Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,070
Nakushukuru sana,
Kwanza inaelekea mwenzetu hujui kazi ya serikali. Sikutegemea kusikia maneno kama hayo kutoka kwako.
Kwahiyo inamaanisha kuanzia sasa hivi waTanzania tuanze kujihudumia wenyewe sio??? Mimi nakupa option mbili
Ya kwanza, naomba mwambie Raisi na serikali yake waache kukusanya kodi zetu. Ili tujikusanyie pesa sisi wananchi wenyewe. Tujijengee visima na kuboresha huduma zetu. nina hakika hivyo visima tutajenge bila kigugumizi.
Kwasababu tuna shida, nina uhakika
tukijichangisha tunaweza fanya jambo la maana. Kuliko kuichangia serikali. Ili wao wasafiri na kutalii kila kukicha.
Option ya pili mwaambie waache kusimamia rasili mali zetu. Kila mtu atumie ardhi yake kwa manufaa yake mwenyewe. Wazungu watolewe kule Barick. Na wakurya warudishiwa ardhi yao.
Kazi ya serikali ni nini? hebu tuambie maana nahisi we mwenzangu ndio hata maana ya serikali inakusumbua.
Unataka kunambia rais Kennedy alivyowaambia wananchi wake kwamba wafikirie wataifanyia nini marekani alikuwa hajui anachokisema?
Matatizo ya nchi hayaletwi na viongozi ni watu kama wewe wanaokaa lawama tu kila kukicha.