Salaams,
Kila kukicha ni wewe na kila uchao unavuma kwa mambo ambayo hayana msingi na wala hayana mwelekeo wa kuiendeleza Iramba Magharibi. Yawezekana umesahau jukumu lako kama mbunge wetu matokeo yake unafanya kazi za CCM na serikali ndani ya Bunge. Kumbuka kuwa wewe haupo bungeni kuiwakilisha serikali, au usalama wa taifa au CCM, upo bungeni kwa niaba ya wana Iramba Magharibi. Mengi unayozungumza bungeni ni yale uliyonayo kichwani mwako na si yale ambayo wana Iramba wamekutuma.
Huna sifa za kuwa mwakilishi wa wana Iramba. Ulipoteuliwa na wana CCM kugombea ubunge wana iramba wengi walidhani wamepata mtu wa kuisogeza Iramba. Niliwaskitikia sana wana Iramba wenzangu kwa kuwa na mtazamo huo. Ni kwa sababu walikuwa hawakujui. Mie niliyepata kukufahamu japo kidogo nilisikitika sana. Nakumbuka ulipokuwa UDSM kipindi kile cha mgomo wa kushinikiza marehem Mkili atolewe magereza, kila uliposimama kutoa hoja watu walikuzomea na kukutaka ukae chini. Si kwa sababu walikuwa wankuchukua, ila kwa sababu hukuwa na uwezo wa kujenga hoja za kushawishi watu. Hilo liko wazi, watanzania walio wengi wanakuzomea kila uzungumzapo bungeni. Sidhani kama hiyo ni sifa nzuri kwa kiongozi mzuri.
Umekuwa ukihusishwa na mambo mengi ya hovyo, wahenga walisema lisemwalo lipo.... Sidhani sana kama unajitambua na unatambua uyafanyayo. Wakati mwingine huwa nafikiri huenda yale maisha yako ya kukaa porini kwa muda mrefu ukichunga ng'ombe yaliathiri ukuaji wako kiakili kiasi kwamba hujitambui, huwezi kujenga hoja zikashawishi watu, ukatumiwa na wenzako kwa kila aina ya jambo lisilojema na wewe ukalibebea bango pasipo tafakuri ya kutosha. Ama kwa hakika umekuwa limbukieni wa kila jambo. Kumbuka cheo ni dhamana, na hukuzaliwa kuwa kiongozi milele. Muda wako utakwisha watakuja wengine nao watapita. Ni vema sasa ukatumia muda huu kufanya mambo ambayo watu watakukumbuka nayo kwa wema.
Ulikuwa mchunga ng'ombe hebu kumbuka kufanya mambo ambayo yatawasaidia wale wachunga ng'