Uchaguzi 2020 Waraka kwa Wagombea Urais

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
WARAKA WA WAZI KWA WAGOMBEA URAIS

Na, Robert Heriel

Andiko hili ni kwa Maslahi ya nchi hii. Yeyote mwenye nafasi kubwa anaweza kulitumia katika kuinua taifa hili. Hata hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anaweza tumia waraka huu kujiimarisha. Kwani nguvu ya mtu mmoja mmoja ndani ya taifa ndio nguvu ya taifa letu.

Niliwahi kuandika humu humu kuishauri serikali, pia katika Kitabu changu cha "NADHARIA ZA TAIKON" nimeeleza jambo hili kuwa, ''huwezi kuondoa umasikini kama hujui ni wpai utaupeleka. Kama utaondoa umasikini bila kujua wapi utaupeleka utasababisha unyonyaji na dhuluma ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi. Yaani tutanyonyana wenyewe kwa wenyewe"

Leo nimeona nirudie jambo lile lile, kuwaasa na kuwashauri wagombea wote wa Urais kwa vyama vyenu, Iwe ni Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Mhe. Tundu Lisu, Mhe Benard Membe na wengineo.

Waraka huu umelenga kushauri mambo yafuatayo;
1. KUINUA UCHUMI WA NCHI YETU NA KUWA TAIFA LENYE NGUVU AFRIKA
2. KUIMARISHA FIKRA ZA UTAMBUZI WA MTU MMOJA MMOJA NDANI YA NCHI
3. KUIMARISHA UTAMADUNI

Nimetaja mambo hayo kwa kuzingatia kuwa mwanadamu anaongozwa na mambo yafuatayo;
1. Akili
2. Imani
3. Hisia
4. Matendo.

Utawala wowote lazima uzingatie mambo hayo manne yanayomungoza mwanadamu. Na ile mtu atawaliwe basi ni lazima ahakikishe anaathiri mambo hayo manne.

Kwanza aanze na Akili, kisha imani, alafu Hisia na mwisho matendo ya watu automatiki yatakuwa yametawaliwa.

AKILI, huzaa mtazamo, uvumbuzi, maarifa, ujuzi, uchambuzi, uzoefu na mambo yote yahusuyo akili.

IMANI huzaa, mila, desturi, utamaduni, miiko, na mambo yote yahusuyo imani

HISIA huzaa, hali(hali kama njaa, kiu) upendo, chuki, furaha, amani, hasira, uzuri na mambo yote yahusuyo na yenye mguso wa kihisia

MATENDO huzaa, shughuli zote za kibinadamu, kazi za mikono na miguu, kazi za mdomo, ambazo ni matokeo ya mambo matatu hapo juu yaani Akili, imani na hisia.

Serikali yoyote lazima ijikite katika mambo hayo manne ili iweze kutawala.

Wakoloni na nchi zote zilizotawala nchi zingine walitumia mambo hayo manne kuyadhibiti

Serikali lazima itambue kuwa haiwezi kuendelea kwa kujifungia ndani ya nchi. Serikali haiwezi kuendelea kwa kutumia wananchi wake pekeake.

Taifa haliwezi kuendelea ikiwa linatumikiwa na wanachi wake pekeake. hii ni Kanuni au siri namba moja ya kulifanya taifa letu liwe taifa kubwa.Taifa haliwezi kuendelea kwa kujitumikia lenyewe. Lazima lijitumikie lenyewe kisha litumikiwe na mataifa mengine iwe ni mataifa mawili au zaidi. Siri hii imetumika pia na mataifa mengine na tawala zingine ambazo nitazitaja.

Hii pia ipo kwa Mtu Binafsi. Yaani mtu hawezi kuendelea na kuwa na maisha mazuri kwa kujitumikia mwenyewe. Hawezi kuwa tajiri kwa kujitumikia yeye mwenyewe. Huwezi tumia masaa 24 kujitumikia alafu uwe tajiri, hiyo haipo. Ni lazima ujitumikie mwenyewe kisha na wengine wakutumikie. Na hapa ndipo ile siri ya utajiri.

Huwezi kutajirika bila kuajiri watu wengine wakutumikie ili uzidi kuwa tajiri.

Wagombea mnaowania nafasi za Urais, nawahakikishia kuwa hata muwe wote marais kwa wakati mmoja, mkae ikulu, mshauriane namna ya kulifanya taifa hili kuwa taifa tajiri. Mkaondoa Rushwa, Ufisadi, sijui wizi, uvivu miongoni mwa mambo mengine. Taifa hili litabaki kuwa la kawaida tuu, na usishangae mambo yakazidi kuwa magumu kupitiliza.

Niliwahi kuandika kuwa; Kama unataka kuufukuza umasikini sharti ujue unaufukuza kwenda kwa nani, wapi na utakaa kwa muda gani. Umasikini kuufukuza unahitaji usimamizi wa hali ya juu, unataka uupeleke wewe mwenyewe kama ulivyoletwa.

Umasikini haukuja kwa bahati mbaya, haukutokea tuu, kama vile utajiri jisni ulivyo. Umasikini uliletwa iwe na watu tuwajuao au tusiowajua. Umasikini uliletwa, na aliyeuleta aliukataa huko kwao.

Mimi ni moja ya watu wanaoamini katika matabaka. Naamini dunia imeumbwa ikiwa na matabaka. Siamini katika watu wato ni sawa. Ninaamini kuwa wapo walioumbwa ili wafanywe masikini na wenzao wenye akili. Ila hakuna aliyeumbwa masikini kwa asili.

Serikali lazima iandae mpango wa kuzitawala nchi zingine. Hiyo ndio siri ya mafanikio ya taifa lolote kubwa duniani. Tangu zamani za kale dunia kuumbwa.

Lazima tutafute nchi kadhaa tutakazozipelekea umasikini wetu, ujinga wetu, maradhi yetu, imani potofu zetu, lakini kama hatutazitafuta nchi hizo, mimi Taikon nasema, umasikini, ujinga na Maradhi havitaondoka nchini kwetu hata aje Malaika.

NAPENDEKEZA MAMBO YAFUATAYO;

1. Matumizi sahihi ya Migogoro nchi Jirani
Nchi yetu inazungukwa na nchi zenye migogoro ya kisiasa, Kuna Congo, Somalia, Kenya, Msumbuji n.k
Nchi yetu ilishawahi kuzisaidia baadhi ya nchi dhidi ya waasi bila ya kupata faida nono.
Kupitia migogoro kuna kupata mali kwa kuiba, kuwauzia chakula na bidhaa mbalimbali, kuajiri vijana waliokosa ajira nchini kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi waende wakatafute mali huko kwenye nchi zisizotaka amani.

Kabla ya kuingilia migogoro au vita katika nchi yoyote serikali iingie mkataba wa kisheria juu ya makubaliano kuwa baada ya vita basi wafanyabiashara wa nchi yetu watakuja kufanya biashara kwa punguzo kubwa la kodi, pia nchi yenye mgogoro itatumia bandari yetu ndani ya muda wa makubaliano kama ni miaka 20 sawa, kama ni 50 haya, basi ilimradi

Kama nchi zinazotuzunguka hazina mgogoro basi ni wajibu wa serikali kuanzisha migogoro bila kujulikana.

Migogoro ni moja ya siri ya kulifanya taifa lolote liwe kubwa. Iwe mgogoro wa kutengeneza au wao wenyewe.

Wakati wao wanafikiri kusuluhisha mgogoro ninyi mnatafakari namna ya kuzalisha zaidi.
Migogoro pendekezwa
1. Mgogoro wa kisiasa
2. Mgogoro wa kiuchumi
3. Mgogoro wa masuala ya kiafya kama magonjwa
4. Mgogoro wa teknolojia
5. Mgogoro wa kisanaa

2. DINI
Serikali ihakikishe inatumia watu wa dini wenye ushawishi kwa kuwapa sapoti kwa siri kubwa. Dini zinaweza kuwa za aina nyingi na zenye sheria tofauti tofauti.

Kanda ya kaskazini waanzishe dini kisha kwa mwaka wawe wanaenda kuhiji Mlima Kilimanjaro, waumini wa dini hiyo watozwe pesa kulingana na wanapotoka. Watu wenye akili, wanafalsafa, wanafasihi, waandishi, wanasheria wakae kuunda kanuni na taratibu zitakazoendana na mahitaji ya kidini na dunia ya sasa na ijayo

Kanda ya Ziwa nayo iunde Dini ambayo kwa Mwaka watakuwa anaenda kuhiji Ziwa Victoria. Au kivutio chochote kilichopo Kanda ya Ziwa ambacho duniani ni ngumu kukikuta.

Kanda ya Mashariki na Kanda ya kusini bila kusahau Magharibi. Zote ziundwe dini kubwa zitakazo sapotiwa na vyombo vya habari. Viongozi wa dini hizo wathibitishwe kuwa ni mashuhuri kwa akili, mikakati, ushawishi na sifa zingine zenye kuvutia watu.

Dini ni utamaduni. Kupitia dini, tutatangaza vivutio vya nchi yetu kulingana na kanda. Viongozi wa dini hizo wapewe sapoti ya kuanzisha dini hizo nchi zingine, pia wapewe miaka kumi kumi ya kufikia malengo ya kuongeza waumini katika mataifa ya nje.

Kuepuka ukabila, kila kiongozi wa dini kutoka dini ya kanda fulani ni sharti mke wake awe ameoa kutoka kanda nyingine. Mfano Kama Kiongozi wa kidini ni Muha, kutoka kanda ya magharibi Basi Mke wake awe Mzaramo, au mdendereko kutoka kanda ya mashariki.

Dini ni biashara, dini ni moja ya miradi yenye pesa. Mataifa yote makubwa yanalijua jambo hilo. Taifa lolote linalochukulia dini kama sehemu ya imani kamwe haliwezi kuendelea. Kwa nje dini ionekane ni imani kwa Mungu, lakini kwa ndani dini ionekane kama sehemu ya biashara na mradi wenye faida

3. ELIMU
Serikali ijenge Vyuo vikuu vikubwa, viwili kwa kila kanda. Viwe vikubwa vya hadhi ya kimataifa.
Kisha itoe scholarship kwa wanafunzi wa nchi za nje ili kuvutia wanafunzi wa nchi za nje na kutengeneza soko kwa nchi husika. Kwa mfano, serikali kwa nchi moja itoe Scholarship ya wanafunzi kumi. Kisha iendelee kutangaza chuo hicho kwenye nchi husika.
Mbali na kupata soko la wanafunzi kutoka nchi hizo pia ni rahisi kuweka mapandikizi kwenye nchi hizo. Nashauri uwiano wa Gender uwe 7:3 kwenye hiyo Scholarship. Wanawake 7, wanaume 3.

Mbinu hii inatumiwa zaidi, na nchi za dunia ya pili kwa sasa ambazo ni Uchina, malasyia, ufilipino, n.k Zamani mbinu hii ilitumiwa na nchi ya Dunia ya kwanza kama vile Ujerumani, uingereza, Uruso, Marekani n.k. Mbinu hii imesaidia nchi hizo kuweka vibaraka ndani ya nchi za Afrika na Asia.

Siku hizi nchi za Asia kama Uchina, Malaysia, Korea kusini zinajipatia Fedha nyingi kupitia kudahili wanafunzi wa chuo kutoka mataifa ya kigeni.

4. ULOWEZI
Serikali itumie mbinu ya Ulowezi. Itoe hati ya kusafirisha kwa vijana waliofikisha umri wa miaka 21. Baadhi waende ughaibuni kwa mfumo wa serikali iwe kwa kusoma, iwe kwa kutafuta kazi, iwe kwa mashirika ya dini ambayo tayari serikali iliyaanzisha kikanda kisiri. Wawekezaji, wasanii wakubwa, wote wakalowee huko. Kama sio hivyo basi wakazae huko kimkakati. Watu hao wakalowee nchi za watu. Watu hao sharti wale kiapo na wajulikane kama werevu.

Waende wakaoe nchi walizolowea huko. Kila mmoja aoe kwa shabaha, sio ajichukulie mwanamke bila akili.

Mbinu hii imetumiwa na Dunia ya kwanza enzi za zamani kipindi cha nyuma enzi za ukoloni. Lakini kwa sasa mbinu hii inatumiwa na Jamii ya wahindi, Waarabu, Wachina, Waturuki n.k

Hata kwenye nchi yetu tunaona mbinu hii ikifanya kazi.kwa wageni. Embu tembea majiji makubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Zanzibar, nk. Utakuta Wahindi na Waarabu waliolowea ni wengi sana. Hata makampuni makubwa na ya kati mengi wanayamiliki wao. Mbinu hii inaitwa mbinu ya Ulowezi.

Wachina nawaona nao kwa kasi wanakuja kwa mbinu hii hii.

Ulowezi ni moja ya mbinu ya kutawala jamii nyingine.

5. SANAA, FASHENI NA MITINDO
Ni muhimu kutumia sanaa kutawala nchi zingine. Endapo tutatumia sanaa kutawala nchi zingine basi tutatengeneza ajira maelfu kwa vijana wetu wa kitanzania.

Sanaa ya muziki, Sanaa ya Maigizo ya Filamu, Sanaa ya Uandishi wa Fasihi, uchongaji, ususi, Uchoraji n.k.

Serikali iandae mkakati wa kutangaza sanaa ya taifa hili kwa kufanya mashindano makubwa kila mwaka kitaifa au kimataifa. Wachaguliwe vijana wenye sifa na wenye vipaji visivyo na shaka. Serikali iubde utaratibu wa haki miliki, na kuwasaidia wasanii kwenye suala la teknolojia kuhusu MEDIA, EDITING na ANIMATION.

Taifa la Marekani kupitia Hollywood linaingiza mapato mengi sana kupitia filamu, wasanii wakubwa wa Muziki wa USA wamejipatia utajiri mkubwa kupitia sanaa ya muziki. Sio kwamba wasanii hao wanajua zaidi ya wasanii wetu hapa, bali serikali imechkulia jambo hilo kama agenda ya taifa.

Nafurahi kuona Diamond Platnum kwa hapa Afrika mashariki kajitahidi, sasa inabidi wawe kumi kama yeye.

Nigeria, na Afrika ya kusini wametumia mbinu hii kutawala nchi zingine za Afrika. Nasema hivi kwa sababu wasanii wa nchi nyingi ikiwemo Tanzania huimba kwa kufuata mitindo ya Nigeria na Afrika ya kusini.

Waraka huu utaishia hapa kwa leo, maanda nawajua watu wangu, wazee wa fupisha, andiko refu.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Anza kuishauri kwanza NEC itende haki kwa wagombea wote haya mengine yatakuja menyewe

Mimi sishauri jambo moja kila siku Mkuu.

Nilishaongea habari za NEC
Nilishaongea habari ya mauaji na utekaji
Nilishaongea habari za Lisu kushindwa kuwakemea wazungu
Nilishaongea habari za Magufuli kutumia lugha mbaya wakati wa majanga
Nilishaongea habari za Gwajima na ubaguzi
Nilishaongea habari za uhuru wa vyombo vya habari
Nilishaongea habari za vyama vya upinzani kupinga kila kitu
Nilishaongea habari za serikali kujiamulia manunuzi pasipo bunge kupitisha

Nimeongea habari nyingi Mkuu, mpaka sasa nimeongea mambo yasiyopungua 1000

Naongea kwa maslahi ya nchi Mkuu.
Ukikadhania jambo moja itaonekana unamaslahi binafsi
 
haki kwanza, bila haki sera zinaweza kutolewa nzuri sana lakini zisifanyiwe kazi.
 
Mimi sishauri jambo moja kila siku Mkuu.

Nilishaongea habari za NEC
Nilishaongea habari ya mauaji na utekaji
Nilishaongea habari za Lisu kushindwa kuwakemea wazungu
Nilishaongea habari za Magufuli kutumia lugha mbaya wakati wa majanga
Nilishaongea habari za Gwajima na ubaguzi
Nilishaongea habari za uhuru wa vyombo vya habari
Nilishaongea habari za vyama vya upinzani kupinga kila kitu
Nilishaongea habari za serikali kujiamulia manunuzi pasipo bunge kupitisha

Nimeongea habari nyingi Mkuu, mpaka sasa nimeongea mambo yasiyopungua 1000

Naongea kwa maslahi ya nchi Mkuu.
Ukikadhania jambo moja itaonekana unamaslahi binafsi
Hapo sawa mkuu
 
WARAKA WA WAZI KWA WAGOMBEA URAIS

Na, Robert Heriel

Andiko hili ni kwa Maslahi ya nchi hii. Yeyote mwenye nafasi kubwa anaweza kulitumia katika kuinua taifa hili. Hata hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anaweza tumia waraka huu kujiimarisha. Kwani nguvu ya mtu mmoja mmoja ndani ya taifa ndio nguvu ya taifa letu.

Niliwahi kuandika humu humu kuishauri serikali, pia katika Kitabu changu cha "NADHARIA ZA TAIKON" nimeeleza jambo hili kuwa, ''huwezi kuondoa umasikini kama hujui ni wpai utaupeleka. Kama utaondoa umasikini bila kujua wapi utaupeleka utasababisha unyonyaji na dhuluma ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi. Yaani tutanyonyana wenyewe kwa wenyewe"

Leo nimeona nirudie jambo lile lile, kuwaasa na kuwashauri wagombea wote wa Urais kwa vyama vyenu, Iwe ni Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Mhe. Tundu Lisu, Mhe Benard Membe na wengineo.

Waraka huu umelenga kushauri mambo yafuatayo;
1. KUINUA UCHUMI WA NCHI YETU NA KUWA TAIFA LENYE NGUVU AFRIKA
2. KUIMARISHA FIKRA ZA UTAMBUZI WA MTU MMOJA MMOJA NDANI YA NCHI
3. KUIMARISHA UTAMADUNI

Nimetaja mambo hayo kwa kuzingatia kuwa mwanadamu anaongozwa na mambo yafuatayo;
1. Akili
2. Imani
3. Hisia
4. Matendo.

Utawala wowote lazima uzingatie mambo hayo manne yanayomungoza mwanadamu. Na ile mtu atawaliwe basi ni lazima ahakikishe anaathiri mambo hayo manne.

Kwanza aanze na Akili, kisha imani, alafu Hisia na mwisho matendo ya watu automatiki yatakuwa yametawaliwa.

AKILI, huzaa mtazamo, uvumbuzi, maarifa, ujuzi, uchambuzi, uzoefu na mambo yote yahusuyo akili.

IMANI huzaa, mila, desturi, utamaduni, miiko, na mambo yote yahusuyo imani

HISIA huzaa, hali(hali kama njaa, kiu) upendo, chuki, furaha, amani, hasira, uzuri na mambo yote yahusuyo na yenye mguso wa kihisia

MATENDO huzaa, shughuli zote za kibinadamu, kazi za mikono na miguu, kazi za mdomo, ambazo ni matokeo ya mambo matatu hapo juu yaani Akili, imani na hisia.

Serikali yoyote lazima ijikite katika mambo hayo manne ili iweze kutawala.

Wakoloni na nchi zote zilizotawala nchi zingine walitumia mambo hayo manne kuyadhibiti

Serikali lazima itambue kuwa haiwezi kuendelea kwa kujifungia ndani ya nchi. Serikali haiwezi kuendelea kwa kutumia wananchi wake pekeake.

Taifa haliwezi kuendelea ikiwa linatumikiwa na wanachi wake pekeake. hii ni Kanuni au siri namba moja ya kulifanya taifa letu liwe taifa kubwa.Taifa haliwezi kuendelea kwa kujitumikia lenyewe. Lazima lijitumikie lenyewe kisha litumikiwe na mataifa mengine iwe ni mataifa mawili au zaidi. Siri hii imetumika pia na mataifa mengine na tawala zingine ambazo nitazitaja.

Hii pia ipo kwa Mtu Binafsi. Yaani mtu hawezi kuendelea na kuwa na maisha mazuri kwa kujitumikia mwenyewe. Hawezi kuwa tajiri kwa kujitumikia yeye mwenyewe. Huwezi tumia masaa 24 kujitumikia alafu uwe tajiri, hiyo haipo. Ni lazima ujitumikie mwenyewe kisha na wengine wakutumikie. Na hapa ndipo ile siri ya utajiri.

Huwezi kutajirika bila kuajiri watu wengine wakutumikie ili uzidi kuwa tajiri.

Wagombea mnaowania nafasi za Urais, nawahakikishia kuwa hata muwe wote marais kwa wakati mmoja, mkae ikulu, mshauriane namna ya kulifanya taifa hili kuwa taifa tajiri. Mkaondoa Rushwa, Ufisadi, sijui wizi, uvivu miongoni mwa mambo mengine. Taifa hili litabaki kuwa la kawaida tuu, na usishangae mambo yakazidi kuwa magumu kupitiliza.

Niliwahi kuandika kuwa; Kama unataka kuufukuza umasikini sharti ujue unaufukuza kwenda kwa nani, wapi na utakaa kwa muda gani. Umasikini kuufukuza unahitaji usimamizi wa hali ya juu, unataka uupeleke wewe mwenyewe kama ulivyoletwa.

Umasikini haukuja kwa bahati mbaya, haukutokea tuu, kama vile utajiri jisni ulivyo. Umasikini uliletwa iwe na watu tuwajuao au tusiowajua. Umasikini uliletwa, na aliyeuleta aliukataa huko kwao.

Mimi ni moja ya watu wanaoamini katika matabaka. Naamini dunia imeumbwa ikiwa na matabaka. Siamini katika watu wato ni sawa. Ninaamini kuwa wapo walioumbwa ili wafanywe masikini na wenzao wenye akili. Ila hakuna aliyeumbwa masikini kwa asili.

Serikali lazima iandae mpango wa kuzitawala nchi zingine. Hiyo ndio siri ya mafanikio ya taifa lolote kubwa duniani. Tangu zamani za kale dunia kuumbwa.

Lazima tutafute nchi kadhaa tutakazozipelekea umasikini wetu, ujinga wetu, maradhi yetu, imani potofu zetu, lakini kama hatutazitafuta nchi hizo, mimi Taikon nasema, umasikini, ujinga na Maradhi havitaondoka nchini kwetu hata aje Malaika.

NAPENDEKEZA MAMBO YAFUATAYO;

1. Matumizi sahihi ya Migogoro nchi Jirani
Nchi yetu inazungukwa na nchi zenye migogoro ya kisiasa, Kuna Congo, Somalia, Kenya, Msumbuji n.k
Nchi yetu ilishawahi kuzisaidia baadhi ya nchi dhidi ya waasi bila ya kupata faida nono.
Kupitia migogoro kuna kupata mali kwa kuiba, kuwauzia chakula na bidhaa mbalimbali, kuajiri vijana waliokosa ajira nchini kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi waende wakatafute mali huko kwenye nchi zisizotaka amani.

Kabla ya kuingilia migogoro au vita katika nchi yoyote serikali iingie mkataba wa kisheria juu ya makubaliano kuwa baada ya vita basi wafanyabiashara wa nchi yetu watakuja kufanya biashara kwa punguzo kubwa la kodi, pia nchi yenye mgogoro itatumia bandari yetu ndani ya muda wa makubaliano kama ni miaka 20 sawa, kama ni 50 haya, basi ilimradi

Kama nchi zinazotuzunguka hazina mgogoro basi ni wajibu wa serikali kuanzisha migogoro bila kujulikana.

Migogoro ni moja ya siri ya kulifanya taifa lolote liwe kubwa. Iwe mgogoro wa kutengeneza au wao wenyewe.

Wakati wao wanafikiri kusuluhisha mgogoro ninyi mnatafakari namna ya kuzalisha zaidi.
Migogoro pendekezwa
1. Mgogoro wa kisiasa
2. Mgogoro wa kiuchumi
3. Mgogoro wa masuala ya kiafya kama magonjwa
4. Mgogoro wa teknolojia
5. Mgogoro wa kisanaa

2. DINI
Serikali ihakikishe inatumia watu wa dini wenye ushawishi kwa kuwapa sapoti kwa siri kubwa. Dini zinaweza kuwa za aina nyingi na zenye sheria tofauti tofauti.

Kanda ya kaskazini waanzishe dini kisha kwa mwaka wawe wanaenda kuhiji Mlima Kilimanjaro, waumini wa dini hiyo watozwe pesa kulingana na wanapotoka. Watu wenye akili, wanafalsafa, wanafasihi, waandishi, wanasheria wakae kuunda kanuni na taratibu zitakazoendana na mahitaji ya kidini na dunia ya sasa na ijayo

Kanda ya Ziwa nayo iunde Dini ambayo kwa Mwaka watakuwa anaenda kuhiji Ziwa Victoria. Au kivutio chochote kilichopo Kanda ya Ziwa ambacho duniani ni ngumu kukikuta.

Kanda ya Mashariki na Kanda ya kusini bila kusahau Magharibi. Zote ziundwe dini kubwa zitakazo sapotiwa na vyombo vya habari. Viongozi wa dini hizo wathibitishwe kuwa ni mashuhuri kwa akili, mikakati, ushawishi na sifa zingine zenye kuvutia watu.

Dini ni utamaduni. Kupitia dini, tutatangaza vivutio vya nchi yetu kulingana na kanda. Viongozi wa dini hizo wapewe sapoti ya kuanzisha dini hizo nchi zingine, pia wapewe miaka kumi kumi ya kufikia malengo ya kuongeza waumini katika mataifa ya nje.

Kuepuka ukabila, kila kiongozi wa dini kutoka dini ya kanda fulani ni sharti mke wake awe ameoa kutoka kanda nyingine. Mfano Kama Kiongozi wa kidini ni Muha, kutoka kanda ya magharibi Basi Mke wake awe Mzaramo, au mdendereko kutoka kanda ya mashariki.

Dini ni biashara, dini ni moja ya miradi yenye pesa. Mataifa yote makubwa yanalijua jambo hilo. Taifa lolote linalochukulia dini kama sehemu ya imani kamwe haliwezi kuendelea. Kwa nje dini ionekane ni imani kwa Mungu, lakini kwa ndani dini ionekane kama sehemu ya biashara na mradi wenye faida

3. ELIMU
Serikali ijenge Vyuo vikuu vikubwa, viwili kwa kila kanda. Viwe vikubwa vya hadhi ya kimataifa.
Kisha itoe scholarship kwa wanafunzi wa nchi za nje ili kuvutia wanafunzi wa nchi za nje na kutengeneza soko kwa nchi husika. Kwa mfano, serikali kwa nchi moja itoe Scholarship ya wanafunzi kumi. Kisha iendelee kutangaza chuo hicho kwenye nchi husika.
Mbali na kupata soko la wanafunzi kutoka nchi hizo pia ni rahisi kuweka mapandikizi kwenye nchi hizo. Nashauri uwiano wa Gender uwe 7:3 kwenye hiyo Scholarship. Wanawake 7, wanaume 3.

Mbinu hii inatumiwa zaidi, na nchi za dunia ya pili kwa sasa ambazo ni Uchina, malasyia, ufilipino, n.k Zamani mbinu hii ilitumiwa na nchi ya Dunia ya kwanza kama vile Ujerumani, uingereza, Uruso, Marekani n.k. Mbinu hii imesaidia nchi hizo kuweka vibaraka ndani ya nchi za Afrika na Asia.

Siku hizi nchi za Asia kama Uchina, Malaysia, Korea kusini zinajipatia Fedha nyingi kupitia kudahili wanafunzi wa chuo kutoka mataifa ya kigeni.

4. ULOWEZI
Serikali itumie mbinu ya Ulowezi. Itoe hati ya kusafirisha kwa vijana waliofikisha umri wa miaka 21. Baadhi waende ughaibuni kwa mfumo wa serikali iwe kwa kusoma, iwe kwa kutafuta kazi, iwe kwa mashirika ya dini ambayo tayari serikali iliyaanzisha kikanda kisiri. Wawekezaji, wasanii wakubwa, wote wakalowee huko. Kama sio hivyo basi wakazae huko kimkakati. Watu hao wakalowee nchi za watu. Watu hao sharti wale kiapo na wajulikane kama werevu.

Waende wakaoe nchi walizolowea huko. Kila mmoja aoe kwa shabaha, sio ajichukulie mwanamke bila akili.

Mbinu hii imetumiwa na Dunia ya kwanza enzi za zamani kipindi cha nyuma enzi za ukoloni. Lakini kwa sasa mbinu hii inatumiwa na Jamii ya wahindi, Waarabu, Wachina, Waturuki n.k

Hata kwenye nchi yetu tunaona mbinu hii ikifanya kazi.kwa wageni. Embu tembea majiji makubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Zanzibar, nk. Utakuta Wahindi na Waarabu waliolowea ni wengi sana. Hata makampuni makubwa na ya kati mengi wanayamiliki wao. Mbinu hii inaitwa mbinu ya Ulowezi.

Wachina nawaona nao kwa kasi wanakuja kwa mbinu hii hii.

Ulowezi ni moja ya mbinu ya kutawala jamii nyingine.

5. SANAA, FASHENI NA MITINDO
Ni muhimu kutumia sanaa kutawala nchi zingine. Endapo tutatumia sanaa kutawala nchi zingine basi tutatengeneza ajira maelfu kwa vijana wetu wa kitanzania.

Sanaa ya muziki, Sanaa ya Maigizo ya Filamu, Sanaa ya Uandishi wa Fasihi, uchongaji, ususi, Uchoraji n.k.

Serikali iandae mkakati wa kutangaza sanaa ya taifa hili kwa kufanya mashindano makubwa kila mwaka kitaifa au kimataifa. Wachaguliwe vijana wenye sifa na wenye vipaji visivyo na shaka. Serikali iubde utaratibu wa haki miliki, na kuwasaidia wasanii kwenye suala la teknolojia kuhusu MEDIA, EDITING na ANIMATION.

Taifa la Marekani kupitia Hollywood linaingiza mapato mengi sana kupitia filamu, wasanii wakubwa wa Muziki wa USA wamejipatia utajiri mkubwa kupitia sanaa ya muziki. Sio kwamba wasanii hao wanajua zaidi ya wasanii wetu hapa, bali serikali imechkulia jambo hilo kama agenda ya taifa.

Nafurahi kuona Diamond Platnum kwa hapa Afrika mashariki kajitahidi, sasa inabidi wawe kumi kama yeye.

Nigeria, na Afrika ya kusini wametumia mbinu hii kutawala nchi zingine za Afrika. Nasema hivi kwa sababu wasanii wa nchi nyingi ikiwemo Tanzania huimba kwa kufuata mitindo ya Nigeria na Afrika ya kusini.

Waraka huu utaishia hapa kwa leo, maanda nawajua watu wangu, wazee wa fupisha, andiko refu.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Umepotoka
 
Back
Top Bottom