Waraka wa pasaka toka kwa mchungaji wa Pentekoste

Waraka wa pasaka toka kwa mchungaji wa Pentekoste

Kiootz

Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
17
Reaction score
21
WARAKA WANGU KWA VIONGOZI WA DINI KATIKA SIKUKUU YA PASAKA 2018

SALAAMU

Kwanza kabisa ninawasalimu wote katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na pia nina amini kuwa ujumbe huu utawasaidia baadhi ya Watanzania wenye nia njema nai chi yetu.

UTANGULIZI.

Nianze kwa kusema ni masikitiko yangu kama kiongozi wa kiroho kuona kama baadhi Baba zetu wa Imani kama vile baadhi ya Maaskofu na Wachungaji amabao Mungu amewajjlia Neema ya Utumishi na Hekima za Kimungu kuanza kupanda Chuki za Kisiasa ndani ya jamii za awatoto wa Mungu wanaowaongoza.

Napenda nitumie nafasii kuwakumubsha kama kiongozi mwenzenu, Biblia inasema katika Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi 13:1, Kila Mtu aitii Mamlaka iliyokuu, kwa maana hakuna Mmalaka isiyoto kwa Mungu, na ile iliyopo Imeamriwa na Mungu. Biblia haijasema tutumie Madhabahu mbele ya Waumini wetu kumkosoa mwenye Mmalaka aliyewekwa na Mungu. Biblia imesema katika1THIMOTHEO 2:1-2, Basi kabla ya mambo yote nataka Dua na Sala na Maombezi na Shukrani zifanyike kwa ajiri ya watu wote kwa ajiri ya Wafalme na wenye Mmalaka.

Kwahiyo, Biblia haijasema tuandike nyaraka za Uchochezi, kulaumu Kiongozi wa Nchi na Kumkatisha tama. Nataka niwakumbushe baadhi ya Baba zetu wa Imani, Maaskofu na Wachungaji kuwa Mungu humuandaa Mtawala. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, alichaguliwa na Mungu hata kabla misingi ya Ulimwengu huu kuwepo, hata yeye haukujua. Yeremia 1:4-5 inasema, “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa..”

Ni jambo la kusikitisha ,kuhuzunisha na la aibu sana kwa Baba zetu Maaskofu na Wachungaji, kumchafua mtu na kumnenena mabaya mtu amabaye Mungu alimchagua toka ili awe Kiongozi wetu kwa wakati. Na pia nataka niwaeleleze kuwa Rais Magufuli hakuletwa Mdarakani na Wakristo bali aliletwa Madarakani na watu wote. Mungu haangalii Sura, kabila, Elimu wala Umbo BaIi Mungu anaangalia Moyo. Na Moyo wa Rais Magufuli ni Moyo wa Kuwasaidia Watanzania Maskini na Wanyonge.

Mwanzo 12:3, Mungu akamwambia Ibrahimu,atakayekubariki ntambariki na atakayekulaani nitamlaani. Kauli ya kwanza ya Rais wetu baada ya kuapishwa alisema, “Watanzania tumtangulize Mungu mbele…” , “Mimi ni Mtumishi wa Wanyonge……”, “Nataka Tanzania iwe Nchi ya Viwanda..” ‘tujenge Reli ya Standard Gauge…”. Akasema, “Nataka Elimu kuanzia Shule ya Msingi na Sekondari itolewe bure…”

Mambo ambayo hakuyasema, Hakusema yeye anakuja kukandamiza haki za Watanzania na kuwauwa kwenye jukwaa la Kisiasa, Misikitini au Makanisani. Hakusema, atafunga Makanisa au kutoza kodi Zaka na Sadaka za Waumini, hakusema ataingilia haki ya kikatiba ya Uhuru wa kuabudu kwa mtu yeyote katika Nchi hii. Naomba tumuogope Mungu.

Ni jambo kusikitisha na aibu kubwa,Tunapombeza Rais wetu mpendwa kwa kusambaza Nyaraka za Uongo na kumuumiza, kumbuka Biblia imesema katika Kitabu cha Zakaria 2:8, “Amgusaye mtumishi wangu amegusa mboni ya jicho langu”. Mfalme Daudi naye alijua thamani ya Sauli, hakumfanyia Ubaya hata katika makosa ambayo Sauli aliyafanya. Viongozi wa Dini tuhubiri Amani na Upendo, Mshikamano katika kuleta maendeleo ya Watanzania.

Naomba niwakumbushe tena kuwa, Rais wetu mpendwa anayo haki kama ninyi mbele za Mungu ya kuomba na kujibiwa maombi yake kwa Mungu na yeye akipeleka malalamiko yake mbele za Mungu na kupeleka Waraka wake Mbele za Mungu, hakuna mtu atabaki salama kutokana na Uongo, uzushi, fitina mnaoufanya juu yake.

Kama Yesu alivyowafia na akaimwaga Damu yake Msalabani na ndivyo na yeye pia Yesu alimfia msalabani. Kabla hujaondoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako, ondoa boriti kwenye jicho lako kwanza. Kama kweli ninyi ni viongozi mnaosimama mbele za Mungu na wenye hofu ya Mungu, semeni kweli kama wenye hofu ya Mungu, elezeni umma wa Watanzania na Waumini wote mambo mazuri ambayo Rais wetu amefanya kwa kipindi hiki kifupi cha Uongozi wake.

Rais wetu ni Mwanadamu kama wanadamu wengine, kama kuna jambo lolote baya amefanya tumuite tuzungumze naye kwa Upole na kwa Upendo kwa pia amekuwa akiyatembelea makanisa yetu wakati mwingine bila hata kualikwa. Nawaomba kwa Moyo wa Unyeyekevu, tusiseme uongo kwa sababu Uongo ni dhambi. Je,Watu wanakufa kwa ajari, mtasema ameonge na madereva ili wasababishe ajari?, mbona watu wa Chama Tawala walipokuwa wanauawa Kibiti Maaskofu na Wachungaji mlikuwa kimya?.

Naweza kusema, ninyi ni waoga na mnataka kupandikiza hofu kwa Waumini kwa kuficha mambo ya kweli ili kupandikiza Chuki, ukabila na msitumike kama mtaji wa Wanasiasa.

Mimi kama kiongozi wa Kiroho nawaambieni Mungu hapenndi mnachokifanya, acheni kabisa, kwa nini tusubiri siku za Kristmass na Pasaka ndiyo tuyaseme haya?.

Nawaasa viongozi wote wa Dini, tuache uoga kwa kuchochea chuki kwa Waumini, hao si Samaki wa kula mnofu wote na kubakiza mifupa, kuna siku watawageuka na kupoteza imani kwa kuwafukuza madhabahuni na ndipo mtakapoona hasara ya kupanda chuki kwa jamii mnayoingoza.

Mwisho, nataka kusema, Rais wetu, Watanzania wanakupenda, wako Maskini kwa matajiri, wajane, wagane, yatima, watoto, wanakuombea kwa Moyo. Kumbuka, Wayahudi walimshangilia Yesu kwa kumtandikia matende na kuimba Hosana mwana wa Daudi Mbarikiwa, kesho yake wakasema asulubiwe. Lakini Mpango wao wa kumuua Yesu uligeuka Ufufuo wenye utukufu. Ndugu zake Musa walimkataa alipowasaidia, akakimbilia Midiani lakini alimsubiri kwenye kichaka kinachowaka moto ili ampe maagizo kwa ajiri ya ukomozi wa Israel. Mungu amekuchagua kama alivyowachagua viongozi wa dini, Usiogope Maneno yao. Fanya kazi ya Watanzania kwa Moyo, Mungu atakulipa. Neno la Mungu linasema, “Watakuja kwa njia moja, watatawanyika kwa njia saba, watashindanada nawe lakini hawatashinda.”

Mungu akupe Neema, kila Silhala itakayoinuka juu yako haitafanikiwa na kila Ulimi utakoinuka utahukumiwa kuwa mkosaji. Damu ya Yesu ikakufunike katika Pasaka hii, na Damu ya Yesu ikanene mema juu yako, familia yako na Watanzania wote.

Mungu akubariki na aibariki Tanzania.
 
Nilidhani ni walaka ulioandikwa na taasisi,kumbe umeandikwa kwa utashi wa mtu mmoja!
 
Back
Top Bottom