sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,491
Wenye nchi (watawala) wanasema tupo tayari sasa kujitegemea, huku wapinzani wanasema tunahitaji kujitegemea ila siyo sasa. Tuelezeni ni lini tunapaswa kujitegeme?
Hakuna mpangaji anayesubiri hadi nyumbani kwake kuwekwe geti, garden zipendeze, ama rangi ikauke ndipo ahamie huku anaumia na kodi. Wengine huhamia hata nyumba ikiwa na mlango mmoja wakati anamalizia, mwisho wa siku nyumba inakamilika taratibu. Tukisubiri tuweze kujitegemea kila kitu ndipo tusitishe misaada ni uwongo.
Tanzania kukataa misaada yenye masharti 17 ambayo Watanzania hatuyajui na pengine wanataka kuongeza yawe 47, ni sawa na mpangaji aliyeamua kuhamia myumba yake ambayo haijaisha aimalizie pole pole kuepuka kero za kupanga. Mara nyingi baba anapoamua tuhamie nyumba kabla haijaisha, mama ndiye hukataa. Hofu ya wapinzani ni sawa na hofu ya mama ya kuhamia nyumba ambayo haijaisha.