Waraka wa Jumapili kwa Rais wangu.

Waraka wa Jumapili kwa Rais wangu.

Bwana Jericko,vipi nikikuambia kwamba hivi vitu vimezidi kuwagawa waafrika,unakumbuka usemi divide and rule?mwafrika alikuwa ana dini kabla ya watu weupe kuja,ila hawakuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu kwa maana ya kuandika,ndiyo maana dini tuna zoona leo ni wenye herufi zao au walioweza kuandika au kuweka kumbukumbu,neno mungu halijaletwa na mtu mweupe liko kwenye kila kabila la mwafrika,Dini zilizo kuja ni aina fulani ya kutafuta watu wa kukutumikia au kukutetea,mwarabu akipigana muislamu mwafrika anaona ni yake,mzungu akipigana vilevile mkristo mwafrika anaona ni yake na sasa mwisraeli akipigana mlokole ni ni yake,swali hizi dini kitu inayofundisha ni mwenye imani hiyo ndugu yake ni mwenye imani hiyo,na sisi hamna mahala tunafundisha mwafrika ndugu yake mwafrika,utumwa kwa mwafrika utaendelea kimawazo hadi tujitambue,hizi dini zote hakuna hata moja iliyokataza utumwa na waliendelea wakiwa na dini hizo,ili tubadilike lazima tutafakari kitugani kinaendelea duniani na mbo gani waafrika tulipitia na tusikubali mawazo ya watu weupe,Hii tunayo ambiwa demokrasia ina upana kuliko siasa,inakuja na rusha ndani pia (lobbiest),ina gawanya pia taifa kwa kupingana hatakama kuna usahihi,sisemi demokrasia haifai ila tusipokuwa makini tutatumika kupitisha matakwa ya watu weupe na hatutaweza kufika,kwa mimi asilimia 60 ya mfumo unayoletwa kwa mwafrika ni yale yenye manufaa kwa mtu mweupe,kiukweli asilimia 80 ya maendeleo duniani yaliletwa na mfumo usiyo wa demokrasia,aidha ufalme (monachy) au utawala wa kiimla .
Yaani andiko lako limejaa mambo muhimu kuliko thread yenyewe. Dini pia inaatuomba tuwaheshimu walio madarakani lakini kina Yericko ndiyo wa kwanza kushangilia vurigu na kususa. Dini hizi iwe ukristo ama uislamu h@hakuna ya maana. Wakristo waliuza binadamu wenzao kama bidhaa huku wakija na biblia. Waarabu walileta uislam na ndiyo wabaya zaidi ya Wakristo si tu waliuza binadamu wenzao kama bidhaa waliwa wa castrate wanaume pia. Ndiyo maana unawaona waafrika ulaya na marekani lakini huwaoni wengi uarabuni pamoja na kwqmba ndiko biashara ya utumwa ilishamiri. Sielewi hata kidogo nikiona wanaojiita wakristo na waislamu wakilumbana humu JF kama wehu kwa dini hizi za kitapeli.
 
"Utawaka huendenda na damu, uongozi huendenda na tabasamu la moyo na vinywani mwa umma"
 
nimesoma lkn sioni ushauri au kitu kipya hapo mkuu.
Mungu anakataza kuchanganya dini na Siasa.
"ya kaisali Mpe kaisali na Ya Mungu mpe Mungu"...
Vinginevyo Padri,Shehe au Mchungaji mzuri angekuwa pia kiongozi mzuri wa kisiasa.Kitu ambacho kimewahi kufeli vibaya miaka za zama za giza.
Tunachotakiwa Kufanya ni Kuwaombea Viongozi wetu Mungu awape hekima watuletee amani na utulivu pamoja na vichocheo vya maendeleo ili kila mwenye nia ya maendeleo kiimani au kiuchumi afanikiwe bila kikwazo
Ninadhani unahitaji kuelewa ulichosoma sio kusoma tu...

Yes aliposema Jililieni nyinyi na watoto wenu alikuwa na maana pana sana
 
Historia ya siasa duniani haitengani na historia ya dini. Vitu hivi vimekuwa sambamba na vyenye mafaa kwa jamii yoyote ile duniani, lakini vikileta matatizo makubwa sana katika baadhi ya nchi duniani, matharani ubaguzi wa kiimani umeleta machafuko na uharibifu mkubwa mali pamoja na mauti dhidi ya binadamu. Vitu hivi imekuwa ni vigumu sana kutenganisha katika dunia ya leo huku machipuko ya kiimani yakija kwa kasi ya ajabu.

Kwa upande wa Tanzania mfumo wa siasa umekuwa ni wa kuakisi kutoka mataifa ya Magharibi, na uakisi wake umekuwa ni kinyume. Tukiangalia historia ya binadamu tunaona yakuwa kabla binadamu hajajishughulisha na masuala ya siasa na utawala alikuwa anajishughulisha na maswala ya dini, binadamu akawa mcha-Mungu. Ulipofika wakati wa uteuzi wa kiongozi wa jamii mtu aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo alikuwa ni yule aliyeonekana ni mcha-Mungu. Hata katika jamii zetu za kiafrika zilizotuletea kiongozi wa utawala, pia alikuwa kiongozi wa dini.

Ni huyu aliyeongoza shughuli zote za utawala na za dini katika jamii. Itatumika biblia kutoa mifano hai kuthibitisha uhusiano wa dini na siasa. Hakuna ubishi dunia inakubali yakuwa Yesu Kristo ndiye mwanzilishi wa dini ya kikristo. Hii ni kusema kuwa Yesu Kristo alikuwa kiongozi wa dini. Kwaupande wa kabila Yesu alikuwa Muebrania. Alipozaliwa nchini Uyahudi alikuta tayari watu wa kabila lake wanadini yao ya kiyahudi. Viongozi wa dini ya kiyahudi walikuwa pia watawala waliotawala kwa kutumia sheria za kiyahudi zilizomo katika kitabu chao cha sheria kiitwacho TORATI sheria hizo za dini zikawa pia sheria za utawala. Warumi walipoanzisha utawala wao, Wayahudi waliwaruhusu Warumi kufuata sheria zao za dini ambazo pia zilikuwa sheria za utawala wao wa jadi. Kuhani Mkuu ambaye alikuwa kiongozi mkuu wa dini, alikuwa mwenyekiti wa Baraza kuu la utawala lililoitwa Sanhedrin.

Ni baraza hilo ndilo lililotoa hukumu kuwa Yesu auawe (Math 26:65-69). Hata hivyo adhabu yoyote ya kifo iliyotolewa na baraza kuu la wayahudi ilibidi ithibitishwe kwanza na mtawala wa Kirumi kabla haijatekelezwa (Yohana 18:31). Kwa upande wa Yesu Kristo alipoanza kufundisha dini yake mpya alikosoa sheria za kiyahudi ambazo aliziona hazikuwasaidia binadamu kuishi kwa upendo na amani. Aliwataka wafuasi wa dini yake mpya wasiwe na tabia ya kulipa kisasi. Kwamfano sheria za kiyahudi zinasisitiza kauli ya jicho kwa jicho na jino kwa jino. Katika (Math 5:38-41) tunasoma yakuwa Yesu hakutaka sheria hizo, alisema, “Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino, lakini mimi nawaambia msishindane na mwovu lakini mtu akupigae shavu la kuume mgeuzie na la pili na mtu atakaye kushitaki nakuitwaa kanzu yako mwachie na joho.

Uongozi safi wa kidini wa Yesu Kristu uliwavutia wayahudi wa kawaida hata wakaona anafaa kuwa kiongozi wa utawala, wakataka kumfanya awemfalme. Lakini Yesu hakuwa tayari kujiingiza mno katika masuala ya siasa na utawala (Yohana 6:15) alizoea kusema ufalme wake sio wa ulimwengu huu (Yohana 18:36) Katika mafundisho yake, Yesu hakuwahi kuwaambia wafuasi wake wasichanganye dini na siasa. Hata hivyo aliwataka wawe waangalifu katika kuyashughulikia masuala hayo mawili. Alisema, “Ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu”. (Luka 20:25).

Hakuwahi kuwataka wafuasi wake washughulike na mambo ya mungu (dini) tu wasijishughulishe na siasa. Katika hali hii niwazi kuwa kiongozi wa dini hatakiwi kuhubiri siasa katika jengo la ibada akaacha mambo ya mungu. Vilevile anapokuwa nje ya jengo la ibada hana mwiko wakutokuzungumzia masuala ya siasa na utawala. Baada ya kufa Yesu, wafuasi wake waliendelea kujihusisha na masuala ya dini na siasa, mambo ya utawala yakiendelea kuhusishwa na dini. “Iliaminika kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu (Warumi 13:1). Katika hali hiyo kiongozi wa Katoliki duniani Papa wa Roma alipewa mamlaka makubwa ya utawala, eneo lake la Vatican likapewa hadhi ya utawala wa nchi.

Eneo hilo likapewa mamlaka kamili yakupokea mabalozi wakigeni. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na imani ileile iliyojengeka siku nyingi kuwa kiongozi wa dini ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa utawala pia maana kwanjia hiyo atakuwa nanafasi nzuri ya kupambana na maovu. Lakini wakati Papa wa Roma anashughulikia zaidi masuala ya dini kuliko ya siasa na utawala, kuna viongozi wengine wa dini wamewahi kupewa madaraka kamili ya kushika utawala wa nchi. Mfano Askofu Mkuu Makarios wa kisiwa cha Cyprus ambaye aliwahi kutembelea Tanzania. Wakati huohuo kuna nchi duniani ziliamua siku nyingi kuwa nchi za dini mfano Uingereza ni nchi ya kikristo ambapo mishahara ya maaskofu hulipwa na serikali. Pia nchi za Saud Arabia, Moroco, Libya nk ni nchi za kiislamu. Si hivyo tu pia kuna nchi ambazo vyama vya siasa vya kidini vinaruhusiwa mfano Ujerumani Christian Democratic Union (CDU.

Uongozi hutoka kwa watu, Watu ndio wanaweza kukufanya kuwa kiongozi, Ukiona watu wamekuja kukuomba uwe kiongozi wao tena watu hao "wenye tashwishwi na haiba za nera (mvi)" tambua kuwa mamlaka hiyo inatoka kwa Mungu. Pindi uachapo uongozi na kujitwika utawala, Mungu hujitenga nawe na shetani huambatana nawe, Utawala huenenda na damu, uongozi huenenda tabasamu la moyo na vinywani mwa umma.

Ni hayo rais wangu, sikia sauti ya Mungu kupitia makutano yaliyofika mbele yako kukupa uongozi! Tunamtaka Ben Saanane akiwa hai.

Na Yericko Nyerere
Hakika ujumbe wako umenivutia najua walengwa ni wasikivu vyombo husika vitalifanyia kazi huko CHATU kabla kiwanda cha MBEGE hakijaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana Jericko,vipi nikikuambia kwamba hivi vitu vimezidi kuwagawa waafrika,unakumbuka usemi divide and rule?mwafrika alikuwa ana dini kabla ya watu weupe kuja,ila hawakuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu kwa maana ya kuandika,ndiyo maana dini tuna zoona leo ni wenye herufi zao au walioweza kuandika au kuweka kumbukumbu,neno mungu halijaletwa na mtu mweupe liko kwenye kila kabila la mwafrika,Dini zilizo kuja ni aina fulani ya kutafuta watu wa kukutumikia au kukutetea,mwarabu akipigana muislamu mwafrika anaona ni yake,mzungu akipigana vilevile mkristo mwafrika anaona ni yake na sasa mwisraeli akipigana mlokole ni ni yake,swali hizi dini kitu inayofundisha ni mwenye imani hiyo ndugu yake ni mwenye imani hiyo,na sisi hamna mahala tunafundisha mwafrika ndugu yake mwafrika,utumwa kwa mwafrika utaendelea kimawazo hadi tujitambue,hizi dini zote hakuna hata moja iliyokataza utumwa na waliendelea wakiwa na dini hizo,ili tubadilike lazima tutafakari kitugani kinaendelea duniani na mbo gani waafrika tulipitia na tusikubali mawazo ya watu weupe,Hii tunayo ambiwa demokrasia ina upana kuliko siasa,inakuja na rusha ndani pia (lobbiest),ina gawanya pia taifa kwa kupingana hatakama kuna usahihi,sisemi demokrasia haifai ila tusipokuwa makini tutatumika kupitisha matakwa ya watu weupe na hatutaweza kufika,kwa mimi asilimia 60 ya mfumo unayoletwa kwa mwafrika ni yale yenye manufaa kwa mtu mweupe,kiukweli asilimia 80 ya maendeleo duniani yaliletwa na mfumo usiyo wa demokrasia,aidha ufalme (monachy) au utawala wa kiimla .
Fine, utawala wa kiimla utumike kukuza uchumi, sio kuua kama inavyotokea sasa hivi. Unakamia kuwakomesha matajiri na wahangaikaji wazawa unategemea wawekezaji watoke wapi? Mbinguni au???
 
Fine, utawala wa kiimla utumike kukuza uchumi, sio kuua kama inavyotokea sasa hivi. Unakamia kuwakomesha matajiri na wahangaikaji wazawa unategemea wawekezaji watoke wapi? Mbinguni au???
Hivi unajua uchumi wa china kifika hapa ilipo ilipitia changa moto nyingi,tofauti yao na sisi waafrika wenyewe walijitambua na wakalazimika kutunga sheria na kwenda njia yao bila kusikiliza wazungu,advantage waliokuwa nao ni wanadini yao hivyo imekuwa vigumu kuwavuruga.
 
No, sioni ufanano wowote na wachina kwenye move ya hapa kwetu. Double standards zimekithiri, dhambi moja lakini mmoja analindwa mwingine anachinjiwa baharini. Kwa unafiki, visasi na kukomoana utajenga uchumi gani??
 
nimesoma lkn sioni ushauri au kitu kipya hapo mkuu.
Mungu anakataza kuchanganya dini na Siasa.
"ya kaisali Mpe kaisali na Ya Mungu mpe Mungu"...
Vinginevyo Padri,Shehe au Mchungaji mzuri angekuwa pia kiongozi mzuri wa kisiasa.Kitu ambacho kimewahi kufeli vibaya miaka za zama za giza.
Tunachotakiwa Kufanya ni Kuwaombea Viongozi wetu Mungu awape hekima watuletee amani na utulivu pamoja na vichocheo vya maendeleo ili kila mwenye nia ya maendeleo kiimani au kiuchumi afanikiwe bila kikwazo
Kama hujaweza ona tofauti ya KAISARI na KAISALI , ni ngumu sana kutushawishi una akili timamu.Ungepewa nchi wewe sidhani km ungeweza ona tofauti ya Tank na bulldozer.
 
Kama hujaweza ona tofauti ya KAISARI na KAISALI , ni ngumu sana kutushawishi una akili timamu.Ungepewa nchi wewe sidhani km ungeweza ona tofauti ya Tank na bulldozer.
Hahaaa hawa ndio washangiliaji tu walipoambiwa tingatinga linataka urais wakashangilia, leo tingatinga linawathibitishia ubora wa kazi yake wanalia
 
Unamhoji Magufuli kwani ndiye aliyemficha huyo saa kumi sijui saa mbili??
 
Hivi unajua uchumi wa china kifika hapa ilipo ilipitia changa moto nyingi,tofauti yao na sisi waafrika wenyewe walijitambua na wakalazimika kutunga sheria na kwenda njia yao bila kusikiliza wazungu,advantage waliokuwa nao ni wanadini yao hivyo imekuwa vigumu kuwavuruga.
Acheni kuelezea kitu msicho kijua.China ni project ya mataifa ya magharibi.China ni kiwanda yao.
 
Acheni kuelezea kitu msicho kijua.China ni project ya mataifa ya magharibi.China ni kiwanda yao.
Umejibu tu au unadhani watu hawajui,china imejengwa kwa misingi na siyo tu viwanda unavyoona leo,mimi nimetembea china na siyo ya leo unayodhani ya wamachinga kuenda guangzhou na shenzhen,china ya kweli bado iko hubei ukienda huko bado kuna system ya communist,dola mtu binafsi haruhusiwi kuchenchi hadi benki,system ya land tranfer bado inafanya kazi,ukienda shenyang karibu na mongolia utaona misingi ya ujamaa,nakufahamisha ya kuwa mimi siyo machinga wa guangzhou,usidhani watu wote wanaangalia Cnn na kuamini kinachozungumzwa hapo,soma historia kabla hujadhani watu hawajui,soma opium war china walipiga miaka 21 mwaka 1839 hadi 1860 wakati uingereza walipowafanya kuwa mateja ,hii unga unaoona leo mnakamata kina chidi benzi ilipelekwa china na muingereza kipindi hicho lakini walipigana na wakashinda,soma historia ya japan ikitawala china ,soma historia ya Mao,halafu useme watu hawajui,matatizo yenu kizazi kipya hamsomi historia za wenzonu mnaamini media propaganda sana.
 
asante kwa gazeti. jitahidi kuwa brief kwenye maandiko yako. tuna mambo mengi ya kufanya
 
Kama hujaweza ona tofauti ya KAISARI na KAISALI , ni ngumu sana kutushawishi una akili timamu.Ungepewa nchi wewe sidhani km ungeweza ona tofauti ya Tank na bulldozer.
naona unathibitisha ufinyu wa vizio vyako kiakili. Umeruka hoja ukakimbilia kujadili lugha.
Mapengo yakifikra yaliyosababishwa na ushabiki maandazi yamekufikisha hapo.
Siku akili zikitimilika waimarishe na wenzako.
 
Back
Top Bottom