Wapinga nauli ya treni ya 700 na 800/=

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Wapinga nauli ya treni ya 700/- Dar: WADAU wa usafiri wa Reli nchini wamepinga mapendekezo ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) la kutaka nauli ya usafiri wa umma wa treni jijini Dar es Salaam kuwa Sh 700 na 800.
 
bora tuendelee kubanana kwenye dala dala.hizo treni wapande vibopa wa wizarani ili tupunguze gharama za mafuta ya VX
 
Hata 400 sipandi waweke 200 ndio reasonable kama hawawezi wayapeleka mabehewa wakafugie kuku au panya....
 
Mimi nimesikia ni 400 kwa TRL na 500 kwa TAZARA bila kujali umbali wa safari, na usafiri unaanza rasmi jumatatu ijayo. Vituo vya kukatisha tiketi viko zaidi ya elfu mbili.
 
Unajua ili tuweze kujua kama bei ni kubwa au ndogo inabidi tujiulize yafuatayo:-
  • Gharama za uendeshaji
  • Je usafiri mbadala ni kiasi gani ?
  • Je kodi zetu zitumike ku-subsidize huu usafiri ?
  • Issue ya huu usafiri ni kusaidia wananchi kupunguza gharama au ni kupunguza msongamano ?
 
Unajua ili tuweze kujua kama bei ni kubwa au ndogo inabidi tujiulize yafuatayo:-
  • Gharama za uendeshaji
  • Je usafiri mbadala ni kiasi gani ?
  • Je kodi zetu zitumike ku-subsidize huu usafiri ?
  • Issue ya huu usafiri ni kusaidia wananchi kupunguza gharama au ni kupunguza msongamano ?
Na je kipato cha mwananchi wa chini ni kiasi gani?
 
waeleze sababu makini za gharama ya nauli kama hiyo rasivyo waache maana hali za wananchi wenyewe mbaya. kwa walivyosema hivyo hata watu wa daladala wataongeza nauli.
 
Hivi makampuni ya serikali yakifanya hivyo kutakuwa na uhalali gani wa kuwakatalia wenye daladala nao kupandisha nauli? Nijuavyo mimi duniani kote usafiri wa treni pengine ndio usafiri rahisi zaidi na kimbilio la maskini lakini hapa kwetu inakuwa kinyume! Nilitegemea kutoka Ubungo hadi Feri isingezidi sh. 150/= kwa wakubwa na 50/= watoto na wanafunzi. Naona wameanza na mguu mbaya na amini usiamini hii kitu itavuruga kabisa usafiri jijini kwani wenye daladala nao watakuja juu na migomo lukuki.
 
mleta mada tufafanulie, ni nauli ya kwenda na kurudi au? Itakuwa kwa umbali gani?
 
bora tuendelee kubanana kwenye dala dala.hizo treni wapande vibopa wa wizarani ili tupunguze gharama za mafuta ya VX

:biggrin1::biggrin1: naona umeongea kwa jazba hapo...hawa nawashangaa kwanza hizo route walizoziweka hao watu wata afford vipi sh 700? wamechemsha
 
Bila kuambiwa umbali ni ngumu kusema kama nauli ni kubwa ama la...naona tumeshakuwa wapinzani wa kila kitu...How can we judge fares without references to distances?
 
The whole idea of providing transport is that it should be affordable ; otherwise there will be no return on your investment if people do not use your mode because they cannot afford the fare!!
 
Maisha ya mwananchi wa kawaida ni magumu sana nilitegemea usafiri wa umma ungetoa ahueni, kumbe nao ni mzigo mpya. Nauli hiyo ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom