Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimetafakari sana juu ya hii hali ambayo wanasiasa wa vyama vya upinzani wanakumbana nayo. Hata kabla mwaka haujaisha, yapo matukio kadhaa ya viongozi wa upinzani kujikuta wakivuka mipaka ya siasa zao kutokana ama na kutamka maneno yanayovuka mipaka yao ama wanafanya matendo ambayo yumkini hayaendani na kasi ya Serikali ya Hapa Kazi Tu.
Hadi sasa tumeshuhudia wabunge 8 wa upinzani wakiadhibiwa Bungeni. Viongozi wa CHADEMA na Zitto Kabwe wamehojiwa mara kadhaa na jeshi la polisi na huenda wakafunguliwa mashtaka ikiwa upelelezi wa jeshi la polisi utawakuta na makosa.
Nilichogundua ni kwamba viongozi wa upinzani ama uwezo wao wa kufanya siasa safi ni mdogo na hivyo kujikuta wakiendelea na siasa zao za maji taka ama wanafanya makusudi kwa kuendelea kumchezea Rais ili aache mambo yake ya msingi ya kuwaletea maendeleo wananchi na badala yake akimbizane nao. Ama wanafanya hivyo kwa lengo la kutaka kualikwa Ikulu kunywa juice na kupiga Selfie.
Niwatahadhalishe wapinzani. Hizi ni zama za kuwaletea maendeleo wananchi na si vinginevyo. Rais ameshatamka kuwa hatapenda kuona mtu akikwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, chama kilichopewa ridhaa na wananchi ya kuongoza nchi hii. Maana yake ni kwamba, wale watakaojaribu kukwamisha utekelezaji wa Ilani hiyo, lazima watakiona cha Mtema kuni. Na hii ni dhahiri kabisa na uzuri wa Rais wetu ni kwamba hafichi kitu.
Kwa hali hiyo, kama wapinzani mnaona kuwa hamna uwezo wa kudhibiti midomo yenu na maneno machafu, you better plaster your mouths as you did in the House of Parliament. Vinginevyo hakika ni dhahiri kwamba mtaumia. Siasa za Magufuli ni za Hapa Kazi Tu