Waraka wa wazi kwa Dkt. Kitima

Waraka wa wazi kwa Dkt. Kitima

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
319
Reaction score
755
Tumsifu Yesu Kristo,

POLE na majukumu, kwako Katibu mkuu wangu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC, Rev.Dr.Charles Kitima ni mwalimu wangu wa chuo kikuu SAUT na Pia binafsi nimesomeshwa na Kanisa Katoliki, Mimi ni muumini mlei wa Kanisa Katoliki natokea Kanisa Kuu la mtakatifu Antony wa Padua Parokia ya Nyarubele Jimbo katoliki la Geita, Paroko wangu ni Rev.Pd.Thomas Kabika Biringi, na Askofu wangu ni Most.Rt.Rev.Flavian Matindi Kassala, nimebatizwa na kupewa Kipaimara.

Nina haya machache ya kushauriana na Padri wangu msomi wa Falsafa ya Juu ya Sheria za Kanisa Katoliki (Canon Law) Dr. Kitima kabla ya hapo aliwahi kuwa Mwanasheria wa chuo cha SAUT na baadae akawa Vice Chancellor lakini Akiwa VC -SAUT katika kipindi chake chote Walifariki wanafunzi zaidi 160 katika kipindi cha uongozi wake kwa matatizo mbalimbali, ikiwemo magonjwa na ajali, mbaya zaidi hajawahi kutoa takwimu hizi za vifo,

Taarifa yake ya jana ni taarifa ile ile iliyotolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, aliyoitoa tarehe 26/01/2021 Kwa maaskofu nchini, kwahiyo amejiweka Kuwa msemaji wa kanisa na kutoa twakwimu za vifo vya Corona bila Ushahidi,

Takwimu za sensa ya kanisa katoliki mwaka 2020 Roma Ina idadi ya Waumini walei, watawa na makasisi zaidi ya milioni 12 nchi nzima Ina majimbo zaidi ya 34 na majimbo makuu zaidi ya 7, Hi Sawa na nchi ndani ya nchi, Inakuwaje mtu ahoji Idadi ya vifo vya watu 25 na masista 60? nashauri ajibiwe na Muumini wake ili ibakie huko huko kwenye mambo ya kiimani, lengo lake ni kuweka takwimu ili kujenga taharuki kwenye Umma wa watanzania na kuwatia Hofu, hii ni nje kabisa ya maadili ya kiongozi wa kiroho kufanya hivo, kazi ya kanisa ni kuondolea Hofu waumini na kuwapa matumaini ya maisha baada ya kifo,

Binafsi nimesikitika Sana! Lakini naomba kumjibu vizuri kama nitahitajika, Naomba roho wa Mungu anipe hekima ili nisiende kinyume na mapenzi yake ili kutekeleza Haya, Dhamana na utume wa waamini walei ndani ya Kanisa: Ni muda wa vitendo zaidi!

Mkutano wa Chama cha Vijana Wakatoliki Hispania: 1 Agosti hadi tarehe 4 Agosti 2019, huko Avila, nchini Hispania: Kauli mbiu “Kutekeleza ndoto ya Mungu; majiundo ya waamini walei Parokiani” Dr. Ghison anasema, walei ni mhimili wa Kanisa kwani, wanaitwa kutekeleza: Ukuhani, Unabii na Ufalme wa Kristo katika maisha yao, kama sehemu ya mchakato wa kuyatakatifuza malimwengu.

Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Akiwa Vatican alieleza kuwa Dhamana na utume wa waamini walei ndani ya Kanisa kwa namna ya pekee, ni matunda ya maadhimisho ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican unaobainisha: wito, utume na dhamana ya waamini walei katika kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu, kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa Ufalme wa Mungu unaofumbatwa katika misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa dhati.

Waamini walei ni wadau pia katika ujenzi wa Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa! Dr. Linda Ghisoni, Katibu mkuu msaidizi, Idara ya Walei, Baraza la Kipapa la Walei wa Kanisa Katoliki Familia na Maisha katika hotuba yake ya kufunga mkutano wa Chama cha Vijana Wakatoliki Nchini Hispania uliofunguliwa tarehe 1 Agosti hadi tarehe 4 Agosti 2019, huko Avila, nchini Hispania, kwa kuongozwa na kauli mbiu “Kutekeleza ndoto ya Mungu; majiundo ya waamini walei Parokiani” anasema, waamini walei ni mhimili wa Kanisa kwani, wanaitwa kutekeleza: Ukuhani, Unabii na Ufalme wa Kristo katika maisha yao, kwahiyo kuwapa matumaini ni Jukumu la Padri na siyo kuwatia hofu na kuwakatisha tamaa.

kama sehemu ya mchakato wa kuyatakatifuza malimwengu. Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanasema, walei, kama washiriki wa huduma ya Kristo kuhani, nabii na mfalme, wanayo nafasi hai katika maisha ya Kanisa na katika utendaji wake. Ndani ya jumuiya za Kanisa matendo yao yanahitajika sana, kiasi kwamba pasipo haya hata utume wenyewe wa wachungaji huwa hauwezi kufikia mafanikio kamili.

Maana walei wenye roho halisi ya kitume, kama wale wanaume na wanawake waliokuwa wakimsaidia Mtume Paulo katika kueneza Injili (Taz. Mdo 18:18.26; Rum 16:3), wanawakirimia ndugu zao yale waliyopungukiwa, na wanaburudisha roho za wachungaji na za waamini wengine wa taifa la Mungu (Taz. 1Kor 16:17-18). Tangu baada ya Mtaguso Mkuu wa Vatican, kumekuwepo na uanzishwaji wa mashirika na vyama vya kitume sehemu mbali mbali za dunia na vyama hivi vimesaidia kukuza na kudumisha ari na moyo wa kimissionari, malezi na majiundo makini ya maisha ya:

lmani na uadilifu, Sakramenti za Kanisa pamoja na maisha ya sala; mambo muhimu yanayopaswa kumwilishwa katika uhalisia wa maisha ya waamini, kama kielelezo cha imani tendaji!

Adhimisho la Fumbo la Ekaristi Takatifu chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa na hiki ni kiini cha maisha ya Parokia. Kimsingi, Fumbo la Ekaristi Takatifu linaadhimishwa siku ya Bwana; Jumuiya ya waamini inapopata nafasi ya kusikiliza, kutafakari Neno la Mungu na hatimaye, kutumwa kutangaza na kushuhudia matendo makuu ya Mungu katika uhalisia wa maisha yao, kama kielelezo cha imani ntendaji! Neno Parokia, linapata asili yake kutoka katika lugha ya Kigiriki yaani “παρоικια” maana yake “Ujirani”.

Kumbe, kwa maneno machache, Parokia ni kitovu cha maisha na utume wa Kanisa, mahali pa kuinjilisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu, tayari kutoka kifua mbele kutangaza furaha ya Injili; huruma na upendo wa Mungu. Mababa wa Kanisa wanasema, sasa umefika wakati wa kuangalia ya mbeleni kwa matumaini zaidi, ili kukabiliana na matatizo, changamoto na fursa zinazoendelea kujitokeza miongoni mwa waamini walei ndani ya Kanisa Katoliki, ili waendelee kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kumtangaza na kumshuhudia Kristo Yesu, Mkombozi wa Ulimwengu.

Mababa wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Vijana kwa mwaka 2018 wamekazia umuhimu wa Kanisa kufundisha maisha mapya na utume wa Parokia, ili kuleta mvuto na mashiko kwa vijana wa kizazi kipya pamoja na waamini katika ujumla wao, ili kuwajenga kiimani na kuwatia moyo hasa katika sakramenti ya kitubio na mpako wa wagonjwa, ili kujenga familia ya Mungu inayowajibikiana katika: imani, matumaini na mapendo.

Dr. Linda Ghisoni anasema, waamini walei kamwe hawataweza kuyachachua na kuyatakatifuza malimwengu ikiwa kama watashindwa kutoka katika undani wa maisha yao kuwa kweli ni chumvi ya dunia na nuru ya mataifa. Mkutano mkuu wa Chama cha Vijana Wakatoliki Nchini Hispania umehudhuriwa na waamini walei 750 kutoka katika Majimbo 45, huku wakiwa wameambatana na Maaskofu pamoja na Mapadre wao. Waamini walei ndani ya Kanisa wanapaswa kutambua dhamana na wajibu wao kama wabatizwa, yaani watu waliozaliwa upya kwa maji na Roho Mtakatifu; wanao wajibu na haki zao msingi zinazopaswa kumwilishwa katika maisha na utume wa Kanisa.

Kimsingi wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo mintarafu uhalisia wa maisha yao. Waamini walei daima wajibidishe kuchota utajiri na amana ya maisha yao ya Kikristo kutoka katika: Neno la Mungu, Sala, Sakramenti za Kanisa pamoja na Mafundisho Jamii ya Kanisa, dira na mwongozo wa jinsi ya kuyatakatifuza malimwengu. Waswahili wanasema, “kitu kizuri na chema, kula na ndugu yako”. Waamini walei watambue kwamba, amana na utajiri huu wanapaswa kuwashirikisha pia jirani zao kama sehemu ya mchakato wa majadiliano ya kidini na kiekumene; katika kuyatakatifuza maeneo ya kazi pamoja na utume wa familia. Waamini walei wakiwa wamepyaishwa kutoka katika undani wa maisha yao,

wanaweza sasa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa huruma, upendo na msamaha wa Mungu; watu wenye wenye uwezo wa kusikiliza kwa makini na kujibu kilio cha maskini wanaowazunguka; watu wanaoweza kuendeleza majadiliano katika ukweli na uwazi; ukarimu na upendo kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kwasababu ya Hofu ya ugonjwa wa COVID-19

Upya wa maisha unawataka waamini walei kujenga na kudumisha umoja, upendo, mshikamano na mafungamano ya dhati na viongozi wa Kanisa, lakini Dkt. Kitima anatia Hofu waamini walei, ili kuwajibika barabara katika maisha na utume wa Kanisa, kila mwamini akijitahidi kutekeleza wajibu wake. Dr. Linda Ghisoni, Katibu mkuu msaidizi, Idara ya Walei, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha katika hotuba yake ya kufunga mkutano wa walei nchini Hispania, amewaangalisha kuwa macho dhidi tabia ya kudhani kwamba, wanaweza kufanya yote kwa nguvu na jeuri yao, kwa kumweka Mwenyezi Mungu pembezoni mwa vipaumbele, sera na mikakati ya maisha yao.

Katika mtindo na mwelekeo kama huu vi vigumu sana kuweza kutekeleza ndoto ya Mungu katika maisha yao. Mwenyezi Mungu apewe kipaumbele cha kwanza katika sera na mikakati ya shughuli za kichungaji maparokiani na majimboni. Kwa njia hii, waamini walei wataweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu hapa duniani.

Kishawishi kingine ni kile cha kuendelea kubaki wakiwa wanaelea katika ombwe, bila kuzama na kumwilisha maana ya Kanisa na umuhimu wa malezi na makuzi ya awali na endelevu kwa waamini walei. Utakatifu wa maisha ni ushuhuda wenye mvuto katika utume wa Kanisa.

Changamoto na matatizo ya Covid-19 na fursa mbali mbali zinazoendelea kuibuliwa ndani na nje ya Kanisa, ni mahali muafaka ambapo waamini walei wanaitwa na kutumwa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Habari Njema ya Wokovu na kupambana na majanga yaliyotabiliwa kwenye kitabu cha Luka 21:10-11.

Waamini walei wasikatishwe tamaa na dhuluma, nyanyaso na magumu wanayokabiliana nayo katika maisha na utume wao hapa duniani, bali waendelee kusimama kidete kama mashuhuda wa Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo. Huruma na upendo wa Mungu uwaimarishe na kuwapyaisha kutoka katika undani wa maisha yao na siyo kuwaondolea tumaini Jema kwa vitisho vya Corona,

Kanisa Katoliki linaamini katika harusi tatu, a) Kuzaa na kuzaliwa b) Kuoa na kuolewa c) Kifo, Yesu Kristo alipokufa msalabani tulikwishaokolewa na hakuna haja ya kupewa Hofu ya kifo kutoka kwa Kasisi Dkt. Kitima.

Je, Father Kitima anatii mamlaka?

Kitabu cha Warumi 13:1-7
Neno: Bibilia Takatifu
Kutii Mamlaka

1 Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

6 Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. 7 Wal ipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.

Mwisho, Polisi haina mamlaka ya kutolea ufafanuzi afya za watu kama anavyodai Kasisi Dr.Kitima, Wizara ya Afya imeshatoa mwongozo wa kufata ili kujikinga na maambukizi ya Covid-19, tumpuuze Dr.Kitima kwasababu siyo Daktari wa afya ya Jamii, bali ni Daktari wa kiroho na msomi wa Sheria za Kanisa.
Tufuate mwongozo wa watalaamu na siyo vinginevyo.

HOFU NI UGONJWA MWINGINE MKUBWA KULIKO COVID-19.

Tumsifu Yesu Kristo.
Imetolewa leo 04/03/2021
Muumini Mlei Kindakindaki wa Kanisa Katoliki
Budodi Jelard L
Jimbo Kuu la Daressalaam, Tanzania.
 
Umeandika mambo mengi, lakini hoja yako kuu ni moja tu. Hamtaki kusikia mawazo tofauti na yale mnayo yapenda nyinyi. Hii nchi siyo mali yenu. Waacheni watu waongee!! Khaa

Unahoji kama huyo Padre anatii mamlaka!! Mamlaka gani? Mbona hata nyinyi tulio wapa hayo mamlaka hamtutii? Zaidi tu ya kutukejeli na kutusimanga?
 
Unaposema kipindi chake chote hapo SAUT unaongelea kipindi cha muda gani, maana juzi ameongelea kipindi cha miezi 2, Maaskofu 25 masister na manesi 60 wamefariki, jumla ni uhai wa watu 85, kweli idadi yote hiyo ya vifo kwa kipindi cha miezi miwili hamutaki mtu aongee kwa mashaka?
Tuna shida mahali fulani, tena shida kubwa tu.
 
Padre kutokana na majukumu yake, ana nafasi kuu nne.
1. Mchungaji
2. Mwalimu
3. Nabii
4. Kuhani.
Sasa Kama Nabii, ana wajibu wa kuonya, kukumbusha na kupongeza. Mwandishi jifunze kusimamia kweli. Kanisa katoliki limejengwa juu ya misingi ya Kweli.
Umeandika Porojo nying lakin haziendani na mada yako.
 
... Inakuwaje mtu ahoji Idadi ya vifo vya watu 25 na masista 60?
Ungemalizia "ndani ya miezi miwili kwa tatizo la corona", hapo ungekuwa umemnukuu vizuri kama alivyoongea. Lakini bado haujachelewa. Kabla thread haijaenda mbali, edit uandike mapadri 25 sio watu 25, maana isije ikachukuliwa watu wote kwa ujumla, halafu uandike ndani ya miezi miwili
 
Ni mwalimu wako amekufundisha ilikuwa ni adabu na utii ungemtafuta na kuketi nae mkazungumza alafu ungekuja kuandika ukiwa umepata maoni yake pia sasa kuja kumsema hapa wakati yeye hata toa au kijibu hoja zako ni kumuonea ,umesema chuo walikufa watu 160 je ilikuwa ni nimonia?maana msingi wa huyo kiongozi ni tatizo la nimonia na jinsi serikari inavyopiga danadana
 
Umejieleza kama mkatoriki lakini kitu cha ajabu hufahamu kwanini Padri Kitima anaongea kama nani na pia hufahamu hata majukumu ya TEC.

Padri Kitima haongei kama yeye binafsi bali anaongea kama katibu wa TEC na kuna kipindi Kadinari Pengo aliwahi kuongea na waandishi wa habari akawaambia kuwa sio kila askofu, Padri hata yeye akiongea ni msimamo wa kanisa katoriki Tanzania bali wenye mamlaka ya kutoa msimamo wa kanisa katoriki ni TEC.

Ndio maana hata waraka wa kanisa unatolewa na TEC lakini kwa maelezo yako pamoja na kutaja mapadri wako yanaonyesha wazi wewe ni mtu unayejifanya mrc wakati maelezo yako yanapingana .
 
Na Mimi alichonishangaza Doctor huyu ni kuelekeza lawama kwa serikali na wakati huohuo kuwa kipofu wa wajibu wake na wa kanisa!

Kanisa lilishatoa waraka wa maelekezo kwa wakleri na walei juu ya umuhimu na namna ya kujikinga na korona! Mimi ni mkatoliki ninayehudhuria misa kila jumapili lakini makanisa tofauti kulingana na ratiba yangu, hivyo tangazo hilo nililisikia makanisa tofauti niliyohudhuria.

Kinacho nisikitisha ni kwamba makanisa mengi ya RC hayana mpango kabisa wa kutkeleza waraka huo. Waumini wanarundikana kanisani na kwenye shughuli nyingine za kanisa bila tahadhari yeyote. Hakuna cha barakoa (labda upende mwenyewe), hakuna cha kunawa mikono na waumini wanajazana kwenye bench bila kuacha nafasi.

Viongozi wapo, Dr Kitima yupo, tena Katibu wa TEC, mwenyekiti wa Baraza la maaskofu yupo, maaskofu wapo, mapadre wapo! Kinachonishangaza Dr ana guts gani za kunyoshea vidole wengine( japo kiujanja) wakati mwenyewe ameshindwa kuchukua hatua kwenye himaya yake ambayo ana mamlaka nayo?

Kwa kweli hana moral authority ya kukosoa. Asidondokee kwenye siasa za Jamaa zetu ambao wana kosoa wakati wenyewe hawachukui hatua za kujikinga. Hao iko wazi wanatafuta political mileage.
 
Takwimu za sensa ya kanisa katoliki mwaka 2020 Roma Ina idadi ya Waumini walei, watawa na makasisi zaidi ya milioni 12 nchi nzima Ina majimbo zaidi ya 34 na majimbo makuu zaidi ya 7...
Ili kujenga hoja za kuutetea uongo hapa ndo ukaona uifanye entry point yako. Alitaja mapadri waliofariki kwa changamoto ya upumuaji ni 25 na masista 60. Wewe unasema watu 25 na masista 60 je kuna masista a,bao sio watu?
 
Mkuu Kanisa kanisa Katoliki ni Tasisi kama ni hivyo Padri ni Mjumbe.

Pia kama ww ni mkatoliki kweli haya maandishi yanaweza yakawa mabaya kwako umeandika kwa mihemko Padri Kitima akikukung'utia Mavumbi majibu yake unayajua ni mpaka kizazi cha mwisho.

Mwombe Padri Msamaha Ndugu achana na Mihemko
 
Unafiki wa aina hii ndio unaoliangamiza Taifa letu.

Zamani nilikuwa naamini kuwa watetezi wa ujinga wa Serikali ni waumini wa CCM, lakini huu wa sasa una harufu ya Ukabila. Harufu ya Usukuma.

Hii tabia ya kutetea makosa yanayofanywa na Magufuli, ambayo hata watoto wadogo wanaona kuwa siyo sahihi, mtakuja kuijutia.
Fahamuni kwa uhakika kuwa Mwenyezi Mungu hadhihakiwi.

Haya maneno ya kuikana korona tuliyasikia sana yakitamkwa na aliyekuwa Rais wa Burundi, hayati Pierre Nkurunziza. Aliwafukuza watumishi wote wa WHO na kuamuru waondoke Burundi.

Wakaondoka.
Yaliyotokea sote tunayajua.
Acheni kukufuru kwa kulitukana Kanisa Katoliki.
 
Usiondoke rudi hapa jukwaani utuambie Mungu aliyewaweka mafashisti Hitler na wenzake ni Mungu huyo aliyesema tutii mamlaka kwani zimewekwa naye. Je, hao wanaopora kura za wananchi na kujiweka madarakani nao tuwaone wameweka na Mungu?

Huu ni wakati muafaka unifafanulie wale wanasiasa tunaowaona wakisimama anapotakiwa kusimama padri na kuanza kutuhubiria mambo ya nje ya kanisa ni lini wewe utalikemea hilo, au hilo ni sahihi.

Korona ipo na kanisa lilikuwa likiwaelezea waumini wake na mwenye kumsikia amemsikia kwa hiari yake.

Mwisho mbona unatusemea sisi wakati hatukuchagua!
 
Back
Top Bottom