Wapinzani Msione AIBU kuwapokea wahanga wa Demokrasia kutoka CCM

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2011
Messages
497
Points
195

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2011
497 195
Nianze kwa kutoa pole kwa wanasiasa waliopatwa na janga la kufukuzwa uanachama na chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni kwa madai ya kukisaliti chama chao katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Nawashauri wapinzani Wapokeeni tu wageni hao wakija na ikibidi wafuateni Muwashawishi wajiunge nanyi katika kuendeleza gurudumu la siasa nchini kwasababu siasa hazina rafiki wala adui wa kudumu. Kila mtu anayo haki ya kufanya siasa kupitia chama chochote kile cha Siasa na ndio maana hasa na faida ya siasa za vyama vingi.

Wapokeeni mkijua kwamba hao si wanasiasa [HASHTAG]#Uchwara[/HASHTAG] bali ni "Wahanga wa demokrasia" ya ndani ya chama chao kwahiyo chama kitakachowapokea kijue fika kwamba [HASHTAG]#Wageni[/HASHTAG] hao ni watu ambao wakiwa na misimamo yao ya Kidemokrasia hawaogopi kuiweka hadharani na kuisimamia na ndio maana wamebatizwa "jina baya" kwasababu walionesha wazi wanataka nini hawakutaka kuwa wanafiki hivyo hawatakubali Unafiki wa [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa Chama chochote cha upinzani watakachojiunga nacho.

Bila Shaka kila mtanzania anayefuatilia siasa na timbwili za vyama vya siasa Tanzania ameshuhudia jinsi Msamiati [HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] unavyoendelea kutumika kujenga na kuimarisha [HASHTAG]#Usultani[/HASHTAG] wa viongozi wa Vyama vyetu vya siasa hapa nchini kuanzia chama tawala mpaka vyama vya upinzani .

Nimesema ni muendelezo wa matumizi mabaya ya Msamiati huo [HASHTAG]#Usaliti[/HASHTAG] kwa maana kwamba neno hilo halikuanza kutumika juzi kuwang'oa watu wenye mitazamo na fikra tofauti na matakwa ya viongozi wao wa vyama.

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu neno [HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] maana yake ni tendo la kutoa siri za mtu, kikundi au nchi kwa adui wa mtu, kikundi au nchi hiyo

Ila kwa Mujibu wa [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa vyama vya siasa neno [HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] maana yake ni Mtu au kikundi chochote chenye fikra, mtazamo, maoni au chaguo tofauti na matakwa ya viongozi wa juu kuhusu ya masuala muhimu ya chama husika (hasa kuhusu uchaguzi wa wa ndani ya chama) bila kujali kama fikra, mitazamo, maoni au chaguo husika lina dhamira njema kwa Maslahi mapana ya chama na mustakabali wa kidemokrasia.

[HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] ni neno ambalo limekuwa likitumiwa na [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa vyama vya siasa kufifisha hoja yoyote mbadala inayotolewa na mwanachama / wanachama ikiwa hoja hiyo ina dalili za kugusa Maslahi binafsi ya kiongozi / viongozi waliopo madarakani kwa wakati huo au kuathiri mchakato wa viongozi wanaokuja ikiwa viongozi wanaolengwa ni takwa la viongozi waliopo madarakani.

[HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] Ni Msamiati ambao umekuwa ukitumiwa na [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa vyama vya siasa waliofilisika sera katika kupotosha, kutishia na kudhoofisha kila aina ya fikra tunduizi ambayo haifungamani na matakwa binafsi ya viongozi wa Vyama vya siasa nchini.

[HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] ni Msamiati unaotumiwa sana na [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa vyama kuhalalisha maamuzi batili na adhabu kwa wanachama wenye maono na udhubutu kukosoa, kukemea maovu ya chama na kusimamia wanayoyaamini kidemokrasia.

[HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] umetumiwa na [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa vyama kuwaburuza wanachama na kuua Ujasiri wa wanachama kuhoji uhalali mienendo, haiba na mapendekezo ya viongozi wao hata kama ni ya hovyo kiasi gani kwasababu tu ya kuogopa kubatizwa jina la "Wasaliti"

[HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] umetumika kuwachafua watu waliokuwa na sifa nzuri, maadili mission na vision nzuri kwa vyama vyao na kuwafanya waparaganyike na kusababisha [HASHTAG]#Utitiri[/HASHTAG] wa vyama vya siasa Tanzania kila mmoja akijipa moyo kwamba " Labda changu kitaruhusu na demokrasia zaidi kuliko kile".

Dhana ya [HASHTAG]#USALITI[/HASHTAG] kwa mujibu wa [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa vyama imeviathiri vyama vingi tu ikiwemo CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TLP etc.

Athari za harakati za [HASHTAG]#Masultani[/HASHTAG] wa vyama kuwadhoofisha washindani wao kisiasa kwa kuwavua uongozi, kuwashusha vyeo, viongozi kujiuzuru wenyewe na kufukuza wanachama zimeshatafuna na kutingisha vyama vyote vya siasa nchini.

Shime wanachama wa vyama vyote vya siasa tuamke kupigania demokrasia ndani ya vyama kwanza yaani hakikisha demokrasia ipo ndani ya chama chako ndipo uanze kunyooshea vidole wengine.

Mwanachama hai mwenye akili timamu hawezi kukubali kuwa na Mwenyekiti au Katibu mkuu wa chama wa Milele kwasababu tu anaogopa kupinga ataitwa [HASHTAG]#Msaliti[/HASHTAG]. Usipoweza kuipigania utekelezaji wa Demokrasia ndani ya chama chako wala usiwadanganye watu kwamba utaweza kupigania demokrasia nje ya chama chako.

[HASHTAG]#MABADILIKO[/HASHTAG] ni kuwa tayari kubadilika, kujisahihisha na kujitoa kwenye kundi la watu wanaoburuzwa, watu wanaokubali au kukataa uhalisia wa jambo kwa kupuuza facts na kuegemea kuangalia nani amesema.

UKIYAAMINI HAYA, UJUE [HASHTAG]#UNABURUZWA[/HASHTAG]:

1. Ni wana CCM 16 tu ndio waliokuwa wanamtaka Lowassa na ndio walioimba katika mkutano mkuu wa uteuzi wa mgombea wa CCM "Tunaimaaaani na Lowaaasa!!!!"

2. Ni Zitto Kabwe, Prof. Kitila na Mwigamba tu ndio walikuwa wanataka mabadiliko ya Uongozi wa juu wa Chadema.

3. CCM ina Demokrasia ya hali ya juu kwa kuonesha mkutano wake wa kupitisha mabadiliko ya Katiba live kupitia televisheni kwa kuwahoji wajumbe kwa ujumla bila kutoa nafasi hata moja ya mjumbe kuchangia.

4. Ni Dr. Slaa na Prof. Lipumba tu ndio hawakuridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea wa UKAWA.

5. Ni Mbatia tu ndiye aliyepelekea kuanguka kwa wabunge watatu wa NCCR Mageuzi.

6. Baada ya uchaguzi mkuu 2015 Ukimya wa vijana wengi waliokuwa machachari Bungeni na ndani ya vyama umetokana na vijana hao kukua kiumri na kusongwa na majukumu mengine.

7. Wajumbe waliopunguzwa kwenye vikao vikubwa vya CCM wamefurahishwa sana na uamuzi huo unaolenga kuleta Mageuzi katika chama.

8. Prof. Lipumba haijui katiba ya CUF, wana CUF wengi hawamtaki, [HASHTAG]#Msaliti[/HASHTAG], anabebwa na Msajili na ndio maana anaendelea kuwa Mwenyekiti halali mpaka sasa

[HASHTAG]#TeteaUhuruWaMaoniBilaKujaliChama[/HASHTAG]

mwanahapa.
 

Forum statistics

Threads 1,389,938
Members 528,059
Posts 34,039,154
Top