Kauli mbiu yetu ya Tanzania ya viwanda imejifunza nini kutoka China

Ayubu Massau

Member
Apr 24, 2015
16
43
KAULI MBIU YETU YA TANZANIA YA VIWANDA IMEJIFUNZA NINI KUTOKA CHINA.


SEHEMU YA KWANZA

Ndugu ,

Watanzania na Wanabodi

Huu Ni Mwaka Mpya Wa 2018, Ambao Ndio Umeanza Ukiwa Mbichi Kabisa , Lakini Mwaka Huu Unasogeza Mbele Na Kutuelekeza Tukiwa Tumebakiwa Na Miaka Takribani 7, Kukamilisha Dira Ya Maendeleo Ya Taifa Mwaka 2000-2025.

Katika Dira Hii Inatuelekeza Tanzania Kufikia Uchumi Wa Kati Na Kutoka Kundi La Nchi Maskini Duniani Ifikiapo 2025.

Kichecheo kikubwa cha kutupeleka uchumi wa kati , kwa kuboreka hali ya uchumi wa taifa na Tanzania ya viwanda, kama inavyohubiriwa katika sehemu mbalimbali za nchi, jambo ambalo ni zuri na la kutia faraja na matumaini.

Neno, Tanzania ya viwanda limeanza kupata umaarufu ,wakati wa Kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka 2015, ni sera nzuri sana na yenye kutia matumaini kwa wale wote wanaofahamu umuhimu wa viwanda katika ukuaji wa uchumi, katika taifa lolote lile.

Bahati mbaya au nzuri , wahusika wanaotakiwa kutupa Mwongozo wa Tanzania ya viwanda hawajaitoa hadharani ,ili kila mtanzania na wawekezaji toka nje wajue dira yetu katika Tanzania ya viwanda ikoje , japo dondoo tu ambazo zingekuwa Mwongozo ni aina gani za viwanda vinavyotakiwa na malighafi zake zinapatikana wapi.

Kwa kuwa sijapata wala kusikia dondoo za Tanzania ya viwanda , kuanzia sera zake, mpango kazi wake hadi Utekelezaji wake na uhusika wa watanzania moja kwa moja , mimi nitajaribu kuangazia Mapinduzi ya viwanda nchini china ,iliyopata uhuru mwaka 1949 na kuwa Jamhuri ya watu wa china chini ya Uongozi wa rais Mao Tse Tung ( Mao Ze Dong),ni miaka 12 mbele ya uhuru wa Tanganyika ( Tanzania bara) .

Sera Na Mikakati Ya Mapinduzi Ya Viwanda Nchini China.

Mapinduzi ya viwanda china ya sasa yalianza miaka 36 iliyopita , wataalam wa uchumi ,wana Sayansi na wana zuoni mbalimbali huyatazama kama Mapinduzi yenye kasi ya ajabu , tangu Mapinduzi ya viwanda nchi za ulaya miaka 250s iliyopita.

Mapinduzi haya ya viwanda nchini china ,hayakuja hivihivi kwa kutamka tu ,bali mojawapo ya sababu kuu ya Mapinduzi haya ni china kugundua wao ni taifa lenye watu wengi duniani,hivyo wana rasilimali watu na nguvu kazi kubwa zaidi ya kuzalisha malighafi zitakazoweza kutumika viwandani.

China waligundua , chini ya Asilimia 10 ya wakazi wote duniani wameshafanya Mapinduzi ya viwanda na nchi hizi nyingi zilikuwa nchi za ulaya na marekani. China wakagundua kama wao wakifanikiwa katika Mapinduzi ya viwanda itaongeza Asilimia zipatazo 20 katika Mapinduzi ya viwanda duniani na hivyo dunia kuingia katika utawala mpya wa teknolojia na viwanda.


Ukuaji wa uchumi na Mapinduzi ya viwanda nchini china ,ulizishangaza nchi nyingi duniani hasa mataifa ya ulaya na marekani wakiwemo wana uchumi wakubwa duniani, walijiuliza maswali mengi ya kinadharia yasiyo na Majibu , Moja ya swali hilo ni “ inakuwaje nchi yenye watu wapatao bilioni 1.4 kutoka kwenye kilimo kisicho na manufaa na kuwa nchi ya viwanda” wakati nchi nyingi ndogondogo Zenye watu wachache na eneo dogo zimeshindwa kufanya Mapinduzi ya viwanda japo zina mazingira mazuri na yenye kushawishi ukuaji wa uchumi.

Kutokana na ukuaji wa china kiuchumi na Mapinduzi ya viwanda kuwashangaza wana uchumi wengi duniani ( nitaeleza sera na mikakati china iliyotumia katika mwendelezo wa makala hii mbele), wengi walikuwa na maoni tofauti , lakini maoni hayo yaliegemea pande kuu mbili,

Moja “ wapo aliyoina china kama serikali kubwa sana ,ambayo haiko imara na ingesambaratika kwa sababu haikuwa na demokrasia ya kimagharibi,hakuna haki za binadamu,hakuna uhuru wa kuzungumza,hakuna utawala wa sheria,hakuna mifumo ya kimagharibi katika utawala,hakuna masoko mazuri yaliyopangiliwa,hakuna benki binafsi, hakuna ulinzi wa maandiko ya wataalam/wasomi(intellectual properties), hakuna uwezo wa kufanya ugunduzi zaidi ya kukopi na kuiba teknolojia ya nchi za magharibi na biashara za siri, haimiliki vitu vingi dhidi ya nchi ya magharibi ambazo zimemiliki kwa karne nyingi” kwa mtazamo huu wachambuzi wengi wa uchumi baada ya uhuru 1949, waliiona china kama taifa litakaloporomoka muda wowote kama ilivyokuwa huko nyuma.

Kundi la pili, lilikuwa na mtazamo huu kuhusu china “kundi hili liliona ukuaji wa china na Mapinduzi ya viwanda umetokana na historia yake ya vizazi na vizazi na kuhusisha na Tawala zake za kifalme huko nyuma, kwa Mujibu wa historia, china ilikuwa taifa tajiri na kubwa na taifa la kwanza kustaaribika kwa kuwa na mifumo iliyoeleweka kuanzia miaka ya 200K.K hadi 1800K.K, kundi hili linafikiri ilikuwa ni suala la muda tu china kurudisha hadhi yake tukufu ya kutawala tena dunia” maono ya kundi hili la pili yanapata mkazo na msisitizo kupitia Kauli ya mfalme wa Kifaransa enzi hizo (King Napeleon Bonaparte) alivyosema, nanukuu “Let china sleep for a while, when the dragon awakes, she will shake the world” Mwisho wa kunukuu.

Japokuwa ,Makundi hayo mawili yalikuwa na mitazamo yao katika maono,lakini yanachagizwa na u sirias katika Uchambuzi wa kiuchumi, badala ya kutegemea katika Upande wa historia na mawazo ya kufikirika, wachumi waliendelea Kujiuliza hili swali “inakuwaje nchi isiyo kuwa na biashara zinazoeleweka na Ufanyaji tafiti /ugunduzi kuwa na uwezo wa kukua kiuchumi na kufikia digit mbili kwa mwaka, Mfululizo kwa miongo mingi na kufanya mabadiliko yenyewe kwa muda mfupi, kutoka uchumi wa kilimo kisicho na tija hadi kuwa ngome ya Mapinduzi ya viwanda”

Wana uchumi wakubwa ,duniani waliendelea Kujiuliza, kama ni suala la utamaduni na mahusiano ya jamii za kale zilizoanza kustaarabika mapema, Je Kwanini, nchi kama Misri,Ugiriki na Dola la Ottoman wameshindwa kufikia hatua hiyo?. Swali hili limekuwa gumu sana kupata Ufumbuzi juu ya Mapinduzi makubwa ya viwanda nchini china.

Andiko ,hili linajaribu tu kutuelewesha wenzetu china walipotoka na walivyofanikiwa katika Mapinduzi ya viwanda ,kama sisi tunavyoimba Tanzania ya viwanda.

Itaendelea......
 
KAULI MBIU YETU YA TANZANIA YA VIWANDA

Neno, Tanzania ya viwanda limeanza kupata umaarufu ,wakati wa Kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka 2015, ni sera nzuri sana na yenye kutia matumaini kwa wale wote wanaofahamu umuhimu wa viwanda katika ukuaji wa uchumi, katika taifa lolote lile.

Bahati mbaya au nzuri , wahusika wanaotakiwa kutupa Mwongozo wa Tanzania ya viwanda hawajaitoa hadharani ,ili kila mtanzania na wawekezaji toka nje wajue dira yetu katika Tanzania ya viwanda ikoje , japo dondoo tu ambazo zingekuwa Mwongozo ni aina gani za viwanda vinavyotakiwa na malighafi zake zinapatikana wapi.

Kwa kuwa sijapata wala kusikia dondoo za Tanzania ya viwanda , kuanzia sera zake, mpango kazi wake hadi Utekelezaji wake na uhusika wa watanzania moja kwa moja
.
Mkuu Ayubu Massau, kwanza asante sana, kwa uzi huu, hii ni moja ya threads bora kabisa ya kufungulia mwaka!.

Jambo ulilolizingumza hapo ni jambo la muhimu sana, Tanzania yetu ya viwanda ni Tanzania ya Kauli ya Tanzania ya viwanda, ili kuvunia kura za Watanzania lakini hakuna blue print, smart objectives, wala implemention plan!.

Uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo focus ya Tanzania ya viwanda, ilipaswa iwe kwenye agroprocessing industries and manufacturing iwe ya pili, na assembling ndio ya mwisho.

Hivyo uwekezaji mkubwa ulibidi kufanywa kwenye sekta ya kilimo inayotumiwa na 63% ya Watanzania ili izalishe malighafi ya Tanzania ya Viwanda.

Angalia focus yetu ya uwekezaji mkubwa kununulia ndege, SGR, Flyovers na miundomninu ambayo inazamisha billions which has nothing to do with kuinua sekta ya kilimo.

Kwa sasa viwanda vikubwa vya chakula ni S.S. Bakhresa, anachofanya ni kusaga tuu unga wa ngano, ngano yote ni imported 100%, yale mashamba ya ngano kule Babati, yamejaa nyasi Wamasai wanalishia mifugo.

Zile juice za matunda 80% ni imported pulp, only 20% ndio matunda yetu!. Kwenye final product inaandikwa Tanzania product na kupatiwa certificate of orgin kuonyesha imeoriginate Tanzania!, Kenya wamekataa ujinga huu kwa kuzuia products hizo kuingia kwenye EA Common Markets kwa zero tarrif as local, while raw materials zote ni imported!.

Kiwanda kikubwa cha nguo kinachoongoza kwa ku export ni Star Apparel kilichopo pale Mabibo kwenye EPZA, kila kitu kuanzia vitambaa hadi vifungo, ni imported!. Contributions yetu ni nguvu kazi tuu, washona nguo, na kuwa exported kwenye soko la USA, as made in Tanzania!, wakati pamba yetu pale Mwanza, inaozea shambani kwa kukosa masoko!. Viwanda vyote vya khanga hadi Urafiki, vina import bales za raw materials na kuzalisha nguo na sio kuiprocess pamba yetu!.

Nasubiri muendelezo ndipo niendelee kucomment

Paskali
 
I see hadi bidhaa za china zipigwe marufuku na pia bidhaa za ndani ziuzwe kama bei za bidhaa za kichina... la sivyo Ni kudanganyana na keleteana hasara tu.... na kurudishana nyuma kimaendeleo.

Mwanzoni nilijua sera ya viwanda ni serikali ila bajeti ya kiwanda cha Matairi general Tyre nilipoisikia nikaona usanii jazz band tu. Sometimes siamini why serikali haiwezi kuanzisha viwanda inavyovihubiri.

Nyerere alikiwa akisafiri nje za nchi akiona kiwanda huko kimebadilisha technology na kuwa mpya aliomba tech ya zamani auziwe na wazungu wajapani hawakuwa na hiyana walimpa bure kwa kumcheka ila Nyerere alijua vitasaidia tu kama wao vilivyowasaidia ila Tanzania ya sasa hatujielewi kama misukule
 
Ayubu Massau Umeleta mjadala Wa jambo jema sana. Juzi nilipandisha hapa mjadala kuhusiana na kwa nini Viongozi Wa Serikali na wanaopewa nafasi hiyo na Raisi Magufuli hawatimizi matarajio yake. Na nikaenda mbali kusema sio Viongozi tu pekee Bali hata wananchi walio wengi pia hawaelewi Kiongozi wetu anayo maono gani na muelekeo gani dhidi ya Taifa hili.

Nilipanga kuendelea na sehemu ya pili,tatu,nne,Tano na sita juu ya nini kifanyike. Lakini kwa ufupi,niseme tu kuwa ufumbuzi Wa matatizo yetu kama Viongozi na wananchi kwa ujumla uko katika kubadili mitazamo yetu na akili zetu( Mindsets) na jinsi tunavyohusianisha mantiki na akili katika kuamua na kutenda. Hapo ndipo tatizo msingi lilipo.

Huwezi kuwa na maendeleo katika Taifa ambalo watu wake bado wanaamini na kulaani kuwa shida hizi tunazozipata wanadamu/ Watanzania ni kwa sababu Adamu na Hawa walitenda dhambi Bustanini Edeni vinginevyo tungekuwa hatufanyi kazi yoyote ile na maisha yangekuwa yanaendelea kama kawaida na raha mstarehe.

Taifa au jamii ya watu wenye fikra kama hizo ni Taifa la watu wavivu. Ni Taifa la watu wanaosubiria kunyakuliwa kwenda Mbinguni. Ni Taifa la watu waliotega masikio kusikiliza Parapanda Italia kutokea upande upi Wa Dunia ili wakamlaki "Bwana" mawinguni.


Umetolea mfano Wa kuigwa Wa Wachina na Taifa lao. Kwa wale tunaoenda nje na kwa muktadha Wa mfano wako China,ni kwamba Wachina wana utamaduni Wa Umoja.Ushirikiano. Wanafanya mambo kwa pamoja. Hili unaweza kuliona hata namna wanavyokula chakula ama cha mchana au Usiku kwa familia au marafiki pamoja. Siku zote ukiona mahali popote, watu wanahangaika kuwa pamoha ujue na uelewe watu hao wanasukumwa na kiu ya kazi. Kiu ya kufanikisha mambo haraka. Kwetu hapa ni kinyume kabisa.
 
Viwanda siyo majengo ni teknologia. Kutamka Tanzania iwe nchi ya viwanda hakutufanyi tuwe nchi ya viwanda. Viwanda haviji kwa habla kadabra au mazingaombwe. Viwanda ni teknologia ya kuweza kuzalisha bidhaa au kutengeneza malighafi. Hivi viwanda vinahitaji kulishwa ghafi ili kutengeneza hicho tunachokusudia. Hiyo technologia kama mtambo unahitaji wataalamu waendeshaji na unahitaji wataalamu kuukarabati pia unahitaji vipuri vipya au tufanye forging/ tuvifue wenyewe. Kama hatuna taaluma hiyo tuwe na reliable source ya kuvipata vipuri hivyo na tuwe na fund ya kulipia hizi regular au periodic maintanance.

Viwanda vinahitaji designer engineer na utaalam mwingi.
Sisi tunajivunia eti matamshi na utashi wakuwa na Tanzania ya viwanda lakini hatuna knowledge ya katengeneza machines/mitambo hiyo ya kutengeneza hata karakana za kuweza kuvi mentain viwanda hivyo.

Eti kuna amri au tamko linawaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha wanalitekeleza agizo la kuwa na viwanda kila mkoa. Hivi ni vituko kama siyo vichekesho.

Huko mikoani nani avijenge viwanda hivyo?! Wakuu wa mikoa au nani?! Wanajenga viwanda v ya kutengeneza nini?! Kwa teknologia ipi au yanani?! Pesa inatoka wapi na wataalamu tunao?! Wataalamu wa fani gani?! Malighafi tunazo?! Je tunazo karakana na ma engineer au matechnitians wa kutengeneza au kukarabati machine zikiharibika?! Tunao wataalamu wa kufanya processing huko viwandani?! Sipati jibu.

Sera, utashi na maagizo ni tofauti kama tungekuwa na wataalam na teknologia ya kuvitengeneza viwanda na ku vi operate machines.

Idadi ya watu ni factor ya mwisho kwenye viwanda. Unaongelea watumiaji wa bidhaa au soko la ndani.

Tunge weka goal ya nini tunataka kutengeneza au kuzalisha baada ya kufanya upembuzi wa malighafi kwanza, je tunazo?! Kisha tu train wataalamu kisha tutafute nani yuko tayari kutoa teknologia kwa msaada au kununua. Kisha tuwe na programs za kuendelea kuzalisha wataalam ndani kwa gharama nafuu.

Lakini sisi hatuko organized, eti tunadhani amri na matamko paap yanaleta au kuzaa kiwanda.

Viwanda vinahitaji mkakati wa kitaaluma siyo, hizi mnaita ILANI.
 
Mafwi Munda Technologia ipo na inanunulika, kinachotakiwa ni kwenda kwa stage moja na stage tukitaka Leo kushindana na wachina tutajikwaa, Ili tufanikiwe tuanze n very intermediate stages za production, na tujenge uwezo as we grow, unayoyasema ni moja ya failures zilizotuweka hapa, tunajidharau wenyewe
 
Technologia ipo na inanunulika, kinachotakiwa ni kwenda kwa stage moja na stage tukitaka Leo kushindana na wachina tutajikwaa, Ili tufanikiwe tuanze n very intermediate stages za production, na tujenge uwezo as we grow, unayoyasema ni moja ya failures zilizotuweka hapa, tunajidharau wenyewe

Hahaha, tunajidharau?! Sema hatuna skills za kuendesha mitambo ya uzalishaji.Tuseme ukweli sio kubeba pride wakati ni kweli hatuwezi. Kama teknoligia zipo mnapesa za kuzinunua?! Matrekta ya kilimo kwanza mnanunua yakiharibika hamna vipuri hata kama mna ma engineer, je wanatosha?!

Mnaogopa kusema ukweli eti kisa mtaonekana mnajidharau?! Bora mseme ukweli hitaji lenu litafutiwe tiba ya kudumu kuliko kutibu symptoms kila siku.
 
Hata mchina viwanda vingi na vikubwa sio vyake. Anatumika kutoa cheap labor tu, kitu ambacho hata sisi tumeshindwa kufanya. Ukiona made in china haimaanishi kiwanda au technologia ni ya mchina, wachina wengi ni wafanyakazi wa kawaida sio technological expert au skilled workers.

Nyie mnaona wazungu wanachimba madini kwenu mnadhani wanaenda kuvaa shingoni kama sisi?! Kujifunza hamtaki na mkiambiwa hamjui mnakimbilia pride eti ohoo tunajidharilisha mara tunadharilishwa.
Technologia ndiyo viwanda siyo ILANI.
 
Umeleta mjadala Wa jambo jema sana. Juzi nilipandisha hapa mjadala kuhusiana na kwa nini Viongozi Wa Serikali na wanaopewa nafasi hiyo na Raisi Magufuli hawatimizi matarajio yake. Na nikaenda mbali kusema sio Viongozi tu pekee Bali hata wananchi walio wengi pia hawaelewi Kiongozi wetu anayo maono gani na muelekeo gani dhidi ya Taifa hili.

Nilipanga kuendelea na sehemu ya pili,tatu,nne,Tano na sita juu ya nini kifanyike. Lakini kwa ufupi,niseme tu kuwa ufumbuzi Wa matatizo yetu kama Viongozi na wananchi kwa ujumla uko katika kubadili mitazamo yetu na akili zetu( Mindsets) na jinsi tunavyohusianisha mantiki na akili katika kuamua na kutenda. Hapo ndipo tatizo msingi lilipo.

Huwezi kuwa na maendeleo katika Taifa ambalo watu wake bado wanaamini na kulaani kuwa shida hizi tunazozipata wanadamu/ Watanzania ni kwa sababu Adamu na Hawa walitenda dhambi Bustanini Edeni vinginevyo tungekuwa hatufanyi kazi yoyote ile na maisha yangekuwa yanaendelea kama kawaida na raha mstarehe.

Taifa au jamii ya watu wenye fikra kama hizo ni Taifa la watu wavivu. Ni Taifa la watu wanaosubiria kunyakuliwa kwenda Mbinguni. Ni Taifa la watu waliotega masikio kusikiliza Parapanda Italia kutokea upande upi Wa Dunia ili wakamlaki "Bwana" mawinguni.


Umetolea mfano Wa kuigwa Wa Wachina na Taifa lao. Kwa wale tunaoenda nje na kwa muktadha Wa mfano wako China,ni kwamba Wachina wana utamaduni Wa Umoja.Ushirikiano. Wanafanya mambo kwa pamoja. Hili unaweza kuliona hata namna wanavyokula chakula ama cha mchana au Usiku kwa familia au marafiki pamoja. Siku zote ukiona mahali popote, watu wanahangaika kuwa pamoha ujue na uelewe watu hao wanasukumwa na kiu ya kazi. Kiu ya kufanikisha mambo haraka. Kwetu hapa ni kinyume kabisa.
Hii imekaa poa sana ni ukweli kabisa
 
Tanzania hata ustaarabu hatuna.
Serikali haijali wananchi wake, siasa za ajabu
Wananchi hawataki kazi wanashinda kujadili siasa na kujazana chuki baina yao.
Wachina wapo vizuri sana, by 2020 wamepanga kufuta umaskini.

Wao pamoja na kwamba wana historia ya ustaarabu na uvumbuzi lkn wanawatoa vijana kwenda kusoma nje, wanarudi kuijenga nchi yao effective , wana wataalam wa kila aina ambao wameendelea kuvumbua vitu kurahisisha maisha ya jamii yao.

Walitengeneza mitaala ya elimu kulingana na mahitaji yao, wanajitahid sana kuepuka kucopy na kupaste kila kitu cha magharibi.

Kama nchi tunayo matatizo makubwa kuanzia mindset, mitaala ya elimu, katiba n.k ni kama tambala bovu.
 
Hahaha, tunajidharau?! Sema hatuna skills za kuendesha mitambo ya uzalishaji.Tuseme ukweli sio kubeba pride wakati ni kweli hatuwezi. Kama teknoligia zipo mnapesa za kuzinunua?! Matrekta ya kilimo kwanza mnanunua yakiharibika hamna vipuri hata kama mna ma engineer, je wanatosha?!
Mnaogopa kusema ukweli eti kisa mtaonekana mnajidharau?! Bora mseme ukweli hitaji lenu litafutiwe tiba ya kudumu kuliko kutibu symptoms kila siku.

Kwani tumeshindwa kukaribisha viwanda vya vipuri vya matrekta hapo bongo? Kwani hao investors ukimuita john deer akasimika kiwanda chake mwanza, kwa makubaliano ya miaka kumi baada ya hapo anatuachia tukiendeleza wenyewe

Hivo tu Serikali yenu na rais niliyempigia kura ameshindwa kufanya
Huku china kuna viwanda vingi sana kutoka magharibi, wanazalisha bidhaa mbalimbali
 
Tatizo ni porojo tu, waliokuwepo madarakani ndiyo hao hao waliopo sasa watueleze kabla hawatoa manifesto yao walifanya research ya kitalaam kwa muda gani juu ya ya Sera hii ya TANZANIA ya viwanda, na mbaya zaidi wasemaji wa jambo hili ni wana siasa wanaoegemea mlengo wao bila kujua kuwa viwanda ni jambo linalohitaji vitendo na kutoa maelekezo ili kila mwananchi ashiriki kikamilifu kufanikisha jambo hili.

Badala ya kuwekeza nguvu kubwa kwenye kilimo, serikali imejikita kwenye mambo yasio na tija kwa walio wengi na kupoteza rasilimali nyingi, hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda kwa maneno maneno tu, bila malighafi hakuna viwanda zitabaki kuwa mbwembwe tu.
 
Hivi kuhalisia tu ndugu
Hivi maziwa makubwa tuliyonayo, tunashindwa kuwapelekea wakulima wetu maji kimwagilizia mazao yao?? Maajabu ya Tanzania hata maji ya kunywa tu ni shida kwa wananchi wkt maziwa makubwa africa tunayo tena maji baridi??
 
wakuu
natoa muendelezo wa andiko langu hili lenye lengo la kufikirishana , ni namna gani wenzetu walipiga hatua , nimeigawanya makala katika awamu nne ili kuwapa wadau kusoma kwa kina kwa mustakabali wa Taifa letu
 
KAULI MBIU YETU YA TANZANIA YA VIWANDA IMEJIFUNZA NINI KUTOKA CHINA.

SEHEMU YA PILI

Nitajaribu kuelezea namna china walipofika kwa Uchambuzi ulioegemea katika uchumi na kuifanya china ifanye maajabu makubwa katika Mapinduzi ya viwanda, Vilevile tutaona namna nchi nyingi zilivyoshindwa katika Mapinduzi ya viwanda japo zilijaribu.

Watu wengi hasa wachumi hufikiria miujiza ya kiuchumi china inafikia Mwisho ,kwa sababu ya uchumi wa china kuporomoka kutoka digit mbili hadi digit moja (7%), hii ni kutokana na soko lake duniani kuporomoka na pesa yake kukumbwa na Ushindani mkubwa lakini lazima tutambue ya kuwa Marekani imewahi kuwa n mkwamo huo na mdodoro wa uchumi kwa kipindi cha miaka 15 huko nyuma kwa vipindi tofauti.

Ukweli Kuhusu Mapinduzi Ya Viwanda China

Miaka 36 , iliyopita pato la mwaka la china lilikuwa ni moja ya tatu(1/3) ya nchi za kusini mwa Jangwa la sahara ikiwemo Tanzania , lakini leo china ni nchi inayoongoza duniani kwa kuzalishwa bidhaa mbalimbali kutokana na Mapinduzi ya viwanda.

1. Inazalisha Asilimia 50 ya bidhaa za viwandani Zinazozalishwa duniani kote,miongoni mwa bidhaa hizo ni vyuma(crude steel)-asilimia 50 ya uzalishaji na usambazaji duniani ,

2. Simenti(asilimia 60 ya uzalishaji wote duniani),

3. Makaa ya mawe( Asilimia 50 ya uzalishaji duniani),

4. Magari(Asilimia 25 ya uzalishaji n usambazaji duniani), na oda za bidhaa mbalimbali toka viwanda vya china zaidi ya Asilimia 150 dhidi ya marekani,

5. Vilevile china ni mzalishaji mkubwa duniani wa meli,treni za mwendo kasi,roboti,ujenzi wa madaraja, barabara kubwa,madawa,mashine mbalimbali ,kompyuta,simu n.k


Mwanzoni mwa Miaka ya 1970, rais wa marekani aitwaye Richard Nixon , alipotembelea china , china ilikuwa inazalisha bidhaa chache sana Kulinganisha na mareknani, lakini ilipofika mwaka 1980 china ilianza kuzalishwa bidhaa nyingi sana na kuanza kuushangaza ulimwengu kwa kupiga hatua kubwa katika Mapinduzi ya viwanda na ilipofika 2010 ikashika namba katika Mapinduzi ya viwanda na kuiacha marekani kushika namba mbili.

Siri Ya China Kufanikiwa

Ni namna gani china imeweza fanikiwa kwa kipindi hicho cha miaka 36?

Jibu ni rahisi tu, china waligundua formula ya siri secret recipe” ya Mapinduzi ya viwanda, swali wanaojiuliza wachumi wengi duniani , pia watu wa kawaida kama mimi na wewe , ni kivipi waligundua mapema namna hiyo wakati nchi za ulaya iliwachukua miaka mingi kufanya Mapinduzi ya viwanda?.

Katika historia Mapinduzi ya viwanda uingereza huchukuliwa kama Mapinduzi makubwa ya viwanda katika historia ya kiuchumi kwa binadamu, japokuwa Mapinduzi katika historia yalianzia katika moto na kilimo,kabla ya Mapinduzi makubwa ya viwanda kufikiwa.
Kuanzia mwaka 1760,maisha ya wananchi nchini uingereza yalianza kubadilika na kuwa maisha mazuri na hii kupelekea kila nchi duniani kujaribu kufanya Mapinduzi ya viwanda kama ilivyokuwa uingereza.

Lakini ni nchi chache sana zilizofanikiwa, mathalani nchi za kaskazini na ulaya magharibi , marekani,japan na nchi baadhi za bara asia ambazo ni Asian tigers (Hongkong,Singapore,Taiwan na Korea kusini) nchi hizi zilifanikiwa sana katika Mapinduzi ya viwanda baada ya uingereza.


Swali , Kwanini ni nchi chache tu zilifanikiwa?

Jibu , kutokana na Nadharia (theory) ya *utaasisi*( institutional) inasema nchi nyingi zilishindwa kwa sababu ya kutokuwa na Taasisi madhubuti za usimamizi mfano uwepo wa demokrasia, institutional theory inasema vikwazo kwa wasomi/wataalam, soko huria, na biashara huria, ilipelekea nchi nyingi kushindwa katika Mapinduzi ya viwanda .

Japo hili haliwezi kuwa la moja kwa moja hasa ,ikizingatiwa ni Nadharia ya kimagharibi, kwani kuna nchi zilizokuwa madhubuti kiuchumi na Mapinduzi ya kiviwanda kabla ya kuingia katika mfumo wa demokrasia na demokrasia imeshindwa kuleta Mapinduzi mapya ya viwanda katika nchi hizo zaidi ya kuporomoka kabisa, mfano ni Afghanistan iliyoingia kwenye wa demokrasia za kimagharibi ,iraq ,Libya n.k

Hivyo basi Nadharia hii ya kimagharibi inashindwa kabisa ,ndio maana china baada ya kugundua siri ya fomula ya Mapinduzi ya viwanda hawakuitumia kabisa.


Historia Ya China Kushindwa Katika Mapinduzi Ya Viwanda Kati ya Mwaka 1860 hadi 1978.

China imejaribu zaidi ya mara nne hadi kuja kufanikiwa katika Mapinduzi ya viwanda kwa zaidi ya miaka 118, kupitia nyakati tofauti tofauti za utawala kabla ya kupata uhuru kamili 1949.

Jaribio la kwanza ,

Ilikuwa kati ya mwaka 1861 na 1911, jaribio hili lilishindwa vibaya kwani baada ya china kushindwa katika vita na uingereza mwaka 1860, katika vita iliyoitwa “Second opium war” baada ya vita hiyo china ililazimishwa kuingizwa katika mikataba inayozibeba nchi za ulaya magharibi katika viwanda vyao.

Ufalme Qing,ambao ndio ulikuwa unatawala china yote na uliokuwa unafanya jitihada za Mapinduzi ya viwanda kupitia uchumi wa kilimo, kujenga meli za kisasa na mfumo wa viwanda ulirudi nyuma kwa kasi kubwa. Miaka 50 baadae juhudi za china kuwa taifa la viwanda zilififia kabisa, na serikali kubaki na madeni makubwa.

Jaribio la pili ,

Mapinduzi ya viwanda nchini china ,Baada ya matumaini kupotea kabisa ,lilizuka vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa,yaliyofatiwa na machafuko ndani ya jamii na Mwisho wa siku kupelekea Mapinduzi yaliyoitwa Xinhai ( Xinhai Revolution) mnamo mwaka 1911.

Hii ilipelekea kuuvunja utawala wa kifalme(Qing Monarchy) na kuanzishwa rasmi Jamhuri ya China(Republic of China),serikali ya kwanza ya china iliyokuwa na mifumo na muundo wa kimagharibi. Jamhuri mpya ya china ilijaribu kurudisha matumaini ya Mapinduzi ya viwanda kwa kukopi mfumo wa marekani wa “Political institution”, kwa Kuingiza mambo ya demokrasia na mgawanyo wa madaraka ( bunge,serikali na mahakama).

Katika ,kipindi hiki Kauli mbiu Maarufu miongoni mwa wachina ilikuwa “ Ni Sayansi na demokrasia pekee vitaisaidia china, wana Mapinduzi wasomi waliamini utawala wa kifalme umeshindwa kufanya Mapinduzi ya viwanda na kuirudisha china nyuma na hii ilitokana na kukosekana demokrasia na ushiriki wa kisiasa( kama Nadharia ya political institution inavyosema).

Japo wana Mapinduzi wasomi ,waliamini katika misingi na nadharia za kimagharibi, toka mwaka 1911 ya Xinhai Revolution, miaka 40 baadae china iliendelea kubaki kuwa nchi maskini duniani.

Hali hii ilipelekea mavuguvugu mbalimbali ,ikiwemo kutaka china huru kutoka koloni la uingereza kupitia japan na ilipofika mwaka 1949, jamhuri ya china ilishindwa vibaya na jeshi la wakulima wakomunist ( Communist peasant army) na kuundwa Jamhuri ya watu wa china .

Jaribio la tatu,

Mapinduzi ya viwanda nchini china ,serikali mpya iliingia na hali ya kusahihisha makosa ya serikali Zilizopita katika Mapinduzi ya viwanda , kipindi hiki serikali ya china iliamua kukopi sera za shirikisho la kisovieti (USSR) kwa kutumia mpango uliojulikana kama “ Central Planning Model” , miaka Takribani 29 ilipita tena ,lakini mpango wa kuifanya china ya viwanda ulishindwa tena.

Mnamo mwaka 1978, china ilibakia katika umaskini mkubwa tu huku pato la taifa likiwa halitofautiani sana na kipindi cha mwaka 1860 wakati wa vita kati ya china na uingereza iliyojulikana kama “second opium war”

Sababu ya china kushindwa katika harakati za Mapinduzi ya viwanda kwa vipindi vitatu tofauti Mfululizo ambavyo vinaleta jumla ya miaka 118. Sababu haikuwa ukosefu mfumo wa soko na mfumo sekta binafsi--- utawala wa Qing(Qing Dynasty) inawezekana ulikuwa na mfumo mzuri wa soko na mfumo mzuri wa sekta binafsi dhidi ya uingereza na nchi nyinginezo za ulaya mnamo karne ya 17 na 18.----Je ilikuwa demokrasia? Serikali ya china ilikuwa na ushirikishwaji mkubwa wa wananchi na hata wanachama wa chama cha kikomunisti waliruhusiwa kuingia serikalini.

Itaendelea...........

Cc:paskal Mayalla,Upepo wa Pesa, Impelle,Ss Jr,Ankozominiotra,Freycloudy,Mafwi Munda,Sodoliki,Duduwasha,SANCTUS ANACLETUS
 
Back
Top Bottom