Wapinzani mko serious? Marekebisho ya Katiba kuruhusu Tume Huru yako wapi?

washwa washwa

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
1,613
717
Wakuu kuna jambo ambalo hata sielewi kama kweli viongozi wa vyama vya upinzani wako serious na wana nia ya kushinda kiti cha urais.

Ni muda muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuhusu kukosekana kwa Tume Huru ya Uchaguzi, Mgombea binafsi, Matokeo ya Rais kuhojiwa Mahakamani na iliafikiwa hata kwenye kwenye kikao cha TCD na Mh Rais kuwa marekebisho ya Katiba yafanywe kabla ya uchaguzi ili ku accomodate hayo mambo.

Sasa nashangaa bunge linamaliza muda wake na wala sioni hata wapinzani waki preshalaizi kupatikana kwa marekebisho hayo muhimu ya Katiba.

Huu ni mchezo wa kuigiza au ni kitu gani? Kama wanaamini tume si huru wanategemea safari hii ufanyike muujiza iwe huru gafla?
 
Wamekubali kushindwa kwa goli la mkono! Refa yuleyule aliyechakachua matokeo 2010 ndiye huyuhuyu wa mechi hii ya 2015. Sijui wanafikiri kupata ushindi kwa njia gani. Sheria inayosema kuwa uamuzi wa refa ndio wa mwisho ndiyo hii inayosimamia mechi hii. Atakayetangazwa natume ndiye raisi hata kama hakushinda kwa kura! Du!!!
 
Nafikiri nia yao ni kuongeza wabunge wawe wengi zaidi.....na sio urais......................
 
Wamekubali kushindwa kwa goli la mkono! Refa yuleyule aliyechakachua matokeo 2010 ndiye huyuhuyu wa mechi hii ya 2015. Sijui wanafikiri kupata ushindi kwa njia gani. Sheria inayosema kuwa uamuzi wa refa ndio wa mwisho ndiyo hii inayosimamia mechi hii. Atakayetangazwa natume ndiye raisi hata kama hakushinda kwa kura! Du!!!
Mimi naanza kuhisi hawa jamaa si wapinzani wa kweli, wanapiga tu dili na kwenye hilo dili bosi wao ni CCM. Sioni ni kwa jinsi gani opposition wanaweza kushinda kama Tume Huru ya Uchaguzi haipo, unless People's Power itumike kwa maana ya kuingia mtaani.
 
Wakuu kuna jambo ambalo hata sielewi kama kweli viongozi wa vyama vya upinzani wako serious na wana nia ya kushinda kiti cha urais.

Ni muda muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuhusu kukosekana kwa Tume Huru ya Uchaguzi, Mgombea binafsi, Matokeo ya Rais kuhojiwa Mahakamani na iliafikiwa hata kwenye kwenye kikao cha TCD na Mh Rais kuwa marekebisho ya Katiba yafanywe kabla ya uchaguzi ili ku accomodate hayo mambo.

Sasa nashangaa bunge linamaliza muda wake na wala sioni hata wapinzani waki preshalaizi kupatikana kwa marekebisho hayo muhimu ya Katiba.

Huu ni mchezo wa kuigiza au ni kitu gani? Kama wanaamini tume si huru wanategemea safari hii ufanyike muujiza iwe huru gafla?
Wewe umechukua hatua gani au kila kitu umeweka kwenye mkoba uliowakabidhi!Je huo muswada ww unakufaa?Kwanini usiongee na mpeleka hoja ambaye ni CCM badala yake unahangaika na mpinga hoja?Ni lipi rahisi ktk kumaliza shauri liloko mbele ya sheria ni kuongea na mshitaki au mshitakiwa?Naomba nikurejeshe kwa mtu aliyeitwa Gen. Moshe Dayan...If you want peace talk to your enemy ,not your friend.Nadhani hapo utanilewa.

mkuu hili ni swala nyeti mno bila tume huru UKAWA hawawezi kushinda uchaguzi mpo humu tupeni jawabu
 
Wakuu kuna jambo ambalo hata sielewi kama kweli viongozi wa vyama vya upinzani wako serious na wana nia ya kushinda kiti cha urais.

Ni muda muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuhusu kukosekana kwa Tume Huru ya Uchaguzi, Mgombea binafsi, Matokeo ya Rais kuhojiwa Mahakamani na iliafikiwa hata kwenye kwenye kikao cha TCD na Mh Rais kuwa marekebisho ya Katiba yafanywe kabla ya uchaguzi ili ku accomodate hayo mambo.

Sasa nashangaa bunge linamaliza muda wake na wala sioni hata wapinzani waki preshalaizi kupatikana kwa marekebisho hayo muhimu ya Katiba.

Huu ni mchezo wa kuigiza au ni kitu gani? Kama wanaamini tume si huru wanategemea safari hii ufanyike muujiza iwe huru gafla?
Wafanye nini kuwezesha marekebisho hayo kufanyika? Makubaliano ilikuwa serikali ilete mswada wa mabadiliko hayo na haijafanya. Kwa mfumo uliopo haitakaa lifanyike hilo, hakuna serikali yoyote iliyoko madarakani italeta kitu ambacho inajua kitaiondoa madarakani! Kama unaona hayo mabadiliko ni mhimu, piga kura ya kuiondoa serikali ukiamini kuwa itakayokuja italeta mabadiliko hayo. By the way unajua hilo la mgombea binafsi mpaka limefika Mahakama ya Afrika ambayo ilitoa hukumu ya kuilazimisha serikali kuliruhusu. Ebu angalia jinsi lilivyowekwa ndani ya Katiba Inayopendekezwa, ni kama halikuruhusiwa! Sielewi unapowalaumu wapinzani unataka wafanyeje...lete mabadiliko wewe na si mwingine.
 
Mimi naanza kuhisi hawa jamaa si wapinzani wa kweli, wanapiga tu dili na kwenye hilo dili bosi wao ni CCM. Sioni ni kwa jinsi gani opposition wanaweza kushinda kama Tume Huru ya Uchaguzi haipo, unless People's Power itumike kwa maana ya kuingia mtaani.

Hamkumsikia Mnyika juzi akiliongelea hilo siku ya kwanza anaomba muongozo? Alisema shughuli za Bunge zisimame na wajadili jambo la dharula ambalo ni mwenendo mbovu wa uandikishaji na pia akalisemea hilo la Tume Huru ya Uchaguzi kua ndio vilipaswa viletwe Bungeni kwa hati ya dharula, Majibu aliyotoa huyo msimbe wenu nadhani kila mtu ni shahidi.
 
Sikubahatika kuona/kusikia hiyo habari. Kwani wapinzani hawakuweza kupeleka kama hoja binafsi? Binafsi napenda mabadiliko na nishajiandikisha kwa ajili ya kuwaondoa CCM lakini kila nikitafakari naona mazingira ya kuiondoa CCM kwa sanduku la kura haiwezekani kama hayo mabadiliko hayatafanyika
 
Sikubahatika kuona/kusikia hiyo habari. Kwani wapinzani hawakuweza kupeleka kama hoja binafsi? Binafsi napenda mabadiliko na nishajiandikisha kwa ajili ya kuwaondoa CCM lakini kila nikitafakari naona mazingira ya kuiondoa CCM kwa sasa haiwekani ikawa sanduku la kura kama hayo mabadiliko hayatafanyika

Kwa kiasi flani nimefanikiwa kulitazama Bunge la Bajeti kila nilipokua nikipata nafasi, Wabunge wa upinzani hasa Mnyika na Silinde walijitahidi sana kuja na hoja binafsi ambazo zina manufaa kwa Jamii nzima ila Ubabe wa Spika ndio unawakatisha tamaa kwani mtu hajamaliza hata kutoa maelezo yake Spika anamkatisha na kutopokea hoja hizo, mfano mzuri ni kwenye miswada iliyokua ikijadiliwa Tundu Lisu alikua anatoa mapendekezo mazuri sana ambayo hata kwa mtu ambae si majuzi wa Sheria unaelewa na kuona mantiki katika hoja anazotoa ila Spika na watu wake(Mawaziri husika na Wabunge wa CCM) wanapinga kwakua tu hoja au mapendekezo yametolewa na mpinzani, rejea mswada wa Cyber crime ambao ulipelekea Bunge kufungwa usiku, Nyoka mwenye makengeza alichangia hoja ambayo ilikua inakubaliana na hoja ya Lisu laki AG aliposimama aliushangaza ulimwengu pale aliposema nakubaliana na Nyoka mwenye makengeza lakini sikubaliani na Lisu, pia mara zote Mnyika na Lisu wanaamua kukubali yaishe ila wanatoa kauli moja tu ambayo ni kua mnapinga kwa wingi wenu lakini hansard zitaweka record na wananchi ndio watakua waamuzi wa mwisho siku itakapowadia ya kufanya maamuzi.
 
Huyu Spika ni hovyo na anajijua ni hovyo ndo maana sijawahi kuona hata mara moja akihojiwa na media. Nafkiri huwa anaingia mitini kila anapoitwa!
 
Back
Top Bottom