Waraka kwa wanasiasa taraji (72 LAWS)

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
453
376
Habari za saa hii wanajamvi,wataalamu wa kufikiri duniani kote,ni heshima kubwa sana kwa Tanzania kuwa na Jamii forum kuwa jukwaa kubwa Africa mashariki limekua chanzo cha taarifa na maarifa mengi, Big up to JF founders.
Leo nazungumzia kunini kadhaa miongoni mwa kanuni 72 nilizofanyia kazi kwa kina ambazo kila mwanasiasa anatakiwa ajue au kiongozi wa kampuni au yeyote anayetaka kuwa na nguvu za kutawala watu.
Hizi ni kanuni kama ilivyo kanuni ya uvutano hata ukatae uwepo wake ipo tuu you cant deny it.
Hizi ni kanuni wanazotumia wafanyiabiashara na wanasiasa maarufu na wakubwa duniani, ukijua hizi kanuni unaweza pata promotion kama wewe ni mbunge ukawa waziri,au ukateuliwa na chama chako kuwa mgombea wa uraisi, au ukapata uteuzi wowote.
1. KANUNI YA KWANZA; NEVER OUTSHINE THE MASTER
Popote unapofanya kazi hata siku moja usije ukajaribu kujionyesha kuwa wewe ni mjanja au ni mwerevu kuliko mkubwa wako wa kazi au chama,
Jitahidi ata siku moja usije ukaonekana kuwa kitisho au mpinzani wa kiongozi wako aliye juu yako.
Viongozi walioko juu wanahitaji wakuone kuwa ni mtiifu na wanaweza kukuamini hata wakukabidhi madaraka makubwa,kamwe usionyeshe makucha yako kwa kiongozi wako usije jichimbia kaburi la kisiasa.

2.DONT PUT TOO MUCH TRUST IN FRIENDS;
Usije ukafanya kosa hili kuamini marafiki zako na ukawaambia malengo yako makubwa au mafanikio yako makubwa uliyonayo tayari au plan zako maana huwezi jua mrengo wao ni upi na pia wanaweza kupata wivu,wakipata wivu ni hatari maana anakuwa adui wa kimya kimya, adui wa kimya kimya ni hatari kuliko adui aliyedhhahiri unayemjua.atukuchekea baada ya kupata wivu lakini atatafuta namna ya kukudhuru au kukudhibiti.

3.CONCEAL YOUR INTENTION S NEVER REVEAL EXACTLY WHAT YOU WANT TO DO.
-Kama Rais au mbunge au CEO mtarajiwa kamwe usidhubutu kwatu wajue malengo yako hasa kuwa unataka kuja kugombea au kuchukuwa nafasi gani hasa ikiwa muda husika haujafika maana watakudhibiti mapema, mfano utangaze sasa hivi utagombea ubunge jimbo flani wataanza kukudhibiti mapema na hautafika.

4.ALWAYS SAY LESS THAN NECESSARY.
Usiwe mtu wa maneno mengi sana, sema pale inapobidi, kwenye wingi wa maneno hapakosi maneno utakayotegwa, sema machache muhimu kutunza heshima na watu wapende kukusikia zaidi. sema maneno machache na muhimu kama huna cha kuongea kaa kimya, au kama si lazima kujibu kashfa flani kaa kimya.

5.SO MUCH DEPENDS ON REPUTATION.
Jijengee sifa njema katika jamii yako, kuwa mtu wa kusaidia jamii yako,usije ukajiingiza kwenye tabia ambazo ni kinyume na maadili ya jamii yako, maana zitakuchafua kisiasa na zitatumka kama silaha ya kukumaliza kisiasa. Ipende na kuitunza familia yako sana na jamii inayokuzunguka.

6.GET OTHERS WORK FOR YOU AND TAKE CREDIT
Hapa sasa tunaanza sheria ngumu, hakikisha unakuwa na watu wanaokusaidia kazi zako za kisiasa kama kuandaa sera na ufanya uchambuzi wa sera za uchumi na vitu vingine vizuri lakini mwisho hakikisha wewe ndio unachukua sifa zote na ionekane wewe ndio umefanya, chochote unachodhani ni kizuri kwako na huna uwezo wa kufanya tafuta wataalamu wakufanyie but mwisho take credit for that,.kama hujui wanasiasa makini wana wanasheria,wachumi na washauri wa kisiasa amabao huwasaidia kuelewa mambo na wao wanaenda ku present tuu na kujifanya kuwa wao ndio wamegundua hizo data na kufanya analysis wao.

7.Court attention at all cost.
Fnya kitu au life stle yako iwe ya standard, vaa vizuri nguo za garama nzuri, gari nzuri, saa nzuri, ishi life amabyo machoni pa watu utaonekana ni mtu wa maana. huwezi kuwa unataka ukurugenzi,ubunge au uraisi alafu unavaa nguo za mtumba, Tafuta mavazi rasmi ya garama special kwa ajlili ya kupata attention. Hpa ni papana sana, hata kwenye michango ya kijamii,kujenga vitu flani flani tafuta marafiki zako wachache wakuunge mkono ukienda kutoa uonekane ni wewe na utapata attention na huruma za wananchi.

8. MAKE OTHERS COME TO YOU,EVEN USE A BITE.
Tumia garama upate wate waje upande wako tumia chakula,pesa au misaada kupata watu upande wako. kuna malkia aliitwa Esta alifanikiwa kupata kuungwa mkono na mfalme mara baada ya kumpikia chakula. Usitarajie kupendwa na watu bure maana wewe sio pesa.

9.WIN THROUGH YOUR ACTION NOT VIA ARGUMENT
Usipende kubishana sana kwa maneno popote pale na wanasiasa wenzako au wapinzani wako, Matendo yako yawe bora na makubwa zaidi hapo utaeleweka zaidi na wapiga kura wako na wanaokuunga mkono. wakisema maneno mengi wewe fanya actions.
10. Play to peoples fantacy.
Unapokuwa na wapiga kura au wafuasi wako chunga sana kuwaambia ukweli,; Mfano upo na vijana unawaambia jiajirini serikali haina uwezo wa kuwaajri,ilo ni kosa waambie serikali itatengeneza ajira., ukiwa na wafanyakazi waambie utaongeza mshahara minono,ukiwaambia kuwa hakuna pesa,au kwa sasa tujenge uchumi kwanza baadaya miaka 50 mtaona matunda hutapata mpiga kura, Watu wanapenda kusikia ahadi nzuri na maneno mazuri,dont tell them the truth kwenye kampeni.

11.Learn to keep people dependent on you.
Mwanasiasa mahiri anajua namna ya kucheza na akili za watu mpaka inafika mahali wapiga kura wanaona hakuna mbadala wake,hapa ndio maana kuna wabunge wana zaidi ya miaka 20 kwenye majmbo yao. ni wanasiasa mahiri wana ojua kanuni za siasa na kucheza na akili za watu.

12.When asking for help, appeal to peoples self interest. Never their mercy or gratitude.
Ukiwa unataka msaada watu wakusaidie either ni kampeni au ni shughuli zako usidhubutu kuwaambia wajitolee sheria za saikolojia inasema kuwa binadamu kwa asili ni mvivu,kwa mujibu wa Mcgregory theory X, Lakini kwa theory Y ni mchapa kazi ikiwa kuna motisha, waambie kuna kitu watapata waahidi hata nafasi kubwa ukishinda au wape posho yoyote ili wakusaidie. usitarajie huruma za watu kamwe, kanuni ya asili ya akili hairuhusu.

13. Tell people what they want to hear.
Ambia watu wanachopenda kusikia, nadhani mlisikia kashfa iliyoipata facebook, kuna kampuni moja uingereza ilichukua data za watu facebook kuona nini wanapenda zaidi na nini hawapendi izo data wakatumia vibaya waka waambia wanasiasa nini raia wanapenda kusikia zaidi.

15.Pose as a friend and work as spy
Kwenye siasa usiamini mtu, kuwa kama rafiki wa kila mtu na wa rafiki zako lakini wachunguze kwa umakini wa hali ya juu kujua madhaifu, nguvu na mirengo yao.

16. Use absence to increase respect and honour
Punguza kuonekana onekana ovyo kuongeza heshima , hii hata wasanii wanaijua sana, unapoonekana onekana au kusikika kila siku ndivyo utachikwa haraka zaidi, law of supply and price.

17.DO NOT COMMIT TO ONYONE.
Usiwe na mrengo au kundi au rafiki wa kudumu wala adui,usijiambatanishe na team flani hii itakusaidia siku moja timu zote zinakuja kukuunga mkongo.

18. KNOW WHO YOU ARE DEALING WITH , DO NOT OFFEND THE WRONG PERSON.
SIasa ni sayansi na mchezo unaotumia akili sana,anaeza tumwa mtu akutukane au akuseme vibaya uchukue uanze kuropoka, kumbe katumwa na watu wako wa karibu ili uchafuke wachukue nafasi yako, uvumilivu ni muhimu mnoo na kutumia akili kubwa,

19. PLAY A SUCKER TO CATCH A SUCKER.
Kuna muda inabidi ujifanye mjinga na hujui kitu na kujichanganya ili wale waliokuwa wapinzani wako kwa siri siri wajitokeze hadharani uwajue, dont act to be smart all the time, jifanye mjinga kuwashika wajinga....
nitaendelea kanuni nyingine muhimu 72 kuzijua,
.SIASA NI SAYANSI.
 
asa mkuu mbona hujasema ulipochukulia hizi laws,unatakiwa mwisho wa andiko uainishe ulipochukulia material.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom