Hakuna sababu za kuogopa jumuiya ya afrika ya mashariki kwa ujumla mimi nimesoma Kenya kwa kipindi kirefu nimefanya kazi kule kidogo na mpaka sasa hivi nina ushirikiano na watu wengi wa huko , hakuna sababu ya kuogopa kufanya nao kazi au chochote tunaweza kushindana kwa lolote endapo tunaamua kwa dhati kwa mtu mmoja mmoja au wote kwa ujumla tuache unafiki na wivu usio na mipango
Pana makala ya Boaz Boaz iliyoainisha kwa kina namna Watanzania wenye inferiority complex wanavyoamua kuunga mkono EAC kama njia mojawapo ya kuonyesha wao "sio waoga", kisha "wamesoma". Kana kwamba haitoshi, watu hao wenye kutaka kujithibitisha walivyo 'wamekucha' huwaita "waoga" Watanzania wenzao wote wanaokataa EAC.
Kwa kawaida hawana uwezo, au kwa sababu nyingine, hawawezi kuchangia mada inayozungumzwa.
Watu hawa ni wa kupuuzwa.
Hoja ipo palepale, Waraka Hamani umesainiwa, Watanzania tufanyeje kuinusuru nchi yetu?
Mikataba ya EAC imeshasainiwa na inaendelea kusainiwa kwa kasi mpya.
"Waraka wa Hamani" ushasainiwa.
Jamani, lipi la ziada tunaloweza kulifanya kuliokoa taifa letu dhidi ya maangamizi?
Mlenge
Wewe unataka nini? [/SIZE]
a) Tuvunje muungano kwa sababu sio waoga!
b) Tuweke ulinzi wa sungusungu Wakenya wasije iba rasilimali zetu?
c) a na b yote sahihi
Chagua jibu sahihi
Mikataba ya EAC imeshasainiwa na inaendelea kusainiwa kwa kasi mpya.
"Waraka wa Hamani" ushasainiwa.
Jamani, lipi la ziada tunaloweza kulifanya kuliokoa taifa letu dhidi ya maangamizi?
Mlenge