Fredrick J Mbwambo
Member
- Jul 3, 2020
- 6
- 97
WARAKA WA WAZI KWA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA
MH.FREEMAN A. MBOWE
Mh. Mwenyekiti pole na majukumu ya ujenzi wa demokrasia nchini, Zaidi pole sana na shughuli za uchaguzi zilizokoma takribani wiki nne zilizopita huku majeraha ya ukiukwaji mkubwa wa demokrasia, uvunjwaji wa haki za raia, ndugu zetu kuuwawa, kufungwa na viongozi wetu wakuu ikiwemo Mh. Lissu na Mh. Lema kuomba hifadhi za kisiasa ili kujinusuru wao na familia zao kutokana na utawala wa mkono wa chuma yakiwa bado hayajapona.
Mh Mwenyekiti umekuwa nguzo imara na kinara wa kuongoza mapambano ya kudai haki, demokrasia na maendeleo ya watu kwenye Taifa letu, navutiwa sana na umahiri, ujasiri, uvumilivu, utu, upendo, moyo wa kusaidia wengine na uongozi wako bora uliotukuka tangu kuasisiwa kwa misingi ya CHAMA chetu mwaka 1992.
Ukiwa kijana mdogo kabisa haikukuzia kuongoza kurugenzi ya vijana kwa ufanisi
kubwa chini ya mwenyekiti wa kipindi hicho mzee wetu Mh. Edwin Mtei ambae alikulea katika misingi imara ambayo vizazi vya leo na vijavyo vina chakujifunza na kujivunia.
Mh. Mwenyekiti nakuandika waraka huu nikiwa na huzuni isiyokoma tangu nisome taarifa za viongozi wa BAWACHA wakiongozwa na Mh. Halima Mdee kufanya maamuzi ya kwenda Bungeni kuapa kama Wabunge wa viti maalumu watokanao na CHADEMA huku nikiwa kwenye wimbi kubwa la sintofahamu kama maamuzi hayo yanabarka za chama au laa.
Kamati kuu ya Chama chetu mara zote imekuwa ikifanya maamuzi sahihi na muhimu kwa mustakabali wa Kuhami Demokrasia ya Taifa letu na Kamwe sijawahi kutilia shaka maamuzi ya kamati kuu iliojaa viongozi makini na wenye weledi, na hata mlipokutana na kuyakataa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa mwaka huu ilikuwa ni sehemu ya maamuzi sahihi na muhimu sana kwani wananchi na wapenda mabadiliko walifurahishwa na maamuzi yale. Je! ni nini kimetokea?
Maamuzi yamebadilika? Kama hayajabadilika kuna viongozi ndani ya Chama wamekuwa
wakubwa kuliko Chama? Natumai hakuna na kamwe hatakuja kutokea.
Mh. Mwenyekiti ni kweli katibu wetu wa vijana Mh. Nusrat Hanje ametoka gerezani kutokana na juhudi zetu, na wingi wa kelele zetu? Hashaa! Mtawala alimuweka gerezani kinyume na utaratibu, kamtoa kinyume na utaratibu na kisha kamzawadia Ubunge kinyume na utaratibu. Sisi tuliojitofautisha kwa sera na itikadi natumaini tutafuata utaratibu kwa mujibu wa katiba kwa manufaa ya kesho ya Chama chetu
Mh mwenyekiti mwisho kabisa nimalize kwa kutoa ushauri wangu kwako na kwa CHAMA;
1. Natambua chama chetu ni miongoni mwa vyama vyenye intelijensia imara hivyo niombe hatua za haraka ziwe zinachukuliwa dhidi ya wale wote wanaopanga kuasi,kuhujumu,au kuzorotesha maamuzi ya chama kabla wao hawajachukua hatua
zitugharimuzo, kutukatisha tamaa na kuturudisha nyuma.
2. Wote walio kwenda kinyume na makubaliano ya KAMATI KUU wafutwe uanachama mara moja ili ku restore Imani ya wananchi kwa chama chetu, na pia maamuzi hayo. yataheshimisha dhamira ya mamia ya ndugu zetu waliouwawa, kuteswa na kutupwa
magerezani.
3. Chama kiunde mfumo wa kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli zake kwani wananchi kwa mapenzi mema wameonyesha wako pamoja na sisi na katu hawatakubali fedha zitokanazo na dhuluma,uonevu na damu za ndugu zetu.
4. Uhusiano mzuri wa wanachama ni ule tu unaoweka maslahi ya Taifa mbele na sio maslahi binafsi, na
5. Chama kiondoke katika fikra za mikakati na kisha kigeukie harakati za vuguvugu la kudai Katiba Mpya bila kuchoka hadi ipatikane, kwani ni wazi Demokrasia ya Vyama vingi haiwezi kutekelezeka chini ya KATIBA iliyoandaliwa mahususi kwa mfumo wa Chama
kimoja. Mh. Mwenyekiti mimi sio sehemu ya maamuzi kwenye chama lakini nilijifunza busara ni kutokunyamaza wala kutulia pale uyapendayo ukihisi yaenda mrama yapasa kusimama na kushauri, kama ulivyofanya mwaka 1995 pindi Mh. Edwin Mtei na Mh. Bob Makani walipogombea urais ndani ya CHAMA na baadae kuonekana kukubalika kwao na uimara wao watakipasua na kukigawanya CHAMA uliandika waraka kushauri kwamba WOTE wasigombee bali wamuunge mkono mgombea wa NCCR, ushauri ambao ulikuwa na tija na unatujenga mpaka leo hii. Mungu ibariki CHADEMA, Mungu Ibariki Tanzania.
Nakutakia Kheri na Maisha marefu yenye Furaha.
FREDRICK M. JUSTINE