Waraka kutoka kwa Tundu Lissu

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Anaandika Mhe. Tundu Lissu
============

Wakubwa salama?

Naona kuna watu wanahangaika sana na suala hili. Wapo ambao hawajawahi kututakia jema katika safari yetu ndefu ya kujenga demokrasia. Leo ndio wa kwanza kutoa machozi kwa kilichofanyika leo. Hayo ni machozi ya mamba na mimi sina haja ya kuwajibu. Kuna ambao wanalialia na kukata tamaa kwa sababu ya haya ya leo. Hawa nawaambia mapambano haya yanahitaji akili, sio jazba na hasira. Wengi hawaelewi kinachoendelea, wanafikiri haya ya leo ndio mwisho wa safari yetu. Hawa ndio ninahitaji kuwafafanulia kinachoendelea.

1. Msichanganye ratiba ya Tume ya Uchaguzi na ratiba ya Mahakama Kuu. Ratiba ya Tume imekamilika leo. Wanachokiita uchaguzi kimefanyika. Kazi yao imekwisha.

Ratiba ya Mahakama inaanza muda wowote kuanzia tarehe 29 Juni hadi 28 December, 2019. Maana yake ni kwamba ninaweza kufungua kesi katika siku yoyote ndani ya hicho kipindi cha miezi sita.

Hadi sasa hazijafika wiki tatu tangu uamuzi wa Spika Ndugai. Bado nina miezi mitano na wiki moja ya kufungua kesi. Kwa hiyo wanaolialia kwamba nimeachia ngazi, etc., wajue sijachelewa hata kidogo.

2. Mwenye haki ya kufungua kesi hiyo ni mimi mwenyewe au mwakilishi wangu ambaye nimempatia mamlaka ya maandishi ya kushtaki kwa niaba, yaani power of attorney.

Power of attorney inatakiwa kusainiwa na mimi mwenyewe mbele ya kamishna wa viapo anayetambuliwa na sheria za Tanzania, basically wakili anayefanya kazi Tanzania anatakiwa kuja kunishuhudia sahihi huku niliko.

3. Baada ya kusainiwa mbele ya kamishna wa viapo, power of attorney hiyo inatakiwa kusainiwa na huyo niliyemkabidhi mamlaka ya kuniwakilisha mahakamani, na saini yake hiyo ishuhudiwe pia na kamishna wa viapo.

4. Baada ya kusainiwa na wahusika wote, power of attorney hiyo inatakiwa kusajiliwa kwenye Ofisi ya Msajili wa Nyaraka Dodoma, Dar, Moshi au Mbeya na kulipiwa ushuru unaotakiwa.

5. Baada ya kusajiliwa ndio sasa kesi inaweza kufunguliwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

6. Sambamba na maandalizi ya power of attorney, nyaraka za kupeleka mahakamani zinatakiwa kuandaliwa kwa umakini mkubwa.

Hakuna ruhusa ya kukosea kwenye maandalizi ya nyaraka hizi. Kosa moja dogo tu na kesi yote inatupiliwa mbali. Kesi ya Josh Nassari ni mfano mzuri.

7. Kwenye kesi hii sisi hatuna ugomvi wowote na Tume ya Uchaguzi. Mgomvi wetu ni Spika Ndugai na uamuzi wake.

Tunachoenda kuiomba Mahakama Kuu iamue ni kama ni halali, kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanzania, kwa mbunge kuvuliwa ubunge kwa sababu zilizotolewa na Spika Ndugai, bila kuulizwa chochote au kupewa fursa ya kujitetea.

Na, pili, tutaiomba Mahakama Kuu ijibu swali la kama kweli Spika Ndugai hakujua mahali niliko kwa muda wote huu tangu September 7, 2017.

Mahakama Kuu ikikubaliana na Spika Ndugai, maana yake ni kwamba niliondolewa ubunge kihalali. Lakini ikisema kwamba Spika Ndugai alikuwa anajua niko wapi na alitakiwa anisikilize kwanza kabla ya kunivua ubunge, basi kilichofanyika leo kitakuwa sawa na sufuri.

8. Taratibu zote hizi za kufungua kesi zimekamilika kwa kiasi kikubwa. Kilichobakia ni kwa mawakili kumalizia malizia kupitia nyaraka zote ili twende mahakamani tukiwa na watertight case.

Natumaini wiki ijayo haitaisha kabla hatujaenda Mahakama Kuu.

Nimekaa kimya sana kwenye suala hili. Ukiwa maelfu ya kilometa nje ya nchi halafu unataka mambo yaende sawa Tanzania unahitaji utulivu na concentration. Vinginevyo utafanya makosa yanayotokana na upungufu wa umakini halafu utaonekana sio mtu makini. Natumaini maelezo haya yatakuwa yamewasaidia kupunguza hofu na kelele.
 
Sasa Kama wakili aweza kwenda ubelgiji kusaini alishindwaje kumwita asaini hati ya Mali aluzonazo na kupeleka tume ya maadili ya viongozi.Maana kwenye clip alijitetea akidai hati hiyo inatakiwa isainiwe na wakili wa Tanzania na yeye alikuwa ubelgiji.
 
Hata mimi kwa hili nilijiuliza sana, maana angeweza kuandika barua na akaituma kwa email. Itakuwa ni kiburi tu!
 
Peleka mahakamani.

Wakili uchwara hawezi kuwaza sahihi.

Tumuombee afya yake na akili pia
 
acha umburura ww..
ulishaambiwa kuwa baada ya kusaini izo nyaraka mbunge inatakiwa aziwasilishe kwa mkono kwenye ofis husika...

Back
Top Bottom