Wapinzani amkeni sasa

Wapinzani amkeni sasa

Joined
Apr 15, 2021
Posts
81
Reaction score
124
Tanzania itajengwa na wazalendo,

Natumaini ndugu zangu mnaendelea vema na majukumu yenu.

Kwa Sasa Vyama vya upinzani Tz inabidi watumie huu muda kujikita ktk mizizi kabisa kwa wananchi.

CCM Sasa wapo ktk malumbano na Tahamaki kubwa hasa baada ya Kifo Cha JPM. Hii Ni nafasi adhimu Sasa, kuimarisha upinzani na kuandaa ajenda muhimu kwa lengo la kuwaeleza wananchi.

Ripoti ya CAG imeivua nguo Serikali Yote ya CCM na ujanja wao wote wa kuficha maovu Yao kwa miaka 6,

Nini chakufanya upinzani?
1) Mdai tume huru ya taifa ya uchaguzi kwa kushirikisha makundi mbalimbali mfano wanaharati, mashirika na wananchi

Hii itasaidia sana kujiwekea mazingira mazuri ktk uchaguzi ujao

2) Kudai katiba mpya Ile ya wananchi

3) Kuandaa viongozi Imara na watu mathubuti kwa ajili ya kugombea 2025, watu hao wapate elimu na uelewa wa kutosha ili kusaidia kuuza Sera na malengo ya chama kwa wananchi.

4) Kwa Sasa wajikite kutafuta wingi wa nafasi bungeni, kwani wingi bungeni utasaidia Sana kubadili mifumo na sheria kandamizi nchini, hii itawezekana km mapendekezo hapo juu[emoji115] yatafanyiwa kazi!!

5) kuwekeza ktk urais Ni kujidanganya, vigumu Sana kupata urais bila kutengeneza uimara wa mfumo hasa ngazi ya ubunge, mjikite ktk mikakati ya ubunge zaidi.

6) CCM ishafeli kitambo kuongoza nchi, vyombo vya Dola ndo tegemeo lao!

Mwisho, niwaombe watanzania wenzangu tuwe wazalendo kwa taifa letu!
 
Hapana mkuu, Ila nguvu kubwa Sana I inatumika kuficha mambo.

Rejea kisa Cha Prof Assad kuvuliwa wadhifa wake.
Hahahahaaaa, poleni sana
Linganisha kiwango cha hati chafu 2015 na 2020 au % ya fedha zilizotumika vibaya, value for money, muda kuakamilika miradi au ongezeko la bajeti ya miradi .
Ni kwamba watu wameamua kukuza issues. Mf. Wanahoji wizi wa Tanzanitebaada ya ukuta na kusahau kuwa tumeongeza mapato kutoka bln 30 kwa robo mwaka mpaka bln 700 kwa robo mwaka
 
Wapinzani waliambiwa na mama wasahau kwa sasa kuhusu katiba mpya nao wakashangilia na kusema mama kaanza vizuri.
 
1618700303874.png
 
Ripoti ya CAG imeivua nguo Serikali Yote ya CCM na ujanja wao wote wa kuficha maovu Yao kwa miaka 6,
Kwani CAG himself yeye ni Chama gani vile 🤔 au bado haja-declare interest 😆 By the way, CAG huyu huyu chini ya serikali tawala ya CCM ndiye huyo huyo wa kuivua nguo serikali ya CCM CCM 😂😂😂
 
Kwani CAG himself yeye ni Chama gani vile [emoji848] au bado haja-declare interest [emoji38] By the way, CAG huyu huyu chini ya serikali tawala ya CCM ndiye huyo huyo wa kuivua nguo serikali ya CCM CCM [emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo kipindi cha mwendazake ilikuwa one man show,
 
Back
Top Bottom