Waraka wa wazi kwa Prof. Ibrahim Lipumba

Waraka wa wazi kwa Prof. Ibrahim Lipumba

Acha kutukana humu jamvini wewe mpuuzi, iq yako ni sawa na zygote



nina uhakika wewe ni chekechea kwa lipumba na hata kujiita mchumi mwenzako ni upuuzi tu maana huna hiz sifa. Siku hizi hata walinzi mnajiita wachumi. Upuuzi wa aina yake huu. Na tangu lini umekuwa ukimsapo prof? Baada ya kujiunga na mabwana zenu aknia mbowe? Ni mara ngapi mmekuwa mkimdhihaki seif? Leo hii kwa kuwa anaendana na interest zenu ndo anaonekana anafaa? Eti unapenda kumpta ushauri, wewe nani mpaka umpe ushari? Eti ni aibu? Hiyo aibu umeiona wewe tu? Na hao nyumbu wenzako? Tuondolee hiki kinyesi chako hapa.
 
keynessian, kila mtu katika maisha huamua juu ya jambo hili au lile. Jukumu la kufikia maamuzi ni la mtu mwenyewe wala haliwezi kuwa la mashabiki wake. Hata kama ulimpenda Prof. Lipumba au hukumpenda, hii haiwezi kumfanya aamue kufuata matakwa yako au ya mtu mwingine yeyote. Katika taarifa yake wakati akizungumza na vyombo vya habari Prof. Haruna Lipumba alisema kuwa hajashawishiwa na mtu yeyote. Mtu unapoamua juu ya jambo lolote huna budi kuwajibika juu ya maamuzi yako. Prof. anajua hivyo (you must be responsible for your own decisions) hivyo siyo jukumu lako kuwajibika juu ya maamuzi ya Prof. Lipumba.
Kinachotoa heshima kwa mtu ingawaje wote wanaamua ni ubora wa maamuzi. Ubora wa maamuzi hupimwa kwa kuangalia matokeo yake. Lakini si kila matokeo huonekana mapema, mengine husubiri muda upite. Mbowe kama kiongonzi wa chama cha siasa, ametoa maamuzi, na Prof. Lipumba kama kiongozi na msomi ametoa maamuzi. Wote wawili wana sababu zilizowaongoza kufikia maamuzi waliyoyafikia. Tungoje matokeo.
Kudai Prof. angeamua kama unavyotaka wewe ni sawa na kusema asiwe Prof. Lipumba awe keynessian kwa kipindi hicho na baada ya matokeo umkane kwa kusema aliamua mwenyewe wala wewe huhusiki. Ni fikira za jaha. Prof. wa kiwango cha kuamua, Lipumba hawezi kufanya hivyo. Hawezi kuuza heshima yake aliyoijenga kwa muda mrefu kwa bei ndogo ya kukufurahisha wewe. Never in earth.
Habari za wasaa huu mchumi mwenzangu Lipumba,

Tunaheshimu uamuzi wako wa kujiuzulu uliouchukua hivi karibuni, ni simanzi kubwa kwa wanaharakati wa mabadiliko nchini.

Kitendo hichi mpaka sasa kimezua maswali maswali mengi kuliko majibu,kimefanya juhudi zako zote za kupigania mabadiliko kuwa sawa sawa na hamna kitu, lakini pia umejivunjia heshima yako kubwa ulijiwekea kwa muda mrefu wananchi walitarajia mtu mwenye busara kama wewe ambayo umejitokeza mara nyingi kuwania nafasi ya urais kwamba utakuwa ni mtu mwenye busara na hekima kubwa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi kwa kutambua athari ya maamuzi yako kwa sasa na baadaye.

Ni aibu sana kwa mwanazuoni mkubwa kama wewe kutoa excuse kwa kusema dhamira yangu inanisuta. Vipi kama ungekuwa kiongozi mkuu wa nchi ni maamuzi mangapi ya hovyo ungeyefanya na kusema dhamira yako imekusuta?

Hii wanazuoni wanaiita intellectual negligence, umeeonesha udhaifu mkubwa sana kwenye maamuzi,umedhalilisha taaluma na ninasema bila kumungunya hauna sifa ya kuwa kiongozi.

Aidha nipende kutoa shukrani kwa dhati kwa watanzania waliokukataa kwenye sanduku la kura miaka yote uliyogombea, lakini lingine ambalo ni likubwa nawashukuru sana viongozi wa CUF wakiongozwa na Maalim Seif pamoja na wanachama wote wa CUF kwa kukupuuza wewe pamoja na kitendo chako cha kujiuzulu.

Ushauri wangu kwako: Kuendelea kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kuponda UKAWA ni kuendelea kujivunjia kale kaheshima kadogo kalichobakia,ingekuwa busara zaidi kama ungekaa pembeni na kuwa mtazamaji.

Ni hayo tu.

Keynessian!
 
Yaan huu mwaka ni mabadiliko tu..hata ukawa agombanie chizi..tunampa au waweke jiwe tutakipa jiwe kura...tumechoka sana na ccm ...were so tired ,tired bas jaman...ccm wapumzike tutajua mbele ya safar
 
Yaan huu mwaka ni mabadiliko tu..hata ukawa agombanie chizi..tunampa au waweke jiwe tutakipa jiwe kura...tumechoka sana na ccm ...were so tired ,tired bas jaman...ccm wapumzike tutajua mbele ya safar

watu wanaongoza miaka zaidi ya 50 wanafunzi wanakaa chini katika nchi yenye maziwa na asali.tumechoka tumechoka.
 
Back
Top Bottom