Waraka wa Mbunge Elibariki Kingu kwa Wabunge CCM kuhusu fao la kujitoa

Serikali wabuni namna nyingine ya kupata vyanzo vya mapato na sio kutolea macho pesa za wavuja jasho.Kodi wanayopata kwenye mshahara inawatosha,hiyo inayoenda kwny mifuko ya jamii waiche kama ilivyo siyo pesa zao hizo!!
 
Wabunge wa CCM Tusiyumbe.

Nimeanza kwa Wabunge wa CCM kwa sababu kubwa kwanza sisi chama chetu ndicho kilicho na dhamana ya kuwaongoza watu wa nchi hii.

Lobbing zimeanza za Makampuni makubwa ya Migodi kupinga sheria ya Fao la kujitoa.makampuni binafsi nayo yataanza soon kupinga uamuzi huu kwa maslahi ya wachache Maslahi yasiyozingatia maono ya nchi na Usalama wa Taifa.Maslahi yanayoangalia siasa za muda za kuwafurahisha wanaharakati huku taifa likikosa nguvu ya kiuchumi.

Nawatahadharisha wabunge wote na hasa wa Chama changu CCM,tuwe makini na kila move hasa kipindi hiki ambacho Rais Magufuli amekuja na mwanga juu ya hatma ya viwanda vya nchi hii;Magufuli ameamua nchi iwe ya viwanda kupitia Mifuko hii ya kijamii,Lakini naona mapandikizo yakutaka kuidhoofisha mifuko hii,Mipango hii wanajua wanaoiratibu nia yao lakini wabunge wenzangu na wana CCM fao lakujitoa ni miongoni mwa mipango ovu ya kutaka kumdhoofisha Rais Magufuli na kudhoofisha mapato ya mifuko hii iliyoelekezwa kusimamia mageuzi ya viwanda nchini.

Kwanini watanzania kila jambo tuliwekee siasa?Uimara wa mifuko.ya kijamii popote duniani ndio kiini cha Usalama wa Taifa,Usalama.wa nchi katika kila nyanja iwe ya dharura za kiulinzi au kukuza uchumi hii ni roho ya nchi hasa nchi Hizi zinazoendelea.

Tuwe makini sana juu ya hawa wanaotaka kuturudisha nyuma.Rais anadira ya viwanda,Mifuko hii imepewa jukumu hili kwanini tuanze kutaka kuwadhoofisha.Kwa haraka haraka NSSF wanaweza kuokoa karibu biln 60 pesa ambazo kwa nchi changa kama hii zikiwekezwa kwa busara na uzalendo zinalifanya taifa lipae kiuchumi.

Watanzania tuache siasa pesa hizi ni za watanzania wakifikisha umri unaostahili watalipwa nchi hii lazima itangulize maslahi ya wengi kwa faida ya vizazi,tuache harakati na siasa za kutaka sifa kwa mambo mazito yanayogusa ustawi na usalama wa nchi.

Tuache mifuko ikusanye pesa a kuwekeza kwenye viwanda .Tuache ubinafsi kwa faida ya vizazi vinavyokuja.

Kingu Elibariki
MP Singida West
hivi si sahihih kusema nchi ya viwanda italetwa kwa kutumia michango yetu sisi wavuja jasho wa nchi hii huku nikufilisika na kukosa dira na maono, haiwezekani mfanyakazi aliye na ajira isiyo na uhakika akaja achishwa kazi kabla umri wa kustaafu eti asubiri huku ni kumnyima haki. Ndo maana tunasema wabunge kama hawa hawapo kwa maslahi mapana ya nchi hii watuachie hela zilizoko huko kwenye mifuko hiyo siyo za serikali. Huyu Kingu wenzie aliokuwa nao kama ma-DC awamu iliyopita na kutemwa na awamu hii ya tano wengine hakuwa wamefisha umri wa kustaafu lakini wanachukuwa mafao/kiinua mgongo yao, Mh Kingu naamini ungeukosa huo ubunge na kisha kutemwa ukuu wa wilaya je ungesubiri kinuanua mgongo mpaka ufikishe umri wa miaka 60 upo hapo ukitaraji kupata kiinua mgongo cha ubunge je ni sahihi wazo hili au ukaletwa mswaada mbele yenu unaotaka mbunge asilipwe kinua mgongo mpaka pale itakapothibika kuu ukosa ubunge aliokuwa nao ndipo apewe, na hiyo ndo maana kinua mgongo. Naamini ungepinga kwa kwa nguvu zako zote na hapo ndipo utakapokuja amini kuwa siasa ndo maisha ya kila siku kwani siasa na wana siasa hujenga na kuamua mustakabali wa nchi hii. Ama kweli CCM ya leo imekuwa siyo mtetezi tena wa mfanyakazi huku nikupoteza misingi iliyo asisi chama cha TANU na
AFRO-SHIRAZI
 
Na huyu ndio Mbunge anayejinasibu kwamba ni "Mpendwa ktk Kristo".....Hawa ndio walokole feki waliojivika kanzu la siasa....Unafiki mpaka katikati ya miguu
Hatari lakini salama. Antafuta kupendwa wakati wananchi Wa jimbo lake wamempenda na kumpa Ubunge! Anatamani awe waziri. Serengeti boys Wa UVCCM walisha rogwa zamani wote wanafanana.
 
Ni ishara wazi kwamba wamekosa hela ya kujengea viwanda sasa wanageukia Pesa za pensheni.

Viwanda si mchezo,vitawapiga hasara haraka sana.
Wachina wamewekeza sana kwenye utafiti wa teknolojia ndio maana kila siku wana bidhaa mpya.

Sisi tangu viwanda vya nguo vijengwe tunazalisha khanga tu.
Huyo mbunge aonyeshe mfano kwa kuyapeleka mafao yake mifuko ya pensheni na asiyachukue mpaka akiwa na miaka 60

Na inaonekana katumwa na mkubwa saana wa hicho chama
 
Huyu mbunge ni wa kupigwa makofi kabisa, haiwezekani ashindwe kujua kabisa ajira zenyewe tunazopata hazina hata security na ni muda wowote tu unatimuliwa. Alitakiwa awaambie ccm wenzake watoe ajira za kudumu kama wana akili sana, huyu na wenzake ni wanafiki kabisa, ningemuamini angeanza na mafao ya wabunge nao wakishamaliza vipindi vyao wasichukue kitu mpaka wafikishe miaka ya kustaafu.
Anazungumzia jambo asilojua uchungu wake na hajui victims wengi ni masikini na sio wao.
Mmeshindwa kujenga viwanda mnategemea hela zetu mjipatie umaarufu wa kijinga, tuambieni na wale wanaofikisha umri halali mnawapa mafao kwa muda ?
 
Hawàna fedha ya kutekeleza ilani......ahadi zimewazidi,na huu ni Mwaka mmoja tu.

Kujenga kiwanda sio mziki wa kitoto,kiwanda kwa maana ya kiwanda!!

Walishauriwa wawekeze kwenye viwanda vidogo vidogo hawasikii!!

They are running out of options ....they are running against time!

Sera si rafiki,,waliingia na swaga za kuita matajiri majina mabaya!! Hizi sio enzi za ujamaa bhana

Kwanza muwalipe nssf,pspf, na mashirika mengine yaliyojenga UDOM.

PSPF inaidai serikali karibu trilioni moja na haijulikani mtalipaje! Bado tena mnataka kukopa.

Kamati ya bunge kila Mwaka inaweka tahadhari kwamba PSPF technically ni bankrupt,imefilisika kutokanà na serikali kutoilipa madeni yake
 
Aiseee angekuwa anaongea haya hadharani angeishia kupigwa mawe watu wanahasira
 
Duh! Mishangao haiishi bongo. Huyu naye ni mbunge eti na anaowawawakilisha. Too pathetic kwa kweli.
Huenda alikuwa anawaambia wabunge wenzake wa ccm wasichukue mafao baada ya miaka mitano kuisha na badala yake wasubiri hadi muda unaotajwa kwenye sheria ya fao la kujitoa ufike. Kama ni hivyo atakuwa sahihi zaidi japo atapata matusi kutoka kwa ccm wenyewe wasiopenda sahani zao ziwekewe miguu.
Lakini asisahau pesa za mifuko ya jamii sio mali ya umma bali za mchangiaji na kumwekea masharti magumu ya namna ya kuzipata ni kuwachonganisha na watawala. Wabunge wa çcm mliopitisha sheria hii mtalaaniwa na waathirika wa sheria hii.
 
Kingu, sio kazi ya nssf kujenga viwanda, kazi hiyo ni ya NDC na TIRDO, na kazi ya kufinance hivyo viwanda ni ya TIB na sio ya nssf,
Hawa wabunge viazi sijui huwa wanawaza nini?
 
Back
Top Bottom