Waraka wa I.G.P kwa Askari wote Tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa I.G.P kwa Askari wote Tz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngaliba Dume, Sep 15, 2012.

 1. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Jana I.G.P S.Mwema alisambaza waraka kwa ma-RPC wote Tz nzima kuwataka waitishe "MABARAZA YA ASKARI" ktk mikoa yote,lengo likiwa ni kutathimini mwenendo wa Jesh la polisi dhidi ya raia. Katika Mabaraza hayo Askari walipewa nafasi kujadili,kutoa mawazo na kupendekeza nini kifanyike baada ya Jesh kupoteza imani kwa raia na jamii. Katika waraka huo wa siri I.G.P aliwataka makamanda wawatie moyo vijana wasikate tamaa,kwan kwa tukio la Iringa imeonekana askari wote wamerudi nyuma na kupunguza hari ya kazi,hii imefanya viongozi wa juu kupata hofu ya utayali wa askari ktk kulitumikia jeshi... Katika maoni,askar wengi wamependkeza RPC Iringa aunganishwe ktk kesi,kwani kumwacha Cleophas Simon peke yake n uonevu,pia wameomba serikali iwakemee viongozi wa CCM wanaoshndkza polisi kuwatandka vyama vya upinzani..ktk kikao cha mkoa wa Iringa askari wengi wameonekana kukata tamaa na kutaka kuacha kazi...hali ya askari wa chini wanaotumika ktk Operation za riots imeshuka sana kwa kutishika na tukio la Iringa. Vijana wengi wameonekana kuchukizwa na hali ya kulazimishwa kutumia nguvu kwa maslahi ya kisiasa,kwa kugundua hilo makamanda wamewatia moyo vijana wengi kuwa wasikate tamaa,kwani swala la Iringa n sehemu ya ajali za kazini ambazo wao kama askari wanatakiwa wakabiliane nazo! Kiukweli vijana wengi wamekata tamaa baada ya kuona panapotokea tatizo ni askari wa vyeo vya chini ndo wanatolewa kafara bila kufuata uwajibikaji wa pamoja na Seniority ya jeshi la polisi ambapo mdogo hafanyi kitu bila mkubwa kutoa amri.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,702
  Trophy Points: 280
  Jeshi la magamba limeanza kuweweseka. Walidhani Watanzania tutaunyamazia UDHALIMU wao wa kuwaua Watanzania wasio na hatia milele. Jeshi la polisi linanuka rushwa, limejaa wauaji na wabambikiaji kesi zisizo na kichwa wala miguu ili kujionyesha kwamba ni watendaji kazi wazuri. Bila fagio la nguvu kupita ndani ya jeshi la polisi jeshi hilo litaendelea kutoaminiwa na kuheshimiwa na Watanzania walio wengi.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kamuhanda asiposhitakiwa tutampeleka the hague kwa yule maza wa kisenegal
   
 4. M

  Mesaka Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Yes, ili kuwatendea haki askari wa vyeo vya chini na raia kwa ujumla Kamuhanda anastahili kushtakiwa no.1.
   
 5. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Very sad kutomuunganisha RPC wa Iringa katika case hii,hasa kwa kuwa alikuwepo pia eneo la tukio.

  Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
   
 6. P

  Penguine JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Hofu yangu ni mantiki ya thread hii. Kwamba jana hiyo IGP alisambaza waraka kwamba pawepo na Mabaraza ya “Wapiga Raia na Uhai wao", jana hiyo hiyo hayo mabaraza yameanza kukutana na kutoa maoni yao halafu hiyo jana Makamanda wakafanya tathmini ya Kushuka kwa ari na wakatiwa moyo!

  Mbali na hiyo logic, nakubaliana nawe kwamba vijana hao wanaitenda dhambi ya kutupasua matumbo ili ccm ipate kuishi.
   
 7. n

  ngala moja Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani tatizo hasa linatokana na kile kinachoitwa general order za polisi zinazomtaka askari kutii amri bila kuhoji uhaklali au ubatili wa amri. mfimo huu ambao umeridhiwa toka kwa mwingereza umepitwa na wakati.mfumo mbovu unaogandamiza uhuru na haki za kiraia kwenye nchi huru. bila kuzibadili bado tutaendelea kuganga majeraha na kuzika wafu wetu ambapo pengine kesho ikawa zamu yangu au yako.
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  tuwekee hapa nakala ya huo waraka ndo tuchangie.
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Kwelii...sasa wakati umefika askari wawe na msimamo na mipaka yao ya kazi iwe inajulikana wasiamrishwe na wanasiasa kulinda udhalimu wao!watekeleze majukumu kwa weledi si utashi wa kisiasa!!RPC lazima aunganishwe na yule kijana "bangusilo"hapo ari ya askari wengi itarejea na kuona its fair na ile ilikuwa ajali kazini!!
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Pamoja na ubaya wa Polisi, tuache kutunga stori na kuziweka humu!
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  i think its a little bit too late for that...damage is already done
   
 12. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  sijafikia kiwango cha kutunga story!uliza polisi watakwambia
   
 13. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Waraka umewafikia makamanda toka juzi jioni..na jana walitakiwa kuitisha vikao,na wamefanya hivo..
   
 14. k

  kakamukubwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa njia ya email,posta...
   
 15. k

  kakamukubwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Edit thread yako,
   
 16. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Mh...mh...ningekuwaga moderator??!
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Awaulize Polisi au awaulize ma RPC? hapa nilipo mimi nipo na Polisi ni rafiki yangu na na yeye ni Polisi wa Mahakamani na huwa havai uniform, ni kwamba jana Polisi wote walipewa amri ya kuvaa uniform kwa ajili ya kukabili maandamano ya waislamu lakini rafiki yangu alivyofika pale Central Polisi alisingizia amefiwa na akaruhusiwa kwenda kuzika lakini ilikuwa ni fix yeye hayko tayari kutumika kwenye ujinga.

  Back to topic ni vizuri kama una hizo Information ungetuwekea huo waraka hapa lakini usiseme waulize Polisi, maana hao Polisi baadhi yao ambao ni wema tuko nao na kama kuna hilo wanalifahamu mimi ningekuwa nimelijuwa. Ila sijakupinga.
   
 18. P

  Penguine JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Hapo nimekuelewa NgalibaD.
  Tuko pamoja sana ktk kuutambua, kuulani na kuukomesha udhalimu.
  Good day kaka.

   
 19. M

  MTK JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Upuuzi mtupu huo!!!! Mabaraza ya askari ni kamati za kisiasa na matawi ya CCM ndani ya jeshi linalotakiwa kuwa non-political, non-partisan and professional.

  Kinachotakiwa ni Polisi kufuata mahitaji ya katiba na general Police orders period.

  kwamba vyama vya siasa vinatakiwa kutoa taarifa (sio kuomba kibali) kwa polisi saa 48 kabla ya kufanya mkutano au maandamano;

  kwamba kufanya mikutano na maandamano ni haki ya vyama vya siasa ili kukidhi mahitaji ya katiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni bila kuvunja sheria.

  Kinacholipelekea jeshi la polisi kupoteza imani ya wananchi ni utayari wake wa kutumika kisiasa kwa mahitaji ya chama tawala CCM; na kujipa madaraka lisilokuwa nayo ya kuamua kama chama cha siasa cha upinzani kifanye mkutano ua la! ni hilo tu na halihitaji kutumwa na CCM kuunda mabaraza ya polisi, hatua hiyo ni sawa na nchimbi kuunda tume ya kuchunguza mauaji ya David Mwangosi wakati vielelezo vyote vipo wazi na wauaji wanajulikana kwa majina, sura na makazi yao!!!


  Kama kweli Saidi Mwema ni askari wa haja asitupotezee muda bali afanye the right thing kwa kukataa CCM kulitumia jeshi la polisi kwa maslahi yao ya kisiasa.

  afterall ni CCM wenyewe ambao kwa makusudi kabisa wamejipaka matope kwa ufisadi na rushwa na kugenisha raslimali za taifa bila kujali maslahi ya taifa, wananchi wameligundua hilo na ndio maana Chadema imepata nguvu ya kuitetemesha serikali, wasitafute mchawi mbali , mchawi wao ni wao wenyewe kwa kuliibia taifa bila huruma, sasa maji yamewafika shingoni wanathubutu kulitumia jeshi la polisi kulinda uovu wao! But as long as umma umeamka; hawataweza; hawatweza, hawataweza.


  Right is devine; it will forever prevail. Eeh Mungu iokoe Mama Tanzania kutoka mikono ya wadhalimu hawa CCM waliomzika Baba wa Taifa kwa gharama kubwa na mbwembwe nyingi kisha siku chache baadaye wakaizika misingi ya uadilifu aliyoijenga muasisi huyo wa taifa letu.
   
 20. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Jeshi sasa aliiendeshwi kwa principles zake kama inavyotakiwa.
  Inajulikana kabisa Askari wa chini anapata order toka kwa senior wake. Katika operation yoyote lazima iwe na commanding officer wa site. Sasa inakuwaje linapotokea kosa awajibishwe aliyepokea amri na si aliyetoa amri hiyo? Lakini zikitolewa sifa na nishani ni hao wenye vyeo ndio wanapata? Kuna tatizo sana na tatizo hilo ni SIASA!
   
Loading...