Waraka maalum kwa Watanzania wote

Waraka maalum kwa Watanzania wote

MODS: Inawezekana kwamba hapa si mahala pa waraka huu, kutokana na maudhui yake. Lakini ukiangalia kwa undani, HAPA ndio mahala pake! Nawasilisha!

Ndugu Zangu Watanzania!

Nakuja kwenu leo nikiwa na waraka huu maalum ambao ni ushauri wangu wa nini kifanyike kuhusu hiki kinachoonekana kuwa mhemko au chokochoko za kidini hapa nchini. Kumbukeni, ni rahisi sana kuipoteza Amani kuliko kuirejesha. Tujihadhari, tusiangukie kwenye mikono ya Shetani, aliyelaaniwa na Mwenyezi-Mungu na kufukuzwa Mbinguni, naye akaapa kuwa Adui Namba Moja wa kila Mwanadam, yaani, kila mtu!

1. Zanzibar: Kama mnavyojionea, hali imekuwa sio shwari huko Zanzibar. Wakristo wanaishi katika hofu kuu ya kuumizwa, kuuwawa au kufanyiwa jambo lolote lile baya, wakati wowote. Nani wa kusema kwamba hali hii ikiendelea, haitafika hapa Bara? Hata kule Mbagala kuna kanisa lilichomwa moto. Lazima mkumbuke kwamba, kihistoria, vita zote mahali popote pale zilifanyika kwa sababu za KIUCHUMI! Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza na ya Pili, zote zilifanyika kwa sababu za KIUCHUMI.

Nani walifaidika? Walifaidika waliotaka kupora mali kutoka kwa matajiri wa mataifa ya Ulaya, Mashariki ya Kati na ya Mbali, walifaidika waliotaka kutengeneza na kuuza silaha, na pia, walifaidika waliotaka kupora ardhi na kila kilichomo ndani yake. Wakati wa Vita Kuu ya Pili, mali nyingi sana (michoro yenye thamani, vito, dhahabu, fedha nyingi) zilipora nchini Ujerumani, Uswisi, Austria, Italia, Uingereza na kwingineko, baada ya wenye kumiliki mali hizo kuuwawa kwenye mashambulizi ya angani na mabomu ya kurushwa kwa makombora na mizinga!Zanzibar kuna nini mpaka kutamaniwe kiasi hicho?

Zanzibar kuna vitalu tano vya mafuta na gesi, msiniulize nani kaniambia, lakini ninafahamu na nimethibitishiwa. Kiwango cha mafuta na gesi kilichopo Zanzibar ni KINGI kuliko kilichopo hapa Bara, kwa hiyo, wenye kuyatamani mafuta na gesi wanafanya kila hila, kuvuruga amani, kwa njia ya hofu ya kidini, ili ionekane kwamba Wazanzibari sasa hawawataki Wakristo ndani ya "nchi" yao. Hilo sio kweli.

Wazanzibari wengi (ambao nimeishi nao kwa muda mrefu huko Zanzibar) ni watu wema, wenye moyo wa ukarimu, na wenye kuwapenda hata wasio Waislam.

Ndio, kuna Wazanzibari ambao (kwa kuhamia kwao huko wanaitwa Wazanzibara... kwa jina la ukweli) ambao waliondoka kwenye Ukristo na kuingia kwenye Uislam, baada ya kuishi huko kwa muda mrefu, lakini pia kuna Wazanzibari wa kuzaliwa kwenye Uislam ambao nao pia waliondoka kwenye dini hiyo na kuingia kwenye Ukristo. Iweje leo, ghafla tu, hali kama hii iingie nchini humo na kuwatia hofu kuu Wakristo, kwamba sasa hawatakiwi nchini humo?

Hizi ni Njama za Shetani, kutaka kutuchonganisha, kupitia mgongo wa mafisadi: Makuwadi wa Vita na Makuwadi wa Nishati ya Petroli.

Mwenye kuusoma waraka huu amjulishe na mwenzake, na mwenzake, ili wote muweze KUMTAMBUA SHETANI na hila zake. Tusipojihadhari na kumrejea Mungu, TUTAANGAMIA! Hakika, TUMLAANI SHETANI!

2. Uchinjaji wa Nyama kwenye Mabucha: Hivi sasa kuna ujumbe mfupi wa simu unaosambaa kwa kasi kubwa sana, ambao unadai kwamba Wakristo wote sasa, kutokana na Azimio la Kanisa (halitajwi kanisa lipi), wanapaswa kuiombea na kuitakasa nyama inayonunuliwa kwenye bucha kwa Damu ya Yesu, kwa kuwa imechinjiwa kwenye madhabahu ya Kiislam kwa kutumia majini. Uislam sasa unahusishwa moja kwa moja na mambo ya kijini, yaani, ya kishetani.Tukumbuke kwamba hali hii haikuwapo hapo awali.

Mwangalieni Shetani jinsi alivyo! Anawachochea Wakristo kupigana na Waislam, kwa njia ya kulipa kisasi baada ya Wachungaji kuuwawa na Makanisa kuchomwa moto, huku anazidi kuwachochea Wakristo kuwatenga Waislam kwa kuihusisha dini yao na Ushetani, lakini pia, anazidi kuwatia hasira Waislam kwa kuihusisha dini yao na Ushetani! Mmemuona Shetani jinsi alivyo?

Wanaosambaza ujumbe huo mfupi wa simu wanafanya makusudi wakijua kwamba watawachochea Wakristo na Waislam kuchukiana. Muislam atamchukia Mkristo kwa kuwa Mkristo amemwambia Muislam kwamba dini yake ni ya Kishetani, huku Mkristo atamchukia Muislam KWA KUWA ameambiwa dini yake ni ya Kishetani. Shetani anatupiga vita kwa kila kona. TUMWOGOPE SANA SHETANI! TUMCHUKIE, TUMLAANI, TUMFUKUZE!

Si Muislam au Mkristo atakayepona na vita hii, TUSIPOJIHADHARI!Tunachopaswa kutambua ni kwamba:
1. Kuna Waislam, sio wote, ambao wanaamini katika mambo ya Ushirikina. Sio wote. Hakuna sehemu yoyote ile ambayo dini ya Kiislam inawafundisha Ushirikina waumini wa dini hiyo. Kwa hakika, Uislam UMEHARAMISHA Ushirikina! Vitabu vyote takatifu vya Kiislam VIMEHARAMISHA Ushirikina! Vimesema: Hakika ni mwenye hasara yule yote mwenye Kumshirikisha Mungu!

2. Kuna Wakristo, sio wote, ambao nao pia wako katika imani za Kishirikina. Nguvu za giza kwao ndio somo kuu. Wanaenda kwa waganga kuomba hiki na kile, badala ya kusali na kumwomba Mungu ulinzi, usalama na msaada wake, kama ilivyoainishwa kwenye Biblia na maandiko mengine takatifu!Kwa kuwa sasa mnatambua hili, nini kifanyike?​

Waislam, wameamrishwa kutamka neno "Bismillahi!" kila wanapochinja mnyama kwa ajili ya chakula, hii ina maana "Ninafanya hivi kwa jina la Mwenyezi-Mungu." Waislam hutamka hivyo pia wakati wa kula. Sikumbuki kama Wakristo wameamrishwa kumtaja Mwenyezi-Mungu wakati wa kuchinja, kwani uchinjaji wa wanyama ulianza tokea enzi za Nabii Abrahamu, ambaye wengi wetu ni wa kizazi chake. Lakini ninachojua kwamba, Wakristo husali na kumtaja Mwenyezi-Mungu wakati wa kula.

"Utamaduni" wa kuwaachia Waislam kuwa wachinjaji wa nyama ULIPOKEWA hapa nchini na dini zote, na kwa hakika, Wakristo wengi walikataa kula nyama ambayo ilikuwa HAIJACHINJWA NA MUISLAM. Wengi, wakati wakifanya sherehe za harusi, kipaimara, n.k., walisisitiza kwamba nyama itakayoliwa iwe IMECHINJWA NA MUISLAM, si vinginevyo.Imetokeaje mpaka leo ikaonekana kwamba nyama inayochinjwa na Muislam imemshirikisha Shetani kwa kupitia majini? Hamuoni kwamba HUU NI UCHONGANISHI MKUBWA wa Shetani?

Narudia tena, TUMWOGOPE SHETANI!

3. Hitimisho: Napenda kuhitimisha hapa leo kwa kusema yafuatayo:Mosi, sisi wote ni ndugu, Uzao wa Mungu kutoka kwa baba na mama yetu Adamu na Hawa. Ndio maana tukaitwa Wanadamu.Mungu alimuumba Adamu, ambaye ni mwanaume. Akampatia usingizi Adamu kisha akautoa ubavu wake mmoja na kumwumba Hawa, ambaye akamwita mwanamke, maana yake, ametokana na mwanaume.Kwa kuwa sisi wote ni ndugu, ila tuna imani tofauti za KUMWABUDU MWENYEZI-MUNGU, hakuna kati yetu mwenye HAKI ya kusema kwamba Muislam ni bora zaidi ya Mkristo, au Mkristo ni bora zaidi ya Muislam.

Sisi wote tuko SAWA MBELE YA MUNGU, kwa kuwa YEYE PEKEE ndiye mwenye HAKI ya kutukosoa na kutuhukumu. Sisi, ingawa Nabii Abrahamu alidiriki kusema na mwenyezi Mungu wakati akiwaombea watu wa Sodoma na Gomora, juu ya kwamba wakikutwa watu kumi tu ambao ni wema kwenye miji hiyo, basi wale waovu nao wasiangamizwe, hakika, Mwenyezi-Mungu amemwumba mwanadamu kwa mfano wake na amemfanya kuwa kiumbe bora zaidi kuliko viumbe wote ambao Mwenyezi-Mungu aliwaumba na kumpelekea Adamu awape majina.

Sasa, iweje leo sisi TUMUASI MUNGU, kwa kuua, kuhukumu, kuchoma moto makanisa, kuwatisha waja wake Mungu, na maasi mengine ambayo HAKIKA Shetani ametudanganya kuyafanya?Ndugu zangu, kumbukeni, kuipoteza Amani ni kuwafurahisha Makuwadi wa Vita na Makuwadi wa Nishati ya Petroli, ambao wote ni WAFUASI WA SHETANI! Hawa wanatokana na makundi ya Freemasons, Illuminati, Skulls and Bones na wengineo, ambao hufanya kazi zao kwenye maficho ya GIZA (Usiku), na si mchana kweupe, kwani mwanga wa jua la mchana unang'aa na kuleta amani, wakati mwanga wa mwezi wa usiku si mkubwa, unaruhusu kuwapo kwa Shetani miongoni mwa wanadamu.

Tafadhali sambazeni waraka huu kwa wanadamu wote waishio Tanzania, sio tu kwa Wakristo na Waislam, bali kwa Wapagani, Wahindu, Wabudhha, Wa Bah'ai, na imani zote nyingine ambazo zina waumini wake hapa nchini.

Vita ikianza, haitambagua mtu kwa imani yake.

Amani ya Bwana Wetu iwe nanyi.

Amina!

Kwa sababu tulikubali wao wachinje sisi tule haiwapi haki ya kuwa lazima wachinje hata nyama za kwenye misiba yetu. Pia haitushushi mpaka wamefikia kutuita MAKHAFILI kama akina Ustaazi ILUNGA wanatuita.
 
1. Kuna Waislam, sio wote, ambao wanaamini katika mambo ya Ushirikina. Sio wote. Hakuna sehemu yoyote ile ambayo dini ya Kiislam inawafundisha Ushirikina waumini wa dini hiyo. Kwa hakika, Uislam UMEHARAMISHA Ushirikina! Vitabu vyote takatifu vya Kiislam VIMEHARAMISHA Ushirikina! Vimesema: Hakika ni mwenye hasara yule yote mwenye Kumshirikisha Mungu!​

Na katika hilo la majini, Mungu amelieleza kwenye sura mbalimbali za Kuran, Mathalani:

Na (wakumbushe) siku atakapowakusanya wote, (awaambie): "enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanadamu." Na marafiki zao katika wanadamu(watawagombania) waseme: "Mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao, na umefika muda wetu uliotuwekea." Basi(Mungu) atasema: "moto ndio makazi yenu, mtakaa humo milele" ila apende Mwenyezi Mungu(kuwarehemu); hakaika Mola wako ndiye mwenye hikima (na) ndiye ajuaye!

Huo ndio msimamo wa Uislamu kuhusu majini! Na kuna aya zingine kadhaa kama hizo zinazozungumzia majini achilia mbali suala la ushirikina! Lakini pamoja na yote, bado ndugu zetu Wakristo wamekuwa washadadiaji wakuu wa kueneza propaganda za kuhusisha Uislamu na majini! Na kuna aya kadhaa wa kadhaa ambazo Waislamu tunaaswa kuzisoma ili kujikinga na majini....sasa hapo ndipo mwenye akili yake angepaswa kushangaa kama Uislamu na Majini ni chanda na pepe, ni kwanini basi pawe na aya kadhaa za kusoma ili kujilinda na majini!

Matokeo yake ni nini sasa! Kama ulivyoeleza kwa ufasaha mtoa mada! Hakuna Mwislamu ambae anaweza kuchekelea kila siku kuambiwa dini yake ni dini ya kishetani wakati ndani ya maandiko kuna rundo la aya za kumlaani shetani!
 
Kwa sababu tulikubali wao wachinje sisi tule haiwapi haki ya kuwa lazima wachinje hata nyama za kwenye misiba yetu. Pia haitushushi mpaka wamefikia kutuita MAKHAFILI kama akina Ustaazi ILUNGA wanatuita.
Msafiri,
Wewe ni muathirika tu wa propaganda....Kafir sio tusi wala neno la kejeli! Kwa mujibu wa Ukristo, hata mimi ni Kafir kwavile siamini kwamba Yesu ni Mungu, au Yesu alikufa na kufufuka! Maana ya Kafir ni Unbeliever, mtu asiyeamini! Na ndio maana nikasema kv wewe ni Mkristo nami ni Muislamu, unaweza kuniita Kafir coz' I don't believe what you believe! Kafiri ni neno la Kiarabu lenye maana ya Unbeliever! sasa tatizo liko wapi? Wewe unaiamini Kuran?
 
Kinachoudhi zaidi ni hizi busara zinazojitokeza hivi sasa baada ya matukio.......kwanini watu mnazificha busara zenu wakati wahadhiri wakikashifiana kila kukicha.......if we all have sense......tokea sasa hivi tuseme mihadhara basi na kama mihadhara inaendelea basi iwe kuhusu imani za wahusika tu........Radio za kidini zihubiri yanayohusu imani zao tu......magazeti ya kidini yaandike yanahusu imani zao tu........ofcourse media hizo zitumike pia kuwafundisha waumini wao upendo, amani na kuvumiliana........sidhani kama kuna ugumu kwenye hayo........

Atakayejitokeza kukashifu au kuchochea uvunjaji wa amani na upendo kwa njia yeyote ile ashughulikiwe mara moja........kuanzia kwenye dini husika hadi vyombo vya dola..........sio kusubiri matukio ndio tuanze kutoa busara.....
 
MODS: Inawezekana kwamba hapa si mahala pa waraka huu, kutokana na maudhui yake. Lakini ukiangalia kwa undani, HAPA ndio mahala pake! Nawasilisha!

Ndugu Zangu Watanzania!

Nakuja kwenu leo nikiwa na waraka huu maalum ambao ni ushauri wangu wa nini kifanyike kuhusu hiki kinachoonekana kuwa mhemko au chokochoko za kidini hapa nchini. Kumbukeni, ni rahisi sana kuipoteza Amani kuliko kuirejesha. Tujihadhari, tusiangukie kwenye mikono ya Shetani, aliyelaaniwa na Mwenyezi-Mungu na kufukuzwa Mbinguni, naye akaapa kuwa Adui Namba Moja wa kila Mwanadam, yaani, kila mtu!

1. Zanzibar: Kama mnavyojionea, hali imekuwa sio shwari huko Zanzibar. Wakristo wanaishi katika hofu kuu ya kuumizwa, kuuwawa au kufanyiwa jambo lolote lile baya, wakati wowote. Nani wa kusema kwamba hali hii ikiendelea, haitafika hapa Bara? Hata kule Mbagala kuna kanisa lilichomwa moto. Lazima mkumbuke kwamba, kihistoria, vita zote mahali popote pale zilifanyika kwa sababu za KIUCHUMI! Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza na ya Pili, zote zilifanyika kwa sababu za KIUCHUMI.

Nani walifaidika? Walifaidika waliotaka kupora mali kutoka kwa matajiri wa mataifa ya Ulaya, Mashariki ya Kati na ya Mbali, walifaidika waliotaka kutengeneza na kuuza silaha, na pia, walifaidika waliotaka kupora ardhi na kila kilichomo ndani yake. Wakati wa Vita Kuu ya Pili, mali nyingi sana (michoro yenye thamani, vito, dhahabu, fedha nyingi) zilipora nchini Ujerumani, Uswisi, Austria, Italia, Uingereza na kwingineko, baada ya wenye kumiliki mali hizo kuuwawa kwenye mashambulizi ya angani na mabomu ya kurushwa kwa makombora na mizinga!Zanzibar kuna nini mpaka kutamaniwe kiasi hicho?

Zanzibar kuna vitalu tano vya mafuta na gesi, msiniulize nani kaniambia, lakini ninafahamu na nimethibitishiwa. Kiwango cha mafuta na gesi kilichopo Zanzibar ni KINGI kuliko kilichopo hapa Bara, kwa hiyo, wenye kuyatamani mafuta na gesi wanafanya kila hila, kuvuruga amani, kwa njia ya hofu ya kidini, ili ionekane kwamba Wazanzibari sasa hawawataki Wakristo ndani ya "nchi" yao. Hilo sio kweli.

Wazanzibari wengi (ambao nimeishi nao kwa muda mrefu huko Zanzibar) ni watu wema, wenye moyo wa ukarimu, na wenye kuwapenda hata wasio Waislam.

Ndio, kuna Wazanzibari ambao (kwa kuhamia kwao huko wanaitwa Wazanzibara... kwa jina la ukweli) ambao waliondoka kwenye Ukristo na kuingia kwenye Uislam, baada ya kuishi huko kwa muda mrefu, lakini pia kuna Wazanzibari wa kuzaliwa kwenye Uislam ambao nao pia waliondoka kwenye dini hiyo na kuingia kwenye Ukristo. Iweje leo, ghafla tu, hali kama hii iingie nchini humo na kuwatia hofu kuu Wakristo, kwamba sasa hawatakiwi nchini humo?

Hizi ni Njama za Shetani, kutaka kutuchonganisha, kupitia mgongo wa mafisadi: Makuwadi wa Vita na Makuwadi wa Nishati ya Petroli.

Mwenye kuusoma waraka huu amjulishe na mwenzake, na mwenzake, ili wote muweze KUMTAMBUA SHETANI na hila zake. Tusipojihadhari na kumrejea Mungu, TUTAANGAMIA! Hakika, TUMLAANI SHETANI!

2. Uchinjaji wa Nyama kwenye Mabucha: Hivi sasa kuna ujumbe mfupi wa simu unaosambaa kwa kasi kubwa sana, ambao unadai kwamba Wakristo wote sasa, kutokana na Azimio la Kanisa (halitajwi kanisa lipi), wanapaswa kuiombea na kuitakasa nyama inayonunuliwa kwenye bucha kwa Damu ya Yesu, kwa kuwa imechinjiwa kwenye madhabahu ya Kiislam kwa kutumia majini. Uislam sasa unahusishwa moja kwa moja na mambo ya kijini, yaani, ya kishetani.Tukumbuke kwamba hali hii haikuwapo hapo awali.

Mwangalieni Shetani jinsi alivyo! Anawachochea Wakristo kupigana na Waislam, kwa njia ya kulipa kisasi baada ya Wachungaji kuuwawa na Makanisa kuchomwa moto, huku anazidi kuwachochea Wakristo kuwatenga Waislam kwa kuihusisha dini yao na Ushetani, lakini pia, anazidi kuwatia hasira Waislam kwa kuihusisha dini yao na Ushetani! Mmemuona Shetani jinsi alivyo?

Wanaosambaza ujumbe huo mfupi wa simu wanafanya makusudi wakijua kwamba watawachochea Wakristo na Waislam kuchukiana. Muislam atamchukia Mkristo kwa kuwa Mkristo amemwambia Muislam kwamba dini yake ni ya Kishetani, huku Mkristo atamchukia Muislam KWA KUWA ameambiwa dini yake ni ya Kishetani. Shetani anatupiga vita kwa kila kona. TUMWOGOPE SANA SHETANI! TUMCHUKIE, TUMLAANI, TUMFUKUZE!

Si Muislam au Mkristo atakayepona na vita hii, TUSIPOJIHADHARI!Tunachopaswa kutambua ni kwamba:
1. Kuna Waislam, sio wote, ambao wanaamini katika mambo ya Ushirikina. Sio wote. Hakuna sehemu yoyote ile ambayo dini ya Kiislam inawafundisha Ushirikina waumini wa dini hiyo. Kwa hakika, Uislam UMEHARAMISHA Ushirikina! Vitabu vyote takatifu vya Kiislam VIMEHARAMISHA Ushirikina! Vimesema: Hakika ni mwenye hasara yule yote mwenye Kumshirikisha Mungu!

2. Kuna Wakristo, sio wote, ambao nao pia wako katika imani za Kishirikina. Nguvu za giza kwao ndio somo kuu. Wanaenda kwa waganga kuomba hiki na kile, badala ya kusali na kumwomba Mungu ulinzi, usalama na msaada wake, kama ilivyoainishwa kwenye Biblia na maandiko mengine takatifu!Kwa kuwa sasa mnatambua hili, nini kifanyike?​

Waislam, wameamrishwa kutamka neno "Bismillahi!" kila wanapochinja mnyama kwa ajili ya chakula, hii ina maana "Ninafanya hivi kwa jina la Mwenyezi-Mungu." Waislam hutamka hivyo pia wakati wa kula. Sikumbuki kama Wakristo wameamrishwa kumtaja Mwenyezi-Mungu wakati wa kuchinja, kwani uchinjaji wa wanyama ulianza tokea enzi za Nabii Abrahamu, ambaye wengi wetu ni wa kizazi chake. Lakini ninachojua kwamba, Wakristo husali na kumtaja Mwenyezi-Mungu wakati wa kula.

"Utamaduni" wa kuwaachia Waislam kuwa wachinjaji wa nyama ULIPOKEWA hapa nchini na dini zote, na kwa hakika, Wakristo wengi walikataa kula nyama ambayo ilikuwa HAIJACHINJWA NA MUISLAM. Wengi, wakati wakifanya sherehe za harusi, kipaimara, n.k., walisisitiza kwamba nyama itakayoliwa iwe IMECHINJWA NA MUISLAM, si vinginevyo.Imetokeaje mpaka leo ikaonekana kwamba nyama inayochinjwa na Muislam imemshirikisha Shetani kwa kupitia majini? Hamuoni kwamba HUU NI UCHONGANISHI MKUBWA wa Shetani?

Narudia tena, TUMWOGOPE SHETANI!

3. Hitimisho: Napenda kuhitimisha hapa leo kwa kusema yafuatayo:Mosi, sisi wote ni ndugu, Uzao wa Mungu kutoka kwa baba na mama yetu Adamu na Hawa. Ndio maana tukaitwa Wanadamu.Mungu alimuumba Adamu, ambaye ni mwanaume. Akampatia usingizi Adamu kisha akautoa ubavu wake mmoja na kumwumba Hawa, ambaye akamwita mwanamke, maana yake, ametokana na mwanaume.Kwa kuwa sisi wote ni ndugu, ila tuna imani tofauti za KUMWABUDU MWENYEZI-MUNGU, hakuna kati yetu mwenye HAKI ya kusema kwamba Muislam ni bora zaidi ya Mkristo, au Mkristo ni bora zaidi ya Muislam.

Sisi wote tuko SAWA MBELE YA MUNGU, kwa kuwa YEYE PEKEE ndiye mwenye HAKI ya kutukosoa na kutuhukumu. Sisi, ingawa Nabii Abrahamu alidiriki kusema na mwenyezi Mungu wakati akiwaombea watu wa Sodoma na Gomora, juu ya kwamba wakikutwa watu kumi tu ambao ni wema kwenye miji hiyo, basi wale waovu nao wasiangamizwe, hakika, Mwenyezi-Mungu amemwumba mwanadamu kwa mfano wake na amemfanya kuwa kiumbe bora zaidi kuliko viumbe wote ambao Mwenyezi-Mungu aliwaumba na kumpelekea Adamu awape majina.

Sasa, iweje leo sisi TUMUASI MUNGU, kwa kuua, kuhukumu, kuchoma moto makanisa, kuwatisha waja wake Mungu, na maasi mengine ambayo HAKIKA Shetani ametudanganya kuyafanya?Ndugu zangu, kumbukeni, kuipoteza Amani ni kuwafurahisha Makuwadi wa Vita na Makuwadi wa Nishati ya Petroli, ambao wote ni WAFUASI WA SHETANI! Hawa wanatokana na makundi ya Freemasons, Illuminati, Skulls and Bones na wengineo, ambao hufanya kazi zao kwenye maficho ya GIZA (Usiku), na si mchana kweupe, kwani mwanga wa jua la mchana unang'aa na kuleta amani, wakati mwanga wa mwezi wa usiku si mkubwa, unaruhusu kuwapo kwa Shetani miongoni mwa wanadamu.

Tafadhali sambazeni waraka huu kwa wanadamu wote waishio Tanzania, sio tu kwa Wakristo na Waislam, bali kwa Wapagani, Wahindu, Wabudhha, Wa Bah'ai, na imani zote nyingine ambazo zina waumini wake hapa nchini.

Vita ikianza, haitambagua mtu kwa imani yake.

Amani ya Bwana Wetu iwe nanyi.

Amina!

Nadiriki kusema kuwa this is the best post tangu misukosuko hii ya kidini ianze. Asante sana MwanaHaki Mungu akubariki...
 
Last edited by a moderator:
MODS: Inawezekana kwamba hapa si mahala pa waraka huu, kutokana na maudhui yake. Lakini ukiangalia kwa undani, HAPA ndio mahala pake! Nawasilisha!

Ndugu Zangu Watanzania!

Nakuja kwenu leo nikiwa na waraka huu maalum ambao ni ushauri wangu wa nini kifanyike kuhusu hiki kinachoonekana kuwa mhemko au chokochoko za kidini hapa nchini. Kumbukeni, ni rahisi sana kuipoteza Amani kuliko kuirejesha. Tujihadhari, tusiangukie kwenye mikono ya Shetani, aliyelaaniwa na Mwenyezi-Mungu na kufukuzwa Mbinguni, naye akaapa kuwa Adui Namba Moja wa kila Mwanadam, yaani, kila mtu!

1. Zanzibar:

Zanzibar kuna vitalu tano vya mafuta na gesi, msiniulize nani kaniambia, lakini ninafahamu na nimethibitishiwa. Kiwango cha mafuta na gesi kilichopo Zanzibar ni KINGI kuliko kilichopo hapa Bara, kwa hiyo, wenye kuyatamani mafuta na gesi wanafanya kila hila, kuvuruga amani, kwa njia ya hofu ya kidini, ili ionekane kwamba Wazanzibari sasa hawawataki Wakristo ndani ya "nchi" yao. Hilo sio kweli.

Wazanzibari wengi (ambao nimeishi nao kwa muda mrefu huko Zanzibar) ni watu wema, wenye moyo wa ukarimu, na wenye kuwapenda hata wasio Waislam.

Si Muislam au Mkristo atakayepona na vita hii, TUSIPOJIHADHARI!Tunachopaswa kutambua ni kwamba:
1. Kuna Waislam, sio wote, ambao wanaamini katika mambo ya Ushirikina. Sio wote. Hakuna sehemu yoyote ile ambayo dini ya Kiislam inawafundisha Ushirikina waumini wa dini hiyo. Kwa hakika, Uislam UMEHARAMISHA Ushirikina! Vitabu vyote takatifu vya Kiislam VIMEHARAMISHA Ushirikina! Vimesema: Hakika ni mwenye hasara yule yote mwenye Kumshirikisha Mungu!

2. Kuna Wakristo, sio wote, ambao nao pia wako katika imani za Kishirikina. Nguvu za giza kwao ndio somo kuu. Wanaenda kwa waganga kuomba hiki na kile, badala ya kusali na kumwomba Mungu ulinzi, usalama na msaada wake, kama ilivyoainishwa kwenye Biblia na maandiko mengine takatifu!Kwa kuwa sasa mnatambua hili, nini kifanyike?

Waislam, wameamrishwa kutamka neno "Bismillahi!" kila wanapochinja mnyama kwa ajili ya chakula, hii ina maana "Ninafanya hivi kwa jina la Mwenyezi-Mungu." Waislam hutamka hivyo pia wakati wa kula. Sikumbuki kama Wakristo wameamrishwa kumtaja Mwenyezi-Mungu wakati wa kuchinja, kwani uchinjaji wa wanyama ulianza tokea enzi za Nabii Abrahamu, ambaye wengi wetu ni wa kizazi chake. Lakini ninachojua kwamba, Wakristo husali na kumtaja Mwenyezi-Mungu wakati wa kula.

"Utamaduni" wa kuwaachia Waislam kuwa wachinjaji wa nyama ULIPOKEWA hapa nchini na dini zote, na kwa hakika, Wakristo wengi walikataa kula nyama ambayo ilikuwa HAIJACHINJWA NA MUISLAM. Wengi, wakati wakifanya sherehe za harusi, kipaimara, n.k., walisisitiza kwamba nyama itakayoliwa iwe IMECHINJWA NA MUISLAM, si vinginevyo.Imetokeaje mpaka leo ikaonekana kwamba nyama inayochinjwa na Muislam imemshirikisha Shetani kwa kupitia majini? Hamuoni kwamba HUU NI UCHONGANISHI MKUBWA wa Shetani?

Amina!

Ndugu yangu mpendahaki, ni vema kuwa hufurahiswi na yanayotokea lakini walaka wako unatia shaka na haulengi kutoa hamasa ya amani hata kidogo. Ingekuwa vema kama ungejikita kwenye kusisitiza tu amani na upendo katika jamii lakini si kutoa mahitimisho na maangalizo ambayo mtu yeyote makini anajua si kweli ila mnajaribu tu kung'ata na kupooza.

" ili ionekane kwamba Wazanzibari sasa hawawataki Wakristo ndani ya "nchi" yao. Hilo sio kweli.
Wazanzibari wengi (ambao nimeishi nao kwa muda mrefu huko Zanzibar) ni watu wema, wenye moyo wa ukarimu, na wenye kuwapenda hata wasio Waislam."

Ukweli ni kwamba si wanzanzibari wasiowataka wakristo bali waislam wa zanzibari hawawataki wakristo zanzibar, na si kweli kuwa wanawapenda hata wasiokuwa waislam bali wanawachukia to death. ntakupa mifano.

  • katika muda nilioishi zanzibar (pemba na unguja) hasa pemba, wakristo wanadharaurika sana na kuna wakati wananyimwa haki zao za msingi kabisa. Kwa mfano wakati wa mfungo wa ramadhani mkristo anakatazwa kula chakula maeneo ya wazi mpaka ajifungie ndani na tena anapopika afunge madirisha ili harufu isitoke nje (hii iko hasa pemba). lakini ikifika kwaresma wenzetu wanajichana hadharani na si tatizo kwa yeyote, sasa hapo mapenzi yakowapi? nimewai kupelekwa kituo cha polisi wete kwa kula aple balabalani wakati wa mwezi huu
  • ukipita pemba kuna kanda za miadhara zinazowakashifu wakristu zinaitwa "tokomeza mfumo kristo" kanda hizi kila cable ya hoteli ya pemba kuna chanel TV inazirusha siku nzima pia mitaani hufunguliwa kwa sauti ya juu katika vibanda mbali mbali, kwa nguvu sana. Heshima na upendo viko wapi
  • Kumekuwa na waraka mbalimbali zanazotolewa unguja zikihamasisha waislam kuhujum waumini wa kikristo na mali zao.kwa yeyote aliyeishi zanzibar hata kwa wiki tu, na ukafanikiwa kupita mitaani lazima utakutana na waraka hizi.Upendo uko wapi?
  • Jumuiya ya UAMSHO imeshatangaza rasmi kuwa ukristo hautakiwi zanzibar..Je hao si waislamu?si wazanzbari?
  • Je hujamsikia ILUNGA akihamasiha waislamu kuua mapadri,askofu na watawa tana bila sababu.Huo ni upendo?

" Wengi, wakati wakifanya sherehe za harusi, kipaimara, n.k., walisisitiza kwamba nyama itakayoliwa iwe IMECHINJWA NA MUISLAM, si vinginevyo.Imetokeaje mpaka leo ikaonekana kwamba nyama inayochinjwa na Muislam imemshirikisha Shetani kwa kupitia majini? Hamuoni kwamba HUU NI UCHONGANISHI MKUBWA wa Shetani?"

Swala la kuchinja ni la mazoea na si makubaliano kama wenzetu wanavyolichukulia..hakuna sehemu wala nyaraka zozote zinazoonyesha kuwa wakristo waliwai kukaa na waislamu wakakubaliana kuwa waislamu watakua "official" wachinjaji katika nchi hii.
Swala ni je kama mkristo akichinja nyama na akala na wakristo wenzake inawaathiri nini waislamu?Mbona kitimoto zinauzwa na wakristo na kuandaliwa nao na si hoja tena.Kama wanavyouziana kitimoto waacheni wauziane nyama pia ya kawaida ilimradi hakuna mkristo anayemlazimisha muislamu kula hiyo nyama.
Tusigeuze mazoea kuwa Sheria na kuanza kuyatumia kuhukumu wenzetu...

Huwezi kusuruhisha matatizo kwa kutunga sababu zako mwenyewe za hayo matatizo na kutaka watu wakuamini, hata siku moja? Ni sawa na kusema kwamba Padri Everist amekufa kwa "MAPENZI YA MUNGU".Mungu gani, wanamdanganya nani?huo ndo utunzi wa sababu wenye malengo ya kutetea uharifu.

KIMSINGI HAUJA ADDRESS SABABU ZA MATATIZO HAYA ...you dont address serious probles with simple solutions brother. call a spade, spade and not kijiko
 
Uislam wenyewe UNAMLAANI huyo Sheikh Ilunga, kwani HAKUNA mahali Mwenyezi Mungu anawaamrisha Waislam WAUE! Haki ya kutoa roho ni yake Mwenyezi Mungu PEKEE! Hata kwenye Kuraini imeandikwa USIUE!

Ilunga HANA TOFAUTI na Shetani. Ayasemayo mdomoni mwake si yake, bali ni ya Shetani, kutokana na ukweli kwamba yeye SI MUUMINI HALISI wa Kiislam! Angekuwa hivyo, ANGEMWOGOPA SANA Mungu!

Kumbuka, Waislam wengi wana elimu duni sana. Hata kwenye Uislam, elimu inahamasishwa. Unaambiwa, ukitaka kumjua Mungu sharti uwe na elimu. Unahitaji Elimu Dunia na Elimu Ahera ili kumjua Mungu na uweze kuepuka na moto wa Jehanam. Waislam wengi ni sawa na BENDERA FUATA UPEPO. Hawana elimu. Viongozi wao, halikadhalika, wako wako tu! Unadhani watu hawa hawatakosa kuwa karibu na Shetani?

Usiiangalie dini ya Kiislam kwa matendo ya Waislam wachache. Iangalie kwa kile inachofundisha. Mimi ninawachallenge WAISLAM WOTE watakaosoma waraka huu, wanitafutie aya zinazoamrisha Waislam kuua mtu yeyote, aliye au asiye Mkristo! Hayo wanayoyafanya huyo Zanzibar HAYAMO katika kitabu chochote kile cha dini ya Kiislam! NI USHENZI TU! HUO SI UISLAM!

Kama nilivyosema, TUMWOGOPE SHETANI!
 
Kwanza nikushukuru kwa kuueleza ni kwa jinsi gani vita hii isivyonufaisha upande wowote. Lakini sikubaliani na wewe hasa maelezo yako niliyoyapa rangi nyekundu. Inaelekea hukujua ni kwanini wakristo waliamua kuliacha suala la kuchinja kubaki kwa waislamu. Si kwamba walikuwa hahwawezi kula nyama iliyochinjwa na mkristo mwenzao ila hawakuona sababu ya wengine (waislamu kutokujumika nao kwenye chakula kwasababu tu hawakuchinja wao. Tatizo linakuja baada ya waislamu kujihalalishia kuwa wao pekee ndio wanaotakiwa kuchinja na si vinginevyo. Sasa hii inatafsiriwa kama dharau kwa imani ya wakristo kwamba wao hahwezi kuchinja. Na kama kuchinja ni ibada kwanini wakristo washiriki ibada ya imani wasio iamini. Ukimya wa wakristo kwenye suala la kuchinja lisitafsiriwe kuwa wao walilidhia kuwa bila waislamu kuchinja wao hawawezi kula nyama hiyo SI KWELI.

Ila naungana na wewe kuwa vita hii haina mwenyewe na haiwezi kuwa na mshidi. They will all loose the war.

Kaka nakukubali kwa hili. Na kingine ni suala zima la kipato. Wenye mabucha/yeyote anapopeleka mnyama machinjioni hulipa Ada ya kuchinja ambayo kwa utaratibu huu wa sasa, maana yake ni kuwa watu wamenyang'anywa moja ya vyanzo vya mapato na kuonekana kuwa wenye haki ya kipato kinachotokana na kuchinja ni waislam tu. Sasa wengine wakale polisi.? Ni suala la kutafakari kwa undani sana na si la kukurupuka tu
 
Back
Top Bottom