Waraka kwa rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by collezione, Feb 28, 2012.

 1. c

  collezione JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Niseme tu machache, ambayo yanahusiana na nchi yetu Tanzania. Awali ya yote Mimi mtanzania ninaeishi ughaibuni. Naandika hii page ikiwa ni ujumbe mzito kwa raisi wetu. Pia nataka waTZ wenzangu muusome hapa. Madhumuni makubwa, kuikomboa nchi yetu.

  Raisi ni kichwa cha waTanzania mil40 na ushehe. Waliopo Tanzania na ughaibuni. Ikiwa mimi mmoja wao. Leo hii najitosa kuzingumzia sector nne. Mosi MIUNDO MBINU, mbili ELIMU, tatu USALAMA, nne UMEME na mwisho KATIBA mpya. Nitaelezea kwa maneno machache nisikuchoshe. Ingali maneno haya yanabeba ujumbe mzito.

  Kabla sijaongelea hizo sector 4. Nianze na utangulizi.

  Ni uwazi usiofichika, nchi yetu inakabiliwa na matatizo mengi. Maradhi, ujinga(poor education), ajira, umeme, maji, rushwa, ajali barabarani(hili linashika kasi sasa) n.k. Sitakosea nikisema Tanzania kwa sasa iko ICU. Kila kukicha umaskini unaongeza. Watu wamekata tamaa na hali inazidi kuwa ngumu.
  Swali linakuja.... Je, wewe kama kichwa na muhimili wa nchi yetu unayaona haya?

  Una mikakati gani kuyapunguza atleast matatizo machache niliyotaja hapo juu. Ningefurahi kusikia 2015 utatuambia elimu TZ kwa sasa ni asilimia mia. Au umeme kwa sasa ni 100% hata vijijini wanapata umeme bila shida.

  Mimi naamini uongozi wako ukipunguza SIASA(politics) na RUSHWA haya yanawezekana. Siasa(politics) Tanzania imeshamili kila mahali. Siasa imefanya rushwa na ufisadi kuota mizizi.

  Kwenye sector za madini, utalii kote kumejaa siasa. Hii inafanya Tanzania tuzidi kuibiwa. Madini na utalii vingeweza kuifanya Tanzania iwe ya neema nyingi. Rushwa na ufisadi unafanya tusiambulie chochote sisi wananchi wa chini.

  Siasa ndio inafanya wabunge walilie kuongezewa posho, wakati madaktari wakifanyiwa mzaha.

  Mimi sio muumini wa siasa. Na waTanzania walio wengi hawaamini siasa. Wanachotaka, ni kuona rasili-mali zao zinatumika kulete maendeleo..
  Kuna siku uvumilivu utatoweka kuona hizo rasili-mali zinanufaisha watu wachache...

  Tanzania inahitaji only strong leadership, ili ku-progress. Kama Rasili-mali tunazo. Mwaka mmoja, unatosha kubadili taswira ya nchi yetu. kama kweli kiongozi wetu una nia.

  Kama nilivyoeleza awali. Matatizo yapo mengi. Si rahisi kumaliza yote kwa pamoja. Vile vile si busara kushindwa kutatua hata tatizo moja, kwa kipindi cha uongozi wako..... Kila nikirudi Tanzania sioni any changes. Cha zaidi naona matatizo yanazidi. Foleni zinazidi, umeme wa shida, n.k.

  Hapa naamanisha nini??
  Wewe, kama kichwa na kiongozi, you should point "matatizo". Yaweke kwenye preference yako. (Watu waliosoma management hapa watakuwa wamenielewa) Anza na tatizo moja moja. Naamimi mpaka muda wako umeisha, atleast mawili matatu utakuwa umeyakabili..... Angalizo, hii itawezekana kama kweli una nia..

  Kwa hali ya sasa inavyooneka, "Raisi UMEkATA TAMAA." Unasubiri 2015 umkabidhi kijiti mwingine.

  Mimi naomba uachane na "kilimo kwanza." Weka nguvu kwenye sector ya elimu, miundo mbinu, security(usalama) na umeme. . Ifikapo 2015 Uwe umepunguza matatizo ya hizo sector hata kwa 50%. Hizi sector zikisimamiwa vizuri, zitainua ajira, kilimo, utalii, biashara, uwekezaji, sector ya afya, kujiajiri, michezo, uvuvi n.k .

  Waziri mkuu mstaafu wa Malaysia ameshawahi sema. "Kiongozi shupavu na jasiri, ni yule anatakae thubutu kubadilisha nchi kutoka kutegemea kilimo mpaka viwanda". Miaka 50 ya uhuru Tanzania bado tunaongelea kilimo kwanza. This is SHAME..... Tulianza na kina Malaysia, China, Thailand, Singapore, India. Hawa wako mbali sasa, sisi bado tumebakia kwenye kilimo.

  Cha kushangaza Wewe kama kiongozi wetu mpaka leo hii unaongelea "kilimo kwanza". Huu ni uvivu wa kufikiria.
  (Watanzania wenye uelewa nilitegemea wakupigie kelele swala hili)


  Ukiboresha ELimu, miundo mbinu, SECURITY, na UMEME. Hamna haja ya kusafiri kila siku kuwapigia magoti INVESTORS. Investors Wataitafuta TZ wenyewe. Hakuna mwekezaji atayekubali kuja nchi ambayo ipo gizani(umeme wa mgao). Au nchi ambayo usalama ni mdogo(security), au nchi ambayo gharama za usafirishaji ni za juu, (kutokana na miundo mbinu mibovu). Otherwise tutasikia wamekazaji uchwara, kama hawa RICHMOND na KAGODA.


  1). Nitaanza na ELIMU.

  Elimu ndo future ya Taifa lolote. Bila elimu, taifa halina future... In Tanzania, less than 30% ya waTZ ndio educated. Sasa hapo tujiulize. Kuna any bright future kwa Tanzania ya sasa na ya kesho. In Kenya 72% of population are educated. Nahisi hapo umeona big difference.
  I thought, Wewe kama baba uliye makini ungekwepa hili swala la East Africa community. Ungeomba hudhuru lisogezwa mbele, maana humo watoto wako watanyanyasika.

  Tanzania tunaweka siasa na ufisadi hata kwenye mambo muhimu kama Elimu. Nasikitika kusikia wanafunzi wa vyuoni kupigwa mabomu mara kwa mara. Kwanini usiondoe siasa na ubabe tuwatimizie madai yao. Hao ndio wataalamu wa kesho.... Swali, Je Watapata wapi muda wa kusoma na migomo isiyokwisha?? Kwanini usitatue matatizo yao ili migomo itokomee...

  Students should work hard to develop career zao na sio migomo ya kila siku. Kuondoa migomo itasaidia kuondoa siasa ma-vyuoni. Kupiga mabomu wanafunzi unapandikiza chuki mioyoni mwao.

  Kuna gap kubwa sana kati ya shule za kata na private. Please work hard to eradicate this. I am sure, ukiamua unaweza.

  Tuboreshe shule zetu, uli kupunguza wanafunzi kusoma nje ya nchi. Nchi inapoteza fedha nyingi kutokana na wazazi kulipa school fees za watoto nje ya nchi.


  2) MIUNDO MBINU

  Miundo mbinu ndio uti wa mgongo wa nchi yoyote hapa duniani. miundo mbinu ya nchi yetu ni mibovu. Cost of living ya maisha ya waTanzania yanapanda kila leo. Hii inachangiwa sana na gharama kubwa za usafirishaji. "Transportation costs are very high in Tanzania."

  Mfanyabiashara yoyote Tanzania lazima auze bidhaa zake kwa bei ya juu, ili ku-cover high transport cost zilizotumika.
  Hii inawafanya wananchi wa kawaida kuzidi kuumia.


  Foleni za mijini, ajali za barabarani, mafuriko yaliyotokea December mwaka jana. Haya yote ni matokeo ya miundo mbinu mibovu. It seems, hakuna kiongozi anayefikira future ya Tanzania kwa kizazi cha kesho.

  kilimo kwanza ulichohaidi hakina mwelekeo. Ikiwa mabarabara ya kwenda vijijini ni mabovu. Kila mara tunasikia wakulima wakilalamika mazao ku-ozea shambani. Huu ni ubabaishaji.

  Nchi yoyote, inayoendelea haina budi kuwekeza katika miundo mbinu. China na india walianza kuwekeza kwenye barabara na reli. Ndio maana uchumi wao unakuwa kila siku. Nimebahatika kuishi india pamoja na China. Hawa watu wana barabara za lami mpaka vichochoroni. Sasa sijui kwanini huwa UNAWADANGANYA waTZ kuwa nchi yetu kubwa sana, haiwezekani kujenga barabara za lami kila kona. China na india ni nchi kubwa sana, kuliko Tanzania yetu. Wao wamewezaje??.

  Mapato yanayopatikana kwenye madini na utalii yanatosha kurekebisha miundo mbinu. Ila kwa sababu ya siasa(politics) na ufisadi kushamiri hakuna kinachopatikana. Ni AIBU kuona shirika la reli na ndege limekufa mikononi mwako. Hii nia AIBU kubwa. Kwa style hii, Tanzania has no future. Kwasababu kila kitu kitakuwa kimekufa.

  Viongozi wetu mnafurahia sana kwenda majuu. Nina uhakika, because of infrastructure services nzuri. Ndio maana mnaenda ulaya kila siku. Kwanini msifanye Tanzania yetu kuwa ulaya?? kwa kuweka super infrastructures. I am sure mkiamua mnaweza.

  To be continue.... PART 2
   
 2. c

  collezione JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nitamalizia KATIBA, umeme na usalama(security) kwenye waraka wa pili. Asante
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,811
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mkuu, umenenena. Lakini kwa kiongozi huyu tuliyenaye....mmmh

  T. Lissu aliwahi sema "Kikwete hajawahi kuchukua maamuzi magumu. Kikwete"

  Twaweza subiri muujiza toka kwake.
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ahsante mkuu
   
 5. m

  mzambia JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Lakini labda anasubiri kitu ndo achukue maamuzi magumu
   
 6. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,029
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  njo uandikie huku bongo, ujumbe utamfikia mapema zaidi ....
   
 7. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,347
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Tatizo raisi Kikwete siyo yeye anayeongoza nchi. Kuna kundi la watu ndio wanaoongoza. Mradi wa kilimo Kwanza Serikali ilikurupuka pasipo kufikiri na ni kwa manufaa ya wachache. Serikali inatenga pesa nyingi kwa ajili ya kuendeleza Kilimo kupitia Kilimo Kwanza lakini wanaonufaika ni wachache ambao ni matajiri wanachukua peas kwa matumizi nje ya kilimo. Inawaacha Wakulima hawana mtaji wa kilimo. Kilimo Kwanza ni propaganda ya kwenye makaratasi lakini utekelezaji haupo kwani Vijijini hawajui kitu na wala hawanufaiki nao.

  Hivyo mawazo yako mazuri lakini hayawezi kufanyiwa kazi katika uongozi uliopo madarakani sasa. Hilo sahau kabisa labda lete mawazo hayo baada ya 2015.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 8. m

  msnajo JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,274
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Ni ushauri mzuri ila hauna maana kwa JK. Yote hayo ameshauriwa ila kaweka pamba masikion. Pia yeye hana kauli kwa utawala wake, wapo ambao wanam-remote! Hili kundi linalomwongoza halina maslahi na Tanzania, ila maslahi binafsi! Kwa hiyo kwa wao kumshauri mambo ya maendeleo ni ngumu sana coz wao self interest ndo inafanya kazi..

  The whole system is corrupt, and so the solution is to have free and fair election. In this case, Constitution amendment is very crutial for the sake of our Nation.
   
 9. c

  collezione JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Anasubiri kitu gani??
  Hapo hamna cha kusubiri.... mpaka sasa nchi iko ICU... Labda niseme jamaa amekata tamaa, anasubiri muda wake upite.

  "He has to be a leader and not a ruler."
  Kama alikubali kuwa raisi, kwanini nchi imshinde???
   
 10. c

  collezione JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mkuu ndo maana nime-andika hapa ili tusaidiane.

  Hata akiwa pamba maskioni nyie pazeni sauti. Nyie mlio huko tunawategemea sana kufikisha ujumbe kila kona ya Tanzania.
   
 11. c

  collezione JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Haha, mkuu nashukuru. Inabidi tusaidiane kama hivi. Tusilale na kuacha watawala hawatimizi wajibu wao. Tuwawajibishe, ikiwezekana. Hii ni kwa manufaa ya watoto wetu
   
 12. c

  collezione JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  mkuu tusisubiri 2015 hali itakuwa mbaya zaidi.

  Hizi ajali za barabarani tunazosikia kila siku na migomo ya madaktari tutafika kweli huo mwaka 2015?? Tuwatendee haki taifa la kesho.
   
 13. New2JF

  New2JF Senior Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone....
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kama maendeleo ya nchi yako yanakugusa sana si ungeenda huko Tandahimba ukawachimbie jambo kisima kimoja kirefu?? umefanya nini kwa nchi yako?

  Au kila mtanzania akae kwenye computer yake aandike waraka kwa rais? wabongo bana
   
 15. m

  msnajo JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,274
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Wamehamia makanisani kununua waumini na mapadre! Bila kuing'oa CCM hakuna kitakachofanyika! Jiulize pale ikulu kuna nini? Nadhani wananchi ndo jukumu lao kuamua waongozwe na nani na kwa misingi ipi. Haiwezekani miaka 50 ya uhuru na mambo yanazidi kuwa mabaya siku hadi siku. Nchi nyingine wameweza kujiwekea mipango madhubuti kuinua uchumi wao na hali ya wananchi wao, fortunately wameweza tena kwa kiasi kikubwa. Eg Rwanda, Botswana etc. Angola wao majuzi tu wametoka kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, but they are doing well! What about us and why not us? Kuna watu wanadai eti hizo Nchi zina idadi ndogo ya watu, lakini cc mbona hata sekta moja isiwe bora kwa viwango vinavyoridhisha? Kama ulivyoshauri, maendeleo hapa Tz yanawezekana tena makubwa na wenzetu wasituone tukiomba misaada yao tena. Tuna kila kitu ila tatizo ni "mind set" za viongozi wetu zipo usingizini! Rushwa ndo kila kitu sasa. Kama hupendi rushwa unaonekana hufai kwenye jamii, hakuna haki. Kuanzia ngazi ya chini hadi huko juu serikalini, wala hakuna utawala wa sheria!. Sheria zinawaadhibu wanyonge na sio viongozi na matajiri. Ukweli ni kwamba "haki huinua Taifa, lakini dhuluma inaangamiza Taifa". Sasa katika mazingira haya maendeleo yatatoka wapi ikiwa Taifa lina angamia? Wananchi wafunguke akili zao (they should open up their mind).
  Unafiki na ujeuri hauna nafasi tena. Watu wanaogopa kupaza sauti zao sababu unahatarisha maisha yako na familia yako!. Mtazame Mwakyembe, yanayomkumba ni kwa sababu alijaribu kuzungumza ukweli. Nasema alijaribu manake hakuzungumza "absolute truth", alitoa tu clues. Matokeo yake inasemekana amepewa sumu! Kauchuguzi kadogo tu hapo Arumeru, rushwa imetembea hakuna mfano!! Ukitaka kupunguza rushwa ni lazima CCM ife kwanza manake ndio uhai wake.
   
 16. c

  collezione JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nakushukuru sana,
  Kwanza inaelekea mwenzetu hujui kazi ya serikali. Sikutegemea kusikia maneno kama hayo kutoka kwako.

  Kwahiyo inamaanisha kuanzia sasa hivi waTanzania tuanze kujihudumia wenyewe sio??? Mimi nakupa option mbili

  Ya kwanza, naomba mwambie Raisi na serikali yake waache kukusanya kodi zetu. Ili tujikusanyie pesa sisi wananchi wenyewe. Tujijengee visima na kuboresha huduma zetu. nina hakika hivyo visima tutajenge bila kigugumizi.

  Kwasababu tuna shida, nina uhakika
  tukijichangisha tunaweza fanya jambo la maana. Kuliko kuichangia serikali. Ili wao wasafiri na kutalii kila kukicha.

  Option ya pili mwaambie waache kusimamia rasili mali zetu. Kila mtu atumie ardhi yake kwa manufaa yake mwenyewe. Wazungu watolewe kule Barick. Na wakurya warudishiwa ardhi yao.
   
 17. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,198
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160

  Well said kaka

  1. Kazi kuvaa sneakers tu huko na fulana...wakija huku miwani mikubwa kama panzi na kulalama mara foleni mara vumbi n ol that....ilhali wanajenga uchumi wa watu huko

  2. Kama kweli wana uzalendo waje hapa tujue la kufanya on our mother land

  3. Kisima watachimba na nini watu wa aina hii kaka......hata kuweka madawati darasa moja tu kijijini kwake hawezi.........ni bora huyu aliyekata tamaa hapa tukifa naye kuliko nyie mlio huko kazi kubwabwaja tu.....rudini huku tukatwe kodi wenzetu wasio na uwezo wanunuliwe japo dawa mahospitalini
   
 18. c

  collezione JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nakushukuru sana ndugu

  Mimi naomba hii sauti tuipaze kila kona. Tusikubali taifa liangamie kabisa. Watoto wetu watatulaumu sana.

  Kuhusu uchache wa watu, hiyo sio point. India wako wangapi? China je? How about Thailand? Brazili?

  Huo ni uvivu wa kufikiria
   
 19. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,347
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Masikio kaweka pamba. Hatoweza kusikia.
   
 20. c

  collezione JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hata Marekani raisi anabeba lawama zote. Kwa sababu zifuatazo

  1) Anapewa mshahara mkubwa, na mahitaji yote ya muhimu ili kuongoza wananchi. Na sio swala la kila mwananchi kijichimbia kisima au kupeleka dawa hospitalini.

  Kama ni hivyo, wananchi wasitoe kodi(tax) yoyote. Na kila mtu ajitegemee kutokana na pesa yake.

  Ndugu zangu, hapa sisi sio tunababwaja. And it seems huelewi kazi ya serikali wewe. Serikali yoyote haitegemei mtu mmoja kujenga kisama wala kununua dawa. That why wanakusanya kodi. Kama kutumia kodi zetu vizuri hawawezi, tunaomba waache madaraka.

  Na kule shinyanga na mwanza. Waache wasukuma wachimbe madini yao wanavyoweza.
   
Loading...