Waraka wa kiume sehemu ya pili

Waraka wa kiume sehemu ya pili

theriogenology

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
8,748
Reaction score
15,731
Mwanaume anayempenda mke/mpenzi wake kwa maneno na matendo huku akimpa heshima mke/Mwenzi wake jua ni matunda ya malezi bora ya Mama yake mzazi na usimamizi wa Baba bora .

Kuna page nyingi sana kwenye mitandao ya jamii kuhusu wanawake kuwapa faraja,kuwashauri,kuwabembeleza na kuwaonyesha makosa yao katika mahusiano,biashara zao na malezi yao.

Kuna page chache sana za kiumeni juu ya kuwapa faraja wanaume wasio na ajira,waliokata tama,wanaume waliumizwa na warembo na wanaume wasio na mahusiano mazuri kwenye ndoa zao na mapenzi yao.

Huu ni waraka wa kiume na jambo zuri kuhusu wanaume ni kuambiana ukweli unaouma huku unakuponya. Sasa ni wakati mzuri wa kuutafakari huu waraka wa kiume kwa mwaka mzima wa 2018 katika kusimama kiume kwenye mahusiano .

Valentine day February 14 ,ipo njiani ni sikukuu ambayo wanawake wanaipenda sana kuisherekea na kuhitaji mahitaji mengi juu ya kilele cha siku hiyo ya wapendano.

Mwanaume hautakiwi kuwa na mwezi wa mapenzi bali unatakiwa kumpenda mwanamke /mpenzi wako siku zote za maisha yenu ya mahusiano na sio Valentine day February 14.

Tengeneza utamaduni wa kuitafuta pesa kwa kutumia akili nyingi na nguvu kidogo kisha tengeneza kipaji cha kuitunza pesa na kuizungusha katika uwekezaji wenye tija kwa muda wa miezi kumi na mbili kisha tenga mwezi mmoja wa kupumzisha mwili na akili na mwenzi wako kwenye sehemu tulivu Tanzania kama vile Zanzibar,Tanga,Morogoro mahala popote penye vivutio Tanzania na sio kuingojea Valentine day February 14.

Mwanaume hutakiwi kumuhonga mwanamke pesa badala yake yatakiwa umtengeneza mwanamke mwenye sifa zote za kuwa mwanamke bora mwenye pungufu la kuomba pesa na kumfanya kuwa mwanamke muwajibikaji kwa kumpa mawazo ya kuitafuta pesa na kuachana na tabia ya kuomba pesa ,kama huna pesa mwambie ukweli kuwa huna na sio kukopa pesa kwa ajili ya mwanamke.

Tabia ya kula mangengeni kwa mwanaume aliye kwenye ndoa au kwenye mahusiano inatokana na mwanaume mwenyewe na sio mwanamke.

Kama upo kwenye mapenzi na mwanamke unayempenda kupindukia na akatambua udhaifu wako jua huwezi kuwa na kauli juu yake ,na utatii anachosema yeye na sio kutii unachosema wewe .

Mwanaume unatakiwa kuwa kichwa cha familia/Nguzo ya familia kuanzia kauli na uwajibikaji,kulalamika matatizo ya kifedha mbele ya mwanamke ni udhaifu ambao hautakiwa kuonyesha kwa mwanaume.

Kwa mwanaume ambaye hajao ni vyema ukatizama mwanamke mwenye ubongo mzuri,utashi mzuri na hazina ya maarifa hawa ni wanawake wenye kipaji cha kutunza ndoa na wachapakazi kundi hili huwa hawana utamaduni wa kuwa tegemezi na kuomba omba pesa .

Achana na wanawake wa kwenye mitandao ya kijamii ambao kila dakika wanapost picture za makalio na picture za Kula Bata,mwanamke ambaye anaomba kuanzia pesa ya airtime,kusuka nywele,bia huyu ni demu ambaye penzi lake huwa lina uhai wa masaa 24 na hamu ya mwili ikikutoka na huna tija naye sababu ulisukumwa na tama ya mwili na sio upendo kwake.

Usimuonyeshe mwanamke udhaifu wake na ni mwiko kila upatapo pesa kumuonyesha mwanamke yatakiwa mwanamke kutokufahamu ukiwa na pesa au usipokuwa nazo .

Wanawake wanapenda surprise so anatakiwa akijua leo wewe una pesa kumbe wewe hauna na siku akijua hauna PESA kumbe wewe unazo .

Kumlilia mwanamke ni moja ya dalili kubwa na udhaifu kwa mwanaume turejeshe tabia halisi za kiume . Men think and act for self-interest, and are inclined to lie, cheat and swindle when doing so brings them benefits.
 
Back
Top Bottom