Wapinzani wamefikia malengo yao

Wapinzani wamefikia malengo yao

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Tangu kadhia ya kupitishwa 'kimagumashi' na 'kuchomekwa' kwa vifungu katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Katiba Bungeni Dodoma,wapinzani hawakulala.Hawakushindwa. Waliendelea kupigania ustawi wa nchi kupitia Katiba mpya bora nje ya Bunge.Wakaitisha mikutano miwili mikubwa: Jangwani na Kibanda Maiti. Wakaungwa mkono. Wakasikika.

Wapinzani walilenga mambo makubwa mawili. Kwanza, kumtaka Rais awe makini katika mchakato huu wa Katiba mpya kwakuwa unabeba mustakabali wa Taifa. Hapa, wakamuomba Rais asisaini Muswada husika.Pia, walitaka kusikilizwa na Rais katika kuwasilisha hoja zao. Walitaka majadiliano na maridhiano ya kitaifa na Rais. Lengo hili limefanikiwa.Mosi, taarifa rasmi za Ikulu zinaonesha kuwa Rais hakusaini Muswada husika. Pili,wapinzani jana wamekutana na Rais Ikulu kusikilizana na kuelewana. Lengo limetimia.

Pia, wapinzani walilenga kurejeshwa Bungeni kwa Muswada huo ili uweze kujadiliwa tena kwa maboresho yalengayo afya ya Taifa.Tayari,Rais 'ameshaamuru' Muswada urejeshwe Bungeni kwa marejesho.Waweza kurejeshwa ukiwa umeshasainiwa au la. Haijalishi. Lengo la pili limetimia pia.

Ingawa wapinzani walibezwa sana hasa na Waandamizi wa CCM yetu, muda si muda mantiki yao itaonekana kwa wengi au wote. Kupigania Katiba bora ni kupigania Taifa bora. Katiba ndiyo msingi wetu wa kwanza. Vingine vyote vinaifuata Katiba. Vingine vyote ndiyo.

Hongereni sana wapinzani: Mbowe,Lipumba na Mbatia na vyama vyenu kwa kufanikiwa hata kwa haya. CCM yetu ijifunze kuendana na wakati na mabadiliko yake.Watanzania si wale jamani,wamebadilika sana.Tusije tukabadilishwa kwa kura!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Tundu Lissu jana alimfunda JK vipengele vya sheria mpaka jamaa akachutama, Lissu yatosha!!!
 
Kamalengo la wapinzani lilikuwa ni kupata audience na Rais, basi wametimiza lengo hilo...
 
jana JK kamwambia Lissu,"... yatosha, upo sahahi, nakukubali...."
 
Kada mwenzangu ZeMarcopolo, 'audience' ni zaidi ya uijuavyo. Kwa Wanasheria kama mimi ni jambo kubwa mno.Ni pamoja na kusikilizwa na kueleweka. Ndio maana asiye Wakili hana audience mahakamani ingawa ni Mwanasheria. Rais atakuwa amewasikia na kuwaelewa wapinzani. Ni kutimiza lengo kuliko kawaida.
 
Last edited by a moderator:
Tangu kadhia ya kupitishwa 'kimagumashi' na 'kuchomekwa' kwa vifungu katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Katiba Bungeni Dodoma,wapinzani hawakulala.Hawakushindwa. Waliendelea kupigania ustawi wa nchi kupitia Katiba mpya bora nje ya Bunge.Wakaitisha mikutano miwili mikubwa: Jangwani na Kibanda Maiti. Wakaungwa mkono. Wakasikika.

Wapinzani walilenga mambo makubwa mawili. Kwanza, kumtaka Rais awe makini katika mchakato huu wa Katiba mpya kwakuwa unabeba mustakabali wa Taifa. Hapa, wakamuomba Rais asisaini Muswada husika.Pia, walitaka kusikilizwa na Rais katika kuwasilisha hoja zao. Walitaka majadiliano na maridhiano ya kitaifa na Rais. Lengo hili limefanikiwa.Mosi, taarifa rasmi za Ikulu zinaonesha kuwa Rais hakusaini Muswada husika. Pili,wapinzani jana wamekutana na Rais Ikulu kusikilizana na kuelewana. Lengo limetimia.

Pia, wapinzani walilenga kurejeshwa Bungeni kwa Muswada huo ili uweze kujadiliwa tena kwa maboresho yalengayo afya ya Taifa.Tayari,Rais 'ameshaamuru' Muswada urejeshwe BUngeni kwa marejesho.Waweza kurejeshwa ukiwa umeshasainiwa au la. Haijalishi. Lengo la pili limetimia pia.

Ingawa wapinzani walibezwa sana hasa na Waandamizi wa CCM yetu, muda si muda mantiki yao itaonekana kwa wengi au wote. Kupigania Katiba bora ni kupigania Taifa bora. Katiba ndiyo msingi wetu wa kwanza. Vingine vyote vinaifuata Katiba. Vingine vyote ndiyo.

Hongereni sana wapinzani: Mbowe,Lipumba na Mbatia na vyama vyenu kwa kufanikiwa hata kwa haya. CCM yeu ijifunze kuendana na wakati na mabadiliko yake.Watanzania si wale jamani,wamebadilika sana.Tusije tukabadilishwa kwa kura!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mbowe anaandaa Maandamano ya kumpongeza JK, yanaanzia Arusha, na kuishia Mbeya, ila Moshi hayapiti!
 
hongereni wapinzani kwa kuwapigania watanzania, aibu yao magamba
 
Hao mnaowaita wapinzani mnakosea,hawa ni warekebishaji wa tabia. Kama sio wao nchi hii ingekuwa kwishney,tungeshuhudia udhalimu mbaya kuwahi kuusikia .
Hongera warekebishaji wa tabia kwa pamoja,wazawa tupo bega kwa bega na nyie!
 
Sawa mkuu.Lakini, kwa makada wa CCM kama mimi itakuwa ngumu kuwaita 'Warekebishaji wa Tabia' ha ha ha ha ha ha ha ha!
 
Kada mwenzangu ZeMarcopolo, 'audience' ni zaidi ya uijuavyo. Kwa Wanasheria kama mimi ni jambo kubwa mno.Ni pamoja na kusikilizwa na kueleweka. Ndio maana asiye Wakili hana audience mahakamani ingawa ni Mwanasheria. Rais atakuwa amewasikia na kuwaelewa wapinzani. Ni kutimiza lengo kuliko kawaida.

huyo nesi vitu kama hivi kwake ni giza utatumia nguvu nyingi sana kumuelewesha!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Wewe huna lolote ni mwendelezo wa ulaghai ule ule ambacho CHADEMA inatumia kulaghai watu.

Unajifanya unafanya kazi ofisi ndogo Makao Makuu ya CCM na kuleta vi-propaganda vya kitoto katika jukwaa la siasa kufurahisha wasomaji wenye akili za kibavicha wakati hufahamu hata ofisi zake zimekaa vipi.

Wewe niwa kupuuzwa tu na hizi propaganda zako za kitoto ambazo haziwezi kukufanya kupata Uongozi Pwani kupitia CHADEMA.

Chama chenye mizizi ya kilaghai hakiwezi kusimama kwenye siasa za ukweli. Endelea na ulaghai wako kama kilivyo chama chako CHADEMA.
Tangu kadhia ya kupitishwa 'kimagumashi' na 'kuchomekwa' kwa vifungu katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Katiba Bungeni Dodoma,wapinzani hawakulala.Hawakushindwa. Waliendelea kupigania ustawi wa nchi kupitia Katiba mpya bora nje ya Bunge.Wakaitisha mikutano miwili mikubwa: Jangwani na Kibanda Maiti. Wakaungwa mkono. Wakasikika.

Wapinzani walilenga mambo makubwa mawili. Kwanza, kumtaka Rais awe makini katika mchakato huu wa Katiba mpya kwakuwa unabeba mustakabali wa Taifa. Hapa, wakamuomba Rais asisaini Muswada husika.Pia, walitaka kusikilizwa na Rais katika kuwasilisha hoja zao. Walitaka majadiliano na maridhiano ya kitaifa na Rais. Lengo hili limefanikiwa.Mosi, taarifa rasmi za Ikulu zinaonesha kuwa Rais hakusaini Muswada husika. Pili,wapinzani jana wamekutana na Rais Ikulu kusikilizana na kuelewana. Lengo limetimia.

Pia, wapinzani walilenga kurejeshwa Bungeni kwa Muswada huo ili uweze kujadiliwa tena kwa maboresho yalengayo afya ya Taifa.Tayari,Rais 'ameshaamuru' Muswada urejeshwe Bungeni kwa marejesho.Waweza kurejeshwa ukiwa umeshasainiwa au la. Haijalishi. Lengo la pili limetimia pia.

Ingawa wapinzani walibezwa sana hasa na Waandamizi wa CCM yetu, muda si muda mantiki yao itaonekana kwa wengi au wote. Kupigania Katiba bora ni kupigania Taifa bora. Katiba ndiyo msingi wetu wa kwanza. Vingine vyote vinaifuata Katiba. Vingine vyote ndiyo.

Hongereni sana wapinzani: Mbowe,Lipumba na Mbatia na vyama vyenu kwa kufanikiwa hata kwa haya. CCM yetu ijifunze kuendana na wakati na mabadiliko yake.Watanzania si wale jamani,wamebadilika sana.Tusije tukabadilishwa kwa kura!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Tangu kadhia ya kupitishwa 'kimagumashi' na 'kuchomekwa' kwa vifungu katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Katiba Bungeni Dodoma,wapinzani hawakulala.Hawakushindwa. Waliendelea kupigania ustawi wa nchi kupitia Katiba mpya bora nje ya Bunge.Wakaitisha mikutano miwili mikubwa: Jangwani na Kibanda Maiti. Wakaungwa mkono. Wakasikika.

Wapinzani walilenga mambo makubwa mawili. Kwanza, kumtaka Rais awe makini katika mchakato huu wa Katiba mpya kwakuwa unabeba mustakabali wa Taifa. Hapa, wakamuomba Rais asisaini Muswada husika.Pia, walitaka kusikilizwa na Rais katika kuwasilisha hoja zao. Walitaka majadiliano na maridhiano ya kitaifa na Rais. Lengo hili limefanikiwa.Mosi, taarifa rasmi za Ikulu zinaonesha kuwa Rais hakusaini Muswada husika. Pili,wapinzani jana wamekutana na Rais Ikulu kusikilizana na kuelewana. Lengo limetimia.

Pia, wapinzani walilenga kurejeshwa Bungeni kwa Muswada huo ili uweze kujadiliwa tena kwa maboresho yalengayo afya ya Taifa.Tayari,Rais 'ameshaamuru' Muswada urejeshwe Bungeni kwa marejesho.Waweza kurejeshwa ukiwa umeshasainiwa au la. Haijalishi. Lengo la pili limetimia pia.

Ingawa wapinzani walibezwa sana hasa na Waandamizi wa CCM yetu, muda si muda mantiki yao itaonekana kwa wengi au wote. Kupigania Katiba bora ni kupigania Taifa bora. Katiba ndiyo msingi wetu wa kwanza. Vingine vyote vinaifuata Katiba. Vingine vyote ndiyo.

Hongereni sana wapinzani: Mbowe,Lipumba na Mbatia na vyama vyenu kwa kufanikiwa hata kwa haya. CCM yetu ijifunze kuendana na wakati na mabadiliko yake.Watanzania si wale jamani,wamebadilika sana.Tusije tukabadilishwa kwa kura!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Tarehe10/10/2013 mswaada ulisainiwa sasa wewe unaongea nini leo hii bavicha bana.
 
Mbowe anaandaa Maandamano ya kumpongeza JK, yanaanzia Arusha, na kuishia Mbeya, ila Moshi hayapiti!
Sawa katibu mwenezi wa magamba tumekulewa na propaganda zako za kitoto
 
Wewe huna lolote ni mwendelezo wa ulaghai ule ule ambacho CHADEMA inatumia kulaghai watu.

Unajifanya unafanya kazi ofisi ndogo Makao Makuu ya CCM na kuleta vi-propaganda vya kitoto katika jukwaa la siasa kufurahisha wasomaji wenye akili za kibavicha wakati hufahamu hata ofisi zake zimekaa vipi.

Wewe niwa kupuuzwa tu na hizi propaganda zako za kitoto ambazo haziwezi kukufanya kupata Uongozi Pwani kupitia CHADEMA.

Chama chenye mizizi ya kilaghai hakiwezi kusimama kwenye siasa za ukweli. Endelea na ulaghai wako kama kilivyo chama chako CHADEMA.
Tungekuona una busara kama ungeishambulia hoja yake badala ya kumshambulia yeye binafsi!
 
Kada mwenzangu ZeMarcopolo, 'audience' ni zaidi ya uijuavyo. Kwa Wanasheria kama mimi ni jambo kubwa mno.Ni pamoja na kusikilizwa na kueleweka. Ndio maana asiye Wakili hana audience mahakamani ingawa ni Mwanasheria. Rais atakuwa amewasikia na kuwaelewa wapinzani. Ni kutimiza lengo kuliko kawaida.

Na ndo maana hata Wasira na wenzake hawakulipenda hilo litokee kamwe!!.
Sababu wanalijua umuhimu wake..
 
Last edited by a moderator:
huyo nesi vitu kama hivi kwake ni giza utatumia nguvu nyingi sana kumuelewesha!!!!!!!!!!!!!
Wewe huwa sikuelewi kama ni mtu au binadamu make katika watu ambao wanaongea ubwabwa wewe wa kwanza.
 
Wewe huna lolote ni mwendelezo wa ulaghai ule ule ambacho CHADEMA inatumia kulaghai watu.

Unajifanya unafanya kazi ofisi ndogo Makao Makuu ya CCM na kuleta vi-propaganda vya kitoto katika jukwaa la siasa kufurahisha wasomaji wenye akili za kibavicha wakati hufahamu hata ofisi zake zimekaa vipi.

Wewe niwa kupuuzwa tu na hizi propaganda zako za kitoto ambazo haziwezi kukufanya kupata Uongozi Pwani kupitia CHADEMA.

Chama chenye mizizi ya kilaghai hakiwezi kusimama kwenye siasa za ukweli. Endelea na ulaghai wako kama kilivyo chama chako CHADEMA.
Una uhakika Mwenezi na unachokisema? Fanya utafiti kwanza Mkuu. Jenga hoja kulinda heshima yako. Mimi sijawahi kuhama chama kama wewe tangu ujana wangu.Karibu Ofisini tuongee vyema
 
Wewe huwa sikuelewi kama ni mtu au binadamu make katika watu ambao wanaongea ubwabwa wewe wa kwanza.
Na ww huwa sikuelewi kama coordination ya mwili wako upo well coordinated, nimejiridhishaga kitambo kuwa coordination of your body system is quiet improper!
 
Back
Top Bottom