Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Wapinzani nawashauri katika mikutano ya kampeni ya chaguzi ndogo za madiwani katika kata 21 kwa upande wa bara na kwa ubunge wa Jimbo la Dimani huko Zanzibar, waelimisha wapiga kura kuhusu siasa za chama tawala.
Ni tabia ya chama tawala kulegeza mambo pale uchaguzi unapokaribia kwa lengo la kuwahadaa wapiga kura jambo ambalo baadhi ya watanzania hawalielewi.
Kwa mfano,hivi sasa kuna huo uchaguzi wa madiwani 22 kwa upande wa Tanzania bara unakuja na huenda hii ndii ikawa sababu ya wamachinga na wachimbaji wa dogo kuruhusiwa kufanya shughuli zao katika maeneo ambayo waliokuwa wameondolewa.
Mbali na wamachinga na wachimbaji wadogo,sitashangaa kipindi hiki kikatumika kutangaza neema kwa wafanyakazi kama vile kulipwa malimbikizo yao, kupandishwa vyeo na hata tukasikia ahadi za watu kuajiriwa,n.k.
Wapinzani ni wajibu wenu kuwaelimisha wapiga kuwa juu ya jambo hili kwa kulifanya kuwa ni moja ya agenda yenu kuu kwenye mikutano ya kampeni itakayoonza tarehe 22 mwezi huu mpaka tarehe 21 mwezi January mwakani.
Baada ya uchaguzi huu wa madiwani kukamilika, nawashauri elimu hii iwe endelevu kwasababu watanzania hawa ni wepesi mno wa kusahau ingawa ni wazuri kwenye kulalamika.
Ni ushauri wa bure hasa katika awamu hii ambapo mwanamchi wa kawaida ni kama amesahaulika huku kipaumbele kikiwa ni ndege na mambo mengine ya aina hiyo..
Kipindi hiki huwezi sikia zile kauli kuwa wanaolalamika ni wapiga dili,n.k bali ni kipindi cha lugha tamu tamu za kutia matumaini ila uchaguzi ukipita tu lugha hizi zitarejea kwa kasi hivyo ni wajibu wenu wapinzani kutoa elimu na msisitizo kwa wapiga kura.
Msishangae pia hata kikao cha CCM kinachotarajiwa kuketi leo hii kikaja na maazimio au kauli tamu kuhusu mwananchi kumbe lengo ni huu uchaguzi mdogo tu na si vinginevyo.
Miko itakayoshiriki kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani imetajwa katika hii post hapa chini ikiwemo Mwanza,Shinyanga na Mara.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani kuanza December 22