Waraka maalum - BAVICHA

kax bedui Jr

Senior Member
Aug 11, 2015
134
96
Nimeamua kuandika WARAKA huu maalum kwa baraza la vijana la chama yaani BAVICHA kwa uwazi kwa sababu za msingi ambazo nitazieleza hapo baadae. Naamini katika uwazi na kuheshimiana katika mawazo na hoja. Naamini katika demokrasia ya kweli ya vitendo siyo ya kwenye maandishi peke yake. Ndiyo maana nimeandika kwa uwazi.
-Bavicha ni tawi la chama au kiungo ndani ya chama. Kwa tafsiri pana Bavicha ni taasisi ndogo na huru ndani ya taasisi kubwa iitwayo Chadema. Hivyo ni tarajio letu wana chama na hasa vijana kuwa BAVICHA itawajibika kuhakikisha maslahi ya chama na Vijana yanalindwa ndani ya chama.
Hali imekuwa tofauti sana katika kipindi hiki. Bavicha imekuwa kama HAIPO, ili Bavicha isikike ni lazima CCM wapige "ngoma" ili Bavicha wacheze nayo kwenye media mbali mbali ikiwemo mitandao ya kijamii. Ikiisha hiyo ngoma basi Bavicha nayo inapoa, inageukia siasa za matukio ya serikalini!! Political wing ya chama Kikuu cha upinzani nchini inacheza ngoma ya chama tawala, hakika kweli tuna safari ndefu ya kujiandaa vizuri kushika dola.
-Huu UKWELI MCHUNGU wengi hawapendi usemwe na wengi hawawezi kusema wazi kwa sababu ya kulinda maslahi yao binafsi ikiwemo nafasi za uongozi. Kuna mambo kadhaa ndani ya Bavicha hayako sawa, nitafafanua hapa kwa hoja na ikibidi nitaomba kujibiwa kwa hoja pia:-

1. Nafasi ya mwenyekiti wa Bavicha "imepwaya sana". Mwenyekiti wa Bavicha Taifa katika nafasi hii nakiri wazi imekuwa kubwa kuliko uwezo wake. Utaniuliza nasema imepwaya nikilinganisha na nani au nikilinganisha na nafasi ya nani?? Jibu rahisi sana.
John Heche mbunge wa Tarime vijijini asiye ogopa nani atamsahau kirahisi?? Huyu alikuwa mwenyekiti wa Bavicha kabla ya Patrobas Katambi. Heche hana uwoga wala hakuwa na uwoga wakati wa uongozi wake.Ndiyo maana rafiki zangu baadhi walisema Bavicha ya kweli iliondoka na Heche.
Kuna haja ya Mwenyekiti sasa kujitazama upya. Siasa za "kushangaa au kuzubaa" kwa sasa na hasa nyakati hizi tulizo nazo hazitakiwi. Naamini katika hili na kwa ukweli huu mchungu utafanyiwa kazi. Furaha yangu ni kuona Bavicha inakuwa imara kila siku.

2. Bavicha imekosa "mipango na hoja mbadala" za kukisaidia chama. Huu nao ni ukweli mchungu ambao wafia chama wasio weza kufikiri vizuri watapinga. Bavicha ilitakiwa kuwa na mikakati yake thabiti nje ya mikakati ya pamoja kama chama. Imefika mahali uhai wa Bavicha unategemea chama kitasema nini au chama kitakuja na operation gani.
-Ilipokuja operation UKUTA, Bavicha ikaonekana iko hai. Ilipo ondoka Bavicha ikarudia kwenye siasa zile zilizo zoeleka za kusubiri matukio ya chama tawala!! Kwa mwendo huu Bavicha inapotea kwa kujitakia.

3. Migogoro mbali mbali ya ndani kati ya Bavicha na CHASO. Mpaka sasa hakuna connection nzuri kabisa kati ya Bavicha na Chaso. Wa kufanya connection hii siyo chama pekee, Bavicha inahusika sana lakini ipo tu, viongozi wa Bavicha wanasubiri mahafali ya wanafunzi walio ndani ya Chaso ili waonekane wana umoja lakini ni tofauti.
Ngoja nitoe mfano, tazama upande wa pili (CCM). Umoja wa vijana wa CCM yaani Uvccm wana coordination nzuri sana na jumuiya za wasomi wa vyuo vikuu ambao ni wana CCM. Network yao siyo ya mitandaoni pekee, inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha CCM ina salimika baada ya kupoteza mwelekeo.

4. Siasa za kulalamika, matamko na vikundi vikundi kwenye mitandao ya kijamii. Kwa siasa za sasa kulalamika ni kelele kwa Wananchi na watawala. Matamko pekee yanatafsiriwa kama mbinu za kutafuta "kiki" hata kama hayana nia hiyo. Vikundi vikundi kwenye mitandao ya kijamii ambavyo vimekuwa "kama" ngao ya Bavicha si jambo jema. Siasa za kulalamika bila kuonyesha njia mbadala ni siasa za kizembe, ni siasa za Afrika ya zamani!!
-Na viongozi Bavicha someni alama za nyakati, utawala wa sasa hauogopi matamko. Unaweza kupewa kibali cha kutoa matamko unavyo taka lakini utawala huu uko makini sana kutazama hatua zinazo chukuliwa baada ya matamko. Bavicha matamko ni mengi sana lakini matendo.......... Mifano ipo mingi sana ya matamko.
-Nini kilifuata baada ya tamko kuhusu wanafunzi walio kosa mikopo?? Tamko la kuzuia mkutano wa CCM Dodoma?? Tuna strategies za kimatamko lakini tuna "implementation measures"?? Kama hatuna tuna fanya nini kuhakikisha matamko hayo yanakuwa na impact chanya?? Baada ya matamko tunatoa mrejesho?? Kwa nani, ili iweje??
Athari za mitandao ya kijamii ni kubwa sana, migogoro mingi imeanzia huko kwenye vikundi, Mtu akikosoa anaitwa CCM, ana njaa, msaliti, ametumwa kisha anaondolewa na hapewi nafasi ya kulinda hoja zake au kujibiwa kwa hoja kwa sababu tu kasema ukweli mchungu, alafu tunadai demokrasia...Wonders shall never end!!

-Hao wanao pachikwa majina ya ajabu ajabu kwa sababu za kuwa zuia wasiseme wanacho amini, ndiyo wana kuwa mwiba, leo hii utakuta hawa wanajiita Bavicha asili, wengine friends of Bavicha, Chadema asili na kadhalika na wote wanapigana madongo!! Na hali hii imejitokeza sana wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama.....

5. Bavicha imekosa "viongozi wa juu" wenye ujasiri na uthubutu wa kukisaidia chama, kukikosoa, kukisimamia na kuhakikisha maslahi ya wanachama ndani ya chama yanalindwa. Kwa nyakati kadhaa wanachama baadhi wamekuwa wakilalamikia masuala mbali mbali ndani ya chama ikiwemo suala la matumizi ya ruzuku (fedha) na masuala ya kiuongozi ikiwemo teuzi mbali mbali hasa nyakati za uchaguzi, Bavicha Taifa nani amewahi kutoka hadharani kwa ujasiri na kuhoji???????

Julius Malema dunia inamfahamu kama moja ya viongozi makini aliye kuwa kiongozi wa vijana ndani ya chama chake cha zamani cha ANC. Baada ya kuhoji mambo ya msingi na kuisimamia anacho kiamini, alifukuzwa akiwa shujaa na leo ndiye "political icon" kwa wana siasa Vijana wengi barani Afrika. Spirit ya Malema leo hii inahitajika sana Bavicha ili tusikumbatie UPUUZI hata ndani ya chama chetu wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Nafasi ya mwenyekiti wa Bavicha "imepwaya sana". Mwenyekiti wa Bavicha Taifa katika nafasi hii nakiri wazi imekuwa kubwa kuliko uwezo wake. Utaniuliza nasema imepwaya nikilinganisha na nani au ni Patrobas Katambi.
Kuna haja ya Mwenyekiti sasa kujitazama upya. Siasa za "kushangaa au kuzubaa" kwa sasa na hasa nyakati hizi tulizo nazo hazitakiwi. Naamini katika hili na kwa ukweli huu mchungu utafanyiwa kazi. Furaha yangu ni kuona Bavicha inakuwa imara kila siku.
Japo hoja zako ni nzuri, you are out of touch with reality!, pole!.

Unamzungumzia M/Kiti wa Bavicha, Petrobtas Katambi as if hujui kinachoendelea ...

Sisi wengine, sio Chadema na hatuna vyama, lakini mlipompendekeza tuu Katambi kugombea uenyekiti Bavicha, tuliwaeleza humu, huyo ni mwanasheria wa SMG, bosi wake ndie M/Kiti wa CCM mkoa wa Mwanza!, mlikuwa mnategemea nini?!.
Kwa taarifa tuu, kijana aliisharejea nyumbani kitambo baada ya kukamilisha kazi aliyotumwa.
P
 
Mkuu namzungumzia Huyu huyu ni error typing tu sio katambi tena Mara 500 ya katamb kuliko huyu..... Pia kwa hoja yako kuhus bwana katambi na kubali 200% na ushahid upo alikuja kutimiza kazi aliyotumwa...... Ubarikiwe sana kunikumbusha mkuu mungu awe nawe japo wew si kada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
W

Makamada Wanapita kwenye huu uzi wanacheki wanasema hiiiiiiiii.

Bavicha wameshasema tusiwakosoe mpaka hapo CDM itakaposhika dola!!! Sijakosea eti makamanda? Pipooooooooz! Ukawaaaaaaaaaa!
 
Japo hoja zako ni nzuri, you are out of touch with reality!, pole!.

Unamzungumzia M/Kiti wa Bavicha, Petrobtas Katambi as if hujui kinachoendelea ...

Sisi wengine, sio Chadema na hatuna vyama, lakini mlipompendekeza tuu Katambi kugombea uenyekiti Bavicha, tuliwaeleza humu, huyo ni mwanasheria wa SMG, bosi wake ndie M/Kiti wa CCM mkoa wa Mwanza!, mlikuwa mnategemea nini?!.
Kwa taarifa tuu, kijana aliisharejea nyumbani kitambo baada ya kukamilisha kazi aliyotumwa.
P
Usiwatoe tongotongo waache hadi wajutie maana wanajifanyaga wajanja na bado
 
Huu Uzi tangu umeanzishwa nimeona watu wawili tu wenye mlengo wa opposition wamechangia na angalau mmoja ambaye ni neutral. Lakini wengi japo kwa comment fupi na nyingi za kejeli wanatoka utawalani. Kwangu thread hii mbali ya maudhui yake mazuri ninayoamini yamewafikia walengwa lakini imenipa kitu cha ziada cha kufikiria. Ukiangalia michango katika Uzi huu utaona wazi "hakuna Simba Imara bila Yanga Makini". Hapa kina imhotep na kundi lake wamebaki wanaelea kwa sababu kila wanachotoa hakijibiwi na upande wa pili. Siasa ni hoja kwa hoja, siasa haiwezi kupambanishwa na utupu(vacuum) kama huu walioamua kuuweka Bavicha hapa. Hata nchi haiwezi kutoka ilipo kwa mawazo yanayofanana. Kwa mfano huu tujifunze, Katika " ukinzani" hutoka kilicho bora zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sina chama ila nadhani ni muda muafaka kwa vyama kukaa kimya na kumwachia mkuu na dola yake wafanye kazi tuone kama chati yake itarudia 96% ama itaendelea kudive! Yetu macho.
Media zote zinatoa ripoti zake tu, taasisi zote zinashangilia hata kama wapiga kura wanalia. Sasa ulitaka waseme nini.
Wengi wao wako lockup pia.
 
Back
Top Bottom