Kwanza kabisa nichukue fursa hii kukupongeza kwa kazi ngumu ambazo umekuwa ukizifanya, naelewa baada ya kukalia hicho kiti umekutana na mambo mengi sana na ya hovyo lakini hiyo ndo nchi yetu ilipofikia, ni Watanzania wazalendo wanaoweza kuikwamua kutoka hapo iliponasa, lakini kikubwa ninachopenda kukushauri, chondechode, wakati unatafuta wale wote waliohusika na ufedhuri huu naomba usiangalie sura, usibague mtu na dini au rika yake, tunaomba sheria ifate mkondo wake ili ukwepe lile dimbwi la double standard.
Baada ya kusema hayo machache naomba sasa nijikite kwenye mada ambayo imenisukuma nikuandikie waraka huu kwa uchungu mkubwa sana juu ya kile kinachoondelea kwa sasa katika nchi yetu juu ya wnafunzi wote tangu 1994 waliosomeshwa na serikali kwa kutumia bodi ya mikopo.
Mimi ni mmoja wa wanafunzi ambao wamesomeshwa na serikali kupitia bodi ya mikopo ila sikuwa kulipa hata shilingi kutokana na sababu nyingi sana ambazo zinatokana na utaratibu mbovu sana wa serikali/bodi ya mikopo.
Nimeskia vitisho vingi vilivyokosa weredi katika kudai pesa/mkopo kutoka kwa wadaiwa, nchi isiendeshwe kwa vitisho kiasi hicho, naomba mamlaka zinazohusika na zoezi hili liende kwa kufata sheria kama zilivyosaniwa na wanafunzi wenyewe kwenye form za kuombea mikopo. Nashangaa sana kusikia bodi inavyokurupuka na kutaka kufanya mambo kwa papara hali wanajua kwamba uzembe wao ndo umesababisha upuuzi kama huu utokee.
Kila mwanafunzi aliyenufaika na mkopo alijaza form ya kuomba mkopo na hiyo form ina details nyingi ikiwemo REPAYMENT PERIOD, Nashangaa sana kuskia matamko yanayotolewa na wafanyakazi wa HELSB, najiuliza sana na nashindwa kuelewa haya matamko yanatoka wapi? kwa sheria au mkataba upi ambao unawasukuma kulazimisha kufupisha muda wa malipo kwa kadiri wanvyotaka wao, huu ni ukiukwaji mkubwa sana wa sheria, mjue pia kuwa tunajua haki na sheria ziko wazi, mheshimu makubaliano na mtumie weredi kufanikisha hili.
Naomba pia niwaeleze kwamba, asilimia kubwa ya wadaiwa wapo tayari kulipa kwa makato yanayostahili kwa mujibu wa mikataba yao walioijaza kwenye form za kuombea mikiopo, mimi nilijaza form yangu 2005/06 na inasema kabisa muda wa kulipa ni miaka mingapi.
Msukumo wa kulipa unakuja kulingana na hali halisi iliyopo katika nchi kwani asilimia kubwa ya wananchi wanaona mambo yanaenda na binafsi napenda kuwa sehemu ya maendeleo katika taifa langu lakini lazima mtambue kuwa, watu wengi hawataki kulipa pesa/kodi pia sababu walikuwa hawaoni pesa yao inafanya nini kama sio kunufaisha mafisadi na mambo mengine ya hovyo, thanks God mambo yanaenda na tunaamini kila kitu kitakaa vizuri.
Bodi ya mikopo ilishindwa kuweka mikakati mizuri ya wanufaika kulipa pesa pindi wanapoanza kazi, ni muda muafaka sasa kwa bodi kuja na mkakati mzuri ambao utaondoa usumbufu na utakuwa rafiki kwa wanafaika wote ili bodi iendelee kutoa huduma kwa watu wengine/wadogo zetu, mfumo au utaratibu uliopo ni wa hovyo sana, tunahitaji mfumo ambao utadumu na utakuwa na ufanisi. Mzigo kubwa mnauweka kwa vijana walioajiriwa tu sijui ambao wamejiajiri mnafanyaje? mnao tracking mechanism nzuri ya kuwatafuta? ni muda wa kutafakari sana juu ya hili.
Mwisho nipende kumpa chanagamoto mheshimiwa rais wetu KIPENZI, Juzi tuliskia alivyowapa wadaiwa sugu na wakwepa kodi muda wa kulipa kodi walizokwepa kwa muda mrefu, sikuskia interest juu ya pesa walizolalia muda mwingi na kuumiza taifa, ila kwa upande wa pili kwetu sisi naskia wanafunzi kuna interest inayotakiwa kulipa kwa kushindwa kulipa kwa wakati mikopo husikia, lakini naomba nikueleze mheshimiwa Rais, hawa wadaiwa ndo wamekuwa wakiendesha nchi kwa kodi zao za PAYE, wafanya biashara wakubwa tumeona ambavyo wamefanya ndani ya taifa hili, kumbuka mzigo wa P.A.Y.E ulivyo mkubwa lakini wananchi hawa wamelipa na kusababisha nchi iende hadi hapa ilipofika, inaskitisha sana serikali inaposhindwa kutambua mchango wa hawa watu ingawa hauonekani directly lakini ni mkubwa sana katika uhalisia.
Nawaachia mlitazame hili, pitieni mikataba ya wanfunzi waliojaza, jiridhishe ni miaka mingapi walikubalaiana kulipa mikopo hiyo na msisahahu kuwa mzigo mliotutwisha ili kufidia wakwepa kodi na mafisadi wa PAYE NI MKUBWA SANA INGAWA THAMANI YETU HAIONEKANI KAMA INAVYOSTAHILI.
NAWATAKIA UJENZI MWEMA WA TAIFA LETU.