Waraka maalum kwa watanzania wote

Waraka maalum kwa watanzania wote

NOTBOOK

Member
Joined
Sep 7, 2013
Posts
6
Reaction score
4
Karibu mwanaJF mzalendo,

Kwanza kabisa natoa shukrani zangu za dhati kwa watanzania ambao kila kukicha wako kazini kuakikisha Taifa ili linasonga mbele. Pia napenda kuwakumbusha wale wanaoigiza kufanya kazi na kuishia kula jasho la wengine kuwa "kazi ni msingi wa maendeleo"(Mwl Nyerere) .Biblia na Msaafu iko wazi kuhusu hilo, hasiyefanya kazi hasile na kufanya hivyo ni kumkufuru Allah /Mungu.

Napenda kuzungumzia mada hii katika Nyanja mbili yaani juu ya Viongozi na Wananchi .Nakuomba wewe mtanzania unaposoma hapa weka Itikadi zako pembeni na utangulize utaifa kwanza kwani katika kujadili mada hii nisingependa uanze matusi na maneno yasiyofaa hasa pale utapoona umeguswa!!!!

VIONGOZI :
Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na viongozi wengi lakini baadhi yao sio wasafi na wasio wasafi wanaweza kutakata iwapo watazingatia haya iwapo najua kuwa msema kweli ni mpenzi wa MUNGu na si mpenzi wa wanadamu.

Viongozi wa Tanzania tutumie muda mwingi kufikiri jinsi gani Tanzania inawezeza kuendelea na kuepukana na kuwa tegemezi tangu tupate uhuru hadi hapo mwisho wa dunia, kwani naamini kuwa mwisho wa dunia upo.

Tanzania iwe na sera na sheria nzuri na zinazotelezeka ambazo zina manufaa kwa watanzania wote badala ya kupoteza muda wa kurumbana kwa mambo yasiyo na maana, baadhi kutetea maslahi binafsiri ,baadhi kufanya biashara isiyo halali hasa ya unga,baadhi kupanga jinsi ya kumwagiana TINDIKALI ,kupigana mabomu,kufunguliana kesi rukuki zisizo na manufaa kwa taifa,baadhi kushambulia,kuteka na kupiga ua watetezi wa haki,baadhi kupanga jinsi ya kuficha mali za watanzania nje ya nchi,baadhi Kupanga vikosi vya kulinda wabadhilifu na wafisili wa Nchi yetu,rushwa kila kona,kila sekunde,kila saa,kila siku,kila wiki,kila mwezi,kila mwaka na miaka,baadhi kutoa ahadi feki,wizi wa kura,kubadilika badilika mithili ya kingonya,kupenda kuitwa waheshimiwa wakati tunayoyatenda hayafanani na kiongozi anayepaswa kuitwa mh,kupenda maisha ya juu sana kana kwamba hakuna kufa! Lakini tukumbuke "hakuna aliye wahi kuzikwa na mali au kwenda nayo mbinguni!!! Ukifa unafuatwa na mazuri au mabaya uliyotenda hapa duniani! Tumuige mwl Nyerere na Waziri Sokoine na asiyependa kuweka katika vitendo aliyoyapenda Nyerere na Sokoine hata kusifia na kunukuu maneno yao tusimsikie!

Msiwafanye watanzania wajutie kupata uhuru na kusema bora tungeendelea kuongozwa na wazungu (Mkoloni) maana baadhi ya viongozi, wananyonya zaidi ya mkoloni !!! ambaye hakubaliani na mimi ajiulize walau kidogo kwa kuangalia suala hili la ununuzi wa rada kwanini pesa ya ufisadi katika ununuzi wa rada inaitwa chenji ya rada! n.k

Pia nguvu zote zinatumika wakati wa kampaini za uchaguzi kama kutembelea wananchi ,kifanya vikao usiku na mchana,kuonesha kuwa mnatupenda! jamani hatukataza jitihada hizo kuendelea katika kuleta maendeleo kwenye jamii zetu.

Baadhi ya wawakilishi wetu tunaona wanavyokwepa bungeni na kujiendea kwenye mambo yao binafsi badala ya kututetea sisi tuliowachagua.Kuhusu hilo huwezi kuniambia kuwa ni dharura, lini robo tatu ,robo ya wabunge mkawa na dharura kwa wakati mmoja.
Na wengine tunawaona wanavyoshangilia tu pale sera mbovu za kutubana sinapojadiliwa mfano mzuri ni katika kupandisha kodi za kutuma na kupokea pesa kupitia simu ambazo kwa asilimia kubwa ndizo tunazozitumia vijijini kwani hakuna benki.

Hili limefanyika kwa kuwapandishia wenye makampuni ya simu na wao wakaamua kutubebesha sisi na mbaya zaidi nashangaa! ambao kwa vinywa vyao wanakazana kutubebesha pia kodi laini za simu ambayo kwetu sisi tunaona kama ni sawa na kututwika gunia la misumari bila ha kuweka kata! Pia ni walewale walioshangia wakati wa kuhusu mafao yetu tunayoweka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii! Na ukifika wakati wa uchaguzi utawaona wanyenyekevu na wengine wakidiliki kuwapigia magoti wapiga kura wao!

Baadhi ya viongozi mkimchagua anahama na kwenda kuishi Dar es salaam! Unapokuwa na kero yako unakwenda kwenye ofisi zao huwaoni utamkuta karani na kuanza kukuuliza wewe ni kada wa chama gani kumbe hawajui kuwa baadhi yetu tunachagua mtu kulingana na utendaji wake na si chama tena.

Baadhi ya Viongozi wamekuwa wa kuonekana kwenye msimu wa kampeini (Msimu wa kulima )na wakati wa mavuno wanajificha! bali misibani wamekuwa hawakosi na si kwamba wanakuwa wameguswa na mziba ila ni ili watu wawaone kuwa ni wema na si kwenye kuleta maendeleo kwa mtanzania.

Viongozi wetu sina shaka kama mtayarekebisha hayo mtaongoza vizuri ,mtapendwa na wapiga kura wenu hapatakuwepo na kuvunjiwa vioo vya magari yenu na wananchi kwa kushindwa kuheshimu mkataba mnaowekeana na wananchi kuwa wawachague muwawakilishe na pia ndipo mtabarikiwa japo sina hakika kama ni wote tunaoamini uwepo wa Mungu!

WANANCHI
Ndugu zangu watanzania kuweni waangalifu na viongozi wasiojali maslahi ya Tanzania, epukeni kuwa na upendo wa mshumaa wa kuchagua mtu akuwakilishe wakati unajua fika kuwa si mzalendo,ni mwizi na jambazi,tuache kulalamika,kushadadia mambo yasiyo na maana,kutumiwa na baadhi ya viongozi, tuache kupokea hongo (Zawadi) za wakati wa uchaguzi au zipokee lakini msiwachague bali fanyeni kazi kwa bidii na tuchague viongozi wema (fungu lililo jema) ambao tutashilikiana nao kuleta maendeleo ya Tanzania.

KURA YAKO WAKATI WA UCHAGUZI YAWEZA KUKUOKOA AU KUKUANGAMIZA WEWE NA UZAO WAKO WOTE.

Mwisho namalizia kwa kusema "maendeleo ya kweli yanalendwa na wananchi wenye"
 
9-7-2013 9-31-40 AMjf.png
 
Last edited by a moderator:
  • Huu mtazamo nimeupenda, Twapaswa kuamka watanzania
WANANCHI
Ndugu zangu watanzania kuweni waangalifu na viongozi wasiojali maslahi ya Tanzania, epukeni kuwa na upendo wa mshumaa wa kuchagua mtu akuwakilishe wakati unajua fika kuwa si mzalendo,ni mwizi na jambazi,tuache kulalamika,kushadadia mambo yasiyo na maana,kutumiwa na baadhi ya viongozi, tuache kupokea hongo (Zawadi) za wakati wa uchaguzi au zipokee lakini msiwachague bali fanyeni kazi kwa bidii na tuchague viongozi wema (fungu lililo jema) ambao tutashilikiana nao kuleta maendeleo ya Tanzania.

KURA YAKO WAKATI WA UCHAGUZI YAWEZA KUKUOKOA AU KUKUANGAMIZA WEWE NA UZAO WAKO WOTE.

Mwisho namalizia kwa kusema "maendeleo ya kweli yanalendwa na wananchi wenye"
 
Mkuu huku ni kuishiwa na hoja kabisa. Hapa hatuangalii amejiunga lini. Ameweka hoja yake hapa jamvini na sisi wana jamvi basi tuijadili kwa mapana, kama ni sehemu ya kumkosoa basi tumkosoe na kama ni kuunga hoja yake basi tufanye hivyo.

Unajua mkuu huyu aweza akawa ni bora kimichango ya hoja zake kuliko wewe uliejiunga kitambo hapa JF. Ugeni au wenyeji kwenye JF si kigezo cha kuwa na hoja zenye mashiko au pumba tupu. Fuatilia mada na jenga hoja, acha uhuni na utoto wa kukosoa vitu vya kijinga kabisa.

Mtoa mada amejitahidi sana kudadavua mambo ya msingi, na hayo ni mawazo yake tu haina maana kuwa basi alichokinena ni sheria. Jitahidi kuwa mstaarabu na pia uache ushamba wa kwenye social network. Kwa ujinga ulionao unafikiri kuwa wewe ni mjanja zaidi kwa kuwa uliwahi sana kujisajili hapa JF. Yawezekana tangu umepata usajili hapa hujawahi kutoa mada au michango ya maana. Kwa kweli watu wa aina kama yako wanalishusha hadhi jukwaa hili la magreat thinker.

Jaribu kuficha upumbavu wako japao kidogo ili angalau kwa namna moja au nyingine utakuwa umechangia ujenzi wa taifa.

Namaliza kwa kusema ”kuficha upumbavu katika jamii ya waerevu basi ni hatu moja katika kujifunza werevu”
 
Namaliza kwa kusema "kuficha upumbavu katika jamii ya waerevu basi ni hatu moja katika kujifunza werevu"
  • Ujumbe umefika, na kukuelewa vyema.
  • Uko sahihi, kila mmoja ana haki kisingi kutoa mawazo yake(kama ulivyoandika hapo juu),Ukizingatia watu tumetofautiana kiufahamu na uelewa.
  • Nilivutiwa na post ya ndugu yetu NotBook, na Kitu cha kwanza nilichonote, ni post yake niya kwanza na ipo makini. Hivyo sikuona kama kuna ubaya kumkaribisha JF. Je nikosa kweli kumwambia ndugu yetu notebook "karibu JF" sidhani.
  • Ila mkuu umekwenda mbali sana. Ila sikulaumu. Sababu Nafahamu kuwa binadamu tumetofautiana.
Nakutakia siku njema. Karibu
 
  • Ujumbe umefika, na kukuelewa vyema.
  • Uko sahihi, kila mmoja ana haki kisingi kutoa mawazo yake(kama
    ulivyoandika hapo juu),Ukizingatia watu tumetofautiana kiufahamu na
    uelewa.
  • Nilivutiwa na post ya ndugu yetu NotBook, na Kitu cha kwanza
    nilichonote, ni post yake niya kwanza na ipo makini. Hivyo sikuona kama
    kuna ubaya kumkaribisha JF. Je nikosa kweli kumwambia ndugu yetu
    notebook "karibu JF" sidhani.
  • Ila mkuu umekwenda mbali sana. Ila sikulaumu. Sababu Nafahamu kuwa
    binadamu tumetofautiana.
Nakutakia siku njema. Karibu

Ustaharabu ni kipimo,na kipimo cha ustaharabu ni jinsi ulivyo na kifua cha kudhibiti hasira zako. Nimefurahi ulivyomwelimisha ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom