Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,439
- 6,692
Wanachama wa vyama vya upinzani 200 wa wilaya ya Tunduru akiwemo diwani wa kata ya Mchoteka kupitia tiketi ya Chama Cha Act Wazalendo Seif Dauda, katibu wa wilaya ya Tunduru wa Chama Cha Act Wazalendo Said Mponda, wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi 2/4/2025 baada ya kumkabidhi kadi za uwanachama wa vyama walivyotoka katibu wa CCM, Balozi Dkt Emanuel Nchimbi akiwa katika ziara yake siku 5 katika mkoa wa Ruvuma.
Wakieleza sababu ya kuhama vyama vyao diwani pamoja na katibu wa Chama Cha Act Wazalendo wamesema wamevutiwa na utekekezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika wilaya ya Tunduru ambapo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhuu Hassan kwa kuleta miradi mikubwa katika kata ya Mchoteka na wilaya ya Tunduru kwa ujumla.