Tetesi: Waraka kutoka Tamisemi kwenda kwenye Halmashauri zote

busegwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
527
199
Wadau nimepata tetesi kuwa waziri wa Tamisemi Mhe Simbachaweni ametoa waraka kwa halmashauri nzote nchini wasitangaze tenda za kukusanya ushuru ili Serikali ikusanye yenyewe kwa mwaka huu naomba mwenye taarifa atujuze naomba kuwasilisha hoja matusi na kejeli hazifai
 
kwani Halmashauri zote ni taasisi binafsi? ama una maanisha nini. Serikali ni nini?
 
waraka ni kufunika kombe tu lkn kiukweli WAZIRI ALITAKIWA KUJIUZULU
 
Kampuni yako ya kukusanya ushuru imeathirika mkuu,pole ndo kuisoma number jifunze hataa kuwa fundi bomba maisha ya (kilugu.....yanaelekea mwisho
 
Maafisa waandamizi tumeupata waraka mapema na uko vizuri.Vimetajwa vyanzo specific vikuzanywe na halmashauri na sio mawakala.Ni vile vyanzo tu ambavyo makusanyo yake yako certain.Mfano Property tax,hotel levy,billboard,land rent.kwa kuwa idadi ya mabango na size inajulikana unabinafsisha nini.Yale mengine ya parking fee nk ni kama kawa.Asanteni TAMISEMI kwa kuzingatia ushauri wangu
 
mfano: tenda ya kukusanya ushuru walikuwa wanapewa mawakala...

ushuru huo utozwa ktk machinjioni, sokoni, stendi, vyoo vya kulipia
na kwa mazao mbalimbali ya kilimo, baharini, misitu nk.

tenda za kukusanya ushuru zipo mikononi mwa watu binafsi ama serikali?, eleza vizuri jomba!!! Kwani walikuwa wanakusanyaje?

au bado ujaelewa?
 
tenda za kukusanya ushuru zipo mikononi mwa watu binafsi ama serikali?, eleza vizuri jomba!!! Kwani walikuwa wanakusanyaje?
serikali ilikuwa inaingia mikataba na mawakala(watu binafsi) ili wakusanye kwa niaba ya serikali.wakala alitakiwa kulipa kiasi fulani kwa serikali na ajikusanyie anavyotaka.mf unapewa ubungo terminal,unaipa serikali 50m kwa mwezi,wewe unakusanya mpaka 200m kwa mwezi.CCM wamekula sana nchi
 
Get u!!
 
kwa makosa gani?
Individual ministerial responsibility or Ministerial responsibility is a constitutional convention in governments using the Westminster System that a cabinet minister bears the ultimate responsibility for the actions of their line of accountability .
 
tenda za kukusanya ushuru zipo mikononi mwa watu binafsi ama serikali?, eleza vizuri jomba!!! Kwani walikuwa wanakusanyaje?
tenda zote za kukusanya ushuru wa serikali ni watu kampuni binafsindio zinapewa uwakala wa kukusanya na hii ni kwa mujibu wa sheria za manunuzi swali kama ni kweli katoa waraka hiyo sheria imebadilishwa lini au ss hivi kila anaemka anatoa waraka pasipo kuangalia sheria
 
Hii ni habar nzuri kwa watumishi waliokuwa wanalala ofisini huku kazi zikifanywa na mawakala..
 
Back
Top Bottom