Uchaguzi 2020 Wapinzani mwaka huu mmekosea kabisa kwenye Kauli Mbiu

Mwanafalsafa

Platinum Member
Jun 24, 2007
662
851
Kaulimbiu ya mwaka huu haikutakiwa kuwa, "Maendeleo ya watu, sio vitu."

Haikutakiwa kuwa hii kwa sababu hii ni kaulimbiu inayofikirisha na haikamati vizuri kwa kuwa ni ngumu kutenganisha maendeleo ya watu na ya vitu. Matokeo yake mnahangaika sana kuanza kufafanua maana ya kaulimbiu.

Sifa ya kaulimbiu haitakiwi kufikirisha. Inatakiwa imkamate mtu pazuri, na imkamate mara moja, bila ya maelezo mareeefu.

Au ile ya "Kazi na bata" imekaa kizushi sana. Hakuna mtu anayeichukulia serious.

Mfano 2015 kaulimbiu ya "Tunataka mabadiliko" ilikamata watu vizuri sana. Kulikuwa hakuna cha kufikiria. Kaulimbiu ilikuwa inafagia kila kitu, kwamba cha kwanza ni mabadiliko, mengine ndo yatafuata.

Sasa sitaki kusema hadharani kauli mbiu gani ni nzuri. Ninayo tayari na ukiisikia tu lazima utakubali kwamba hiyo ndo yenyewe. Kama kuna mpinzani anataka kujua anicheki inbox tuongee biashara.
 
Kama kungekuwa na maendeleo ya watu,
Wangeanza kwanza wazungu
Lakini mbaka leo ukienda ulaya na marekani unakutana na maendeleo ya vitu
Barabara nzuri
Fly over
Barabara zingine ziko mbaka chini ya bahari
Train za umeme dala dala
Magari ya Taka yanazoa taka yenyewe bila tan boy ( maarufu kuri
Hakuna mbu
Hakuna nzi
Hakuna vumbi
Lakini cha kushangaza omba omba kama wote
Watu ni maskini zaid kuliko africa
Na watu ni matajiri zaid kuliko serikali
hiyo ndio ulaya na america maendeleo ya vitu kwanza watu watasubiri sana.
Slowgan ya wapinzani ni kelele za walevi wa faru john..
 
Back
Top Bottom