Kauli mbiu zisiishie kwenye maneno tunanahitaji vitendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli mbiu zisiishie kwenye maneno tunanahitaji vitendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jan 29, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tufanye maamuzi magumu,tuwe na utayari wa kuthubutu tutavuka malengo,kauli mbiu ndani ya nchi yetu zinashamiri siku hadi siku.Kila kukicha utasikia oh mara kilimo kwanza,oh mapinduzi ya kijani,ari mpya zaidi,kasi mpya zaidi na nguvu mpya zaidi.Tukisema kuandika kauli mbiu hizi tunaweza jaza kitabu,lakini mbona kauli mbiu hizi haziendani na hali halisi na matendo ya wahusika wakuu?Mara nyingi kauli hizi zimekuwa kinyume kabisa cha matarajio ya walio wengi.Kuna mikakati kama vile MKURABITA,haieleweki nini maana yake na nini hasa makakati wake,wananchi kabla ya kuufahamu mkakati huu ukafa kifo ambacho wananchi husika tuliokusudiwa hatukutaarifiwa maziko yake.Swali la kujiuliza kauli mbiu hizi zina tija katika maendeleo ya taifa hili au ndo blabla tu.

  Tanzania ni ya kwetu sote,kila mmoja ana haki sawa mbele ya sheria ya kutambuliwa utu wake,ndo maana hata mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema ili tuendele tunahitaji vitu vinne muhimu.watu ardhi,siasa safi na uongozi bora.Hakuna sehemu ndani ya katiba yetu inayozungumzia kauli mbiu.Umahiri wa kutoa maneno ungeendana na utekelezaji kwa vitendo tungepiga hatua mbali.Matokeo ya kushindwa kutekeleza kauli kwa vitendo ni kejeli na matusi kwa wananchi.Mfano mzuri wa kejeli hizo ni kama vile ndege ya rais lazima inunuliwe kwa gharama yoyote hata kama wananchi watakula nyasi.Si hayo tu,matusi ni mengi sana kisa wananchi wanahoji nini matokeo ya kauli hizo.Tuliambiwa tatizo la umeme sasa ni ndoto na historia,kilichotokea kweli ni ndoto na historia,uchumi wa nchi umeanguka kutokana na kushuka kwa uzalishaji,mipango ikawa ya kidharura mpaka tunamaliza awamu ya kwanza ya rais wa awamu ya nne.Hali hiyo haikuishia hapo,watu walipohoji nini mkakati wa serikali kuondoka katika janga hili,majibu yake yanatia kichefuchefu,eti mimi si Mungu kuweza kupanga mvua.Hatari yake nini,nchi inapoteza mapato na mfumuko wa bei unakithiri kutokana na kutoa na mipango ya muda mrefu,wa kati na mfupi.

  Iko wapi ile kauli ya maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana,wakati inaandaliwa manifesto ya chama hawakujua kuwa kauli mbiu hiyo haitekelezeki.Kuna kinara gani leo hii wanaeweza kusimama na kusema maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana akaeleweka kwa wananchi.Uswahili huu hata kwa mambo ya msingi,tuwezaje kuikomboa nchi yetu iliyozama katika kuzalisha matabaka ya watwana na mabwana.Kama ni mifumo ya kimaisha mbona tumeanza kwenye ujima tukafanikiwa mpaka tumefikia hapa tulipo,tena wakati huo tulitumia zana duni.Ni ukweli usiopingika binadamu hupitia mabadilliko mbalimabali ya kifizikia kutokana na umri,alkini cha ajabu badala ya kusonga mbele tunarudi zama zile za mawe.Hatukuwa na nyenzo lakini tulijikomboa tukagundua moto uliosababisha tuweze kula vyakula vilivyopikwa.Teknolojia imekuwa sana lakini fikra zetu zimefika kikomo.Tusiwe wepesi wa kuzindua mapya wakati tuliyoyaanzisha tumeshindwa kuyakabili.

  Wakati tunadai uhuru wa nchi yetu,tulithubutu na tuliweza tukapata uhuru kwa njia ya amani bila kumwaga damu.Leo tunashindwa nini,kutumia dhamira zile zile katika kuleta maendeleo ya kweli kwa kila mtanzania.Kilimo tuliamini ni uti wa mgongo wa taifa letu,tulifanya kazi zetu kijamaa bila kujenga tabaka la wenye nacho na wasio nacho tukafanikiwa,lakini mambo yamegeuka.kila mmoja analalamika.vipau mbele hakuna,,kilichobaki tunakurupuka na kupaka rangi upepo.

  Tunachotakiwa ni kubadilika na kufanya mapinduzi ya fikra,ili kauli mbiu zetu zilete tija na mashiko kwenye nchi yetu.Tufanye kazi tuache kauli zisizo na mantiki,kila mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kazi.Ujamaa na kujitegemea uwe kweli ndo mfumo tuliokubali na kuufuata kwa vitendo,Haiwezekani ukaimba kijamaa kisha ukacheza kibepari.Anayeshindwa kutekeleza wajibu wake rungu la dola limpitie bila kujali mtoto wa shangazi au mjomba.Vijana ni taifa la leo nguvu kazi ya vijana ilete mabadiliko mapya kutokana na changamoto zinazotukabili.Nawakilisha
   
 2. T

  TUMY JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeandika makala nzuri sana mkuu, ila katika kuongeza kidogo tu suala la KUWAJIBISHANA nalo, kwani tumekuwa tukiogopa kuwajibishana pale ambapo inabidi, kama uliahidi jambo ukaleta longolongo basi wawajibishwe wahusika.
   
Loading...