kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,098
- 17,447
Muungano wa Tanzania na Zanzibar ni kitu nyeti cha thamani kubwa sana kinacholindwa kwa gharama yoyote, yaani kwa gharama yoyote ile.
Na watu walioapa kuulinda Muungano kwa gharama yoyote wapo na ni wengi sana pia. Hivyo, hakuna Rais ambae yuko tayari kuona Muungano unamfia mikononi mwake; kila Rais atafanya kila kitu alicho nacho kuhakikisha kuwa Muungano huu hauvunjikii mikoni mwake.
Vyama vya upinzani lazima waimbe kudumisha Muungano kama wakitaka safari yao ya kwenda Ikulu iwe nyepesi kidogo. Kule Marekani hata wao kuna watu hawautaki muungano wao na kuna wengine wanataka muungano wao ufanyiwe marekebisho lakini pamoja na ukweli huu hakuna chama cha siasa kitahubiri japo kwa bahati mbaya habari kuhusu muungano wao.
Vyama vyetu vya upinzani agenda yao kuu wakati wa kampeni ni kuhusu Muungano, Tanganyika, Zanzibar kamili, serikali tatu, muungano wa mkataba, nk. Hoja zao hizi zinachochea wasiwasi kuhusu uhai wa muungano. Hivyo, hakuna Rais aliyeko madarakani atalikubali hilo litokee yeye akiwa Ikulu.
Hata process ya kuandika Katiba mpya inasuasua kwasababu kutekelezwa kwake kwa kuhofia hoja za muungano kwenye uandishi wa katiba mpya.
Tukubaliane tu kwamba wazee wetu walifanya kwa niaba yetu ili tusonge mbele. Muungano huu umegharimu watu wengi hadi kuwa hivi ulivyo sasa, wewe huwezi kuuvunja kihuni tu kwa neno moja.