote isipokuwa kwa sababu Kagame hakuna katika hesabu zao zakutawaliwa Kiuchumi. Na hata hawa Marekani miaka 7 ilopita nao wakamwekea vikwazo Utawala wa Kagame kwa kigezo kile kile cha haki za binadamu.
Nani leo anaweza kuinyooshea kidole Rwanda kwamba walipoteza mahusiano na nchi hizo! Rwanda imeteteleka kiuchumi ama ndio kwanza waliweza kutafuta mbinu zaidi ya kukuza umoja wao na kujitegemea wao wenyewe. Na hii ndio dhana ya vitisho wanayopenda sana kuitumia nchi za magharibi kutishia nchi maskini ambazo hadi leo wana Uhuru wa bendera tu hawajaweza kujitawala kiuchumi. Na hii ndio kazi kubwa ya wanasiasa wetu wanapotangaza siasa ya UJAMAA kwa maana pana zaidi ni kuikomboa nchi kutoka katika mizizi ya kutawaliwa kiuchumi.
Leo, ACT – Wazalendo kwa mapenzi yao ya Upinzani pasipo kujali misingi ya kiimani na kufuata kile wanachohubiri wamekuwa wa kwanza kupigania misaada ambayo kwanza binafsi sioni manufaa yake zaidi ya kuliweka taifa letu ktk lindi kubwa zaidi la Utegemezi. Hivi kweli tunashindwa kujenga barabara zetu hadi tutegemee misaada ya MCC ilihali usafiri ni miundombinu ya kwanza kabisa katika maandalizi ya kujitegemea kiuchumi.
Kuhusu Umeme, ni vyanzo vipi MCC wametuwezesha zaidi ya wao kutuletea Richmond na sasa Symbion ambayo inatukamua hadi tone la mwisho! Hata hiyo kusambaza Umeme vijijini hao MCC wapo Tanzania miaka mingapi ilopita kiasi kwamba leo ni asilimia chini ya 30 tu ndio wana umeme majumbani? Umeme wenyewe wa mgao na magenerata wakituuzia mafuta! Kweli tulihitaji na bado tunahitaji fedha za MCC tu kusambaza umeme nchini wakati hatuna vyanzo vyetu wenyewe vya kudumu! wao ndio wazalishaji umeme na wao ndio wanatusaidia kusambaza.. Mchumi yeyote ataiona faida inamlenga nani?
Nikirudi katika swala la Uchaguzi wa Zanzibar, ACT mnao ushahidi gani wamshindi zaidi ya kwamba mnafuata mkumbo? CUF wenyewe walitangaza kwa uhakika ushindi wa majimbo 20 kati ya 50, na hata kama projection ilionyesha wazi Maalim Seif kashinda bado tunatakiwa kutazama sharia inasemaje. Tuache makosa na mapungufu yote yalotajwa na Jecha ambayo sote hatuna ushahidi wa kutosha tunafahamu wazi Maalim Seif alijitangaza mshindi mapema kabla ya kutangazwa inyume cha sharia! Hili pekee ilitakiwa kufufuta Uchaguzina pengie ushindi apewe Shein, lakini Jecha na ZEC wakatafuta sababu nyingine za kufuta uchaguzi.
Sasa hatuwezi kupuuza sharia ambayo sote tunaijua kwamba Maalim Seif alikiuka tukamjengea hema la kutaka mshindi atangazwe kwa sababu tu tunaamini Maalim Seif alishinda na tunataka CCM itolewe madarakani. Na tunashindwa kujiuliza kwanini Maalim Seifalijitangaza wakati anajua sharia za uchaguzi? Kwa kuhofia CCM watachakachua? Sasa akijitangaza ndio ingeondoa uchakachuaji ama kupinga matokeo yoyote ambayo Jecha au ZEC ingetangaza. Binafsi yangu nitasema Jecha aliwashika mkono CUF kufuta matokeo ya uchaguzi laa sivyo kisheria Maalim Seif alitakiwa kuchukuliwa yeye hatua kali na iwe mfano kwa viongozi wengineo maaa Marekani na nchi zinazotumia mfumo wa wabunge wengi ndio hutangazwa mshindi kupitia hesabu ya kura zinavyohesabiwa na sii jukumu la Tume wala mwenyekiti kutangaza mshindi. Sisi tuna sharia zetu na tunafuata utaratibu wa Umaarufu kumpa mshindi na hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kutangaza wala kupinga matokeo yatakayo tangazwa na mwenyekiti. Sasa ikiwa mwenyekiti ana mamlka haya makubwa kabisa ambayo hata mahakama wala rais hana mamlaka ya kufuta matokeo aloyatangaza, ni nani mwenye mamlaka hayo kikatiba zaidi yake?
ACT – Wazalendo, achene hizi siasa za kutafuta umaarufu kupitia uchaguzi wa Zanzibar kwa sababu kuna makubwa zaidi ya kura unapoona nchi za magharibi zikijitwika mzigo! Wana lao jambo na hakika kesho yakijatokea ya kutokea mtajificha mbali kabisa na balaa litakalo wakumba wananchi na sii wa Zanzibar pekee bali balaa hilo lazima litavuka bahari na kuingia bara!