Erdoğan ashinikiza Uturuki kuingizwa Umoja wa Ulaya(EU) kupitia NATO!

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,277
Katika kile kinachoonekana Uturuki kutamani sana na kuumizwa sana kwa kuwekwa mkwamo kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Rais wa nchi hiyo Erdoğan sasa ameamua kutumia turufu yake dhidi ya Sweden kujiunga NATO.

Erdoğan anasema wataondoa turufu yao dhidi ya Sweden kujiunga NATO pale ambapo mazungumzo ya Uturuki kujiunga EU yatakaporejeshwa na mchakato huo utakapokwamulia. Chancellor wa Ujerumani, Scholz amepinga vikali uamuzi huo akisema hayo ni mambo mawili tofauti kabisa.

Sweden ilishatimiza matakwa yote ya Uturuki ikuwemo kwarejesha Uturuki baadhi ya wapinzani wa Erdoğan waliokuwa uhamishoni nchini humo kabla ya madai mapya ya Erdoğan.

Marafiki wa Putin akili zao zina mfanano kwa kiasi kikubwa sana.

Wataalamu wa Geopolitics, Hivi NATO inaweza kuichoka Uturuki ikamfurusha kutoka umoja huo?
 
... hawa waturuki watu wa dini wanalilia nini kujiunga na maupinde? Wanatia aibu sometimes.
Screenshot_20230710-185624_1.png

Hili ndio jeshi la Nato ukitoa Marekani, Uturuki anafuatia, ni Uturuki ambaye yupo Syria, Iraq, Katoa Anga lake kwa operation ya Usa Iraq, Apeleke misaada ukraine etc.

Kifupi Mataifa mengi ya Ulaya Yanamnyonya Uturuki Nato, kwanini na yeye asiweke vigezo vyake.

Sababu nyie mpo Brainwashed na mioyo yenu mnatamani nchi zote ziwe vibaraka wa magharibi haimaanishi Uturuki nayo ipo hivyo, wana haki na wao kuangalia maslahi ya Taifa lao.
 
Kwanini Erdagon asijiunge na nchi za kiarabu wakati tamaduni za kituruki hata Imani zinafanana na waarabu;Waturuki na wazungu ni wapi na wapi?Bora hata Israeli ingeomba kujiunga na EU kuliko Turkey!
Uturuki na Iran sio Waarabu kila siku humu watu wanarekebishwa na hawafanani Culture per se, Sababu ni waisilamu haimaanishi wana Culture ile ile na waarabu.

Uturuki ni Race nyengine, wanafanana na Wagiriki, Armenia, Azerbaijan etc

Pia Ukitoa London na Paris, Instabul ni Mji wa tatu Ulaya ambao Wazungu wengi wanatembelea, so ina Muunganiko mkubwa na Ulaya kuliko Nchi za Ghuba.
 
View attachment 2684064
Hili ndio jeshi la Nato ukitoa Marekani, Uturuki anafuatia, ni Uturuki ambaye yupo Syria, Iraq, Katoa Anga lake kwa operation ya Usa Iraq, Apeleke misaada ukraine etc...
Kuwa na jeshi kubwa sio ishu, nusu ya bajeti ya NATO inachangiwa na US, Ujerumani na Uingereza.

Vita vya Uturuki Syria sio vya NATO vina mahusiano zaidi na siasa za ndani za Wakurdi ambao wamekuwa wakitaka kujitenga kutoka Uturuki.
 
Ingekua wewe Raisi wa Tanzania, Uingereza Achangie Budget ya Jeshi then upeleke vijana wako wakafe vitani ungekubali?

Hakuna kiasi cha hela kinachonunua Uhai wa mtu, Mchango wa Binadamu wa Uturuki ni mkubwa kuliko mchango wa pesa.

Na huko Syria ndio Uturuki ana anachotafuta ila interest zao zina Align na hao wamagharibi.
 
Kuna proRussia wanasema Urusi inapigana na mataifa 30 au NATO kisa tu Marekani na baadhi ya mataifa ya Ulaya yanapeleka silaha na fedha Ukraine wakati wanaokufa ni Wa-Ukraine!
 
Uturuki na Iran sio Waarabu kila siku humu watu wanarekebishwa na hawafanani Culture per se, Sababu ni waisilamu haimaanishi wana Culture ile ile na waarabu.

Uturuki ni Race nyengine, wanafanana na Wagiriki, Armenia, Azerbaijan etc

Pia Ukitoa London na Paris, Instabul ni Mji wa tatu Ulaya ambao Wazungu wengi wanatembelea, so ina Muunganiko mkubwa na Ulaya kuliko Nchi za Ghuba.
Hili ndio tatizo nilishindwa TU kuweka wazi moja kwa Moja!
 
Katika kile kinachoonekana Uturuki kutamani sana na kuumizwa sana kwa kuwekwa mkwamo kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Rais wa nchi hiyo Erdoğan sasa ameamua kutumia turufu yake dhidi ya Sweden kujiunga NATO.

Erdoğan anasema wataondoa turufu yao dhidi ya Sweden kujiunga NATO pale ambapo mazungumzo ya Uturuki kujiunga EU yatakaporejeshwa na mchakato huo utakapokwamulia. Chancellor wa Ujerumani, Scholz amepinga vikali uamuzi huo akisema hayo ni mambo mawili tofauti kabisa.

Sweden ilishatimiza matakwa yote ya Uturuki ikuwemo kwarejesha Uturuki baadhi ya wapinzani wa Erdoğan waliokuwa uhamishoni nchini humo kabla ya madai mapya ya Erdoğan.

Marafiki wa Putin akili zao zina mfanano kwa kiasi kikubwa sana.
Wataalamu wa Geopolitics, Hivi NATO inaweza kuichoka Uturuki ikamfurusha kutoka umoja huo?
NATO haito mchoka Mturuki kwa sababu jeshi kubwa la Nato ni la Marekani linalo fuatia ni jeshi la Uturuki nalo ni kubwa katika huo Umoja wa NATO.Sio rahisi kwa NATO kumfukuza uanachama Uturuki. NATO inategemea Jeshi toka kwa Uturuki.
 
NATO haito mchoka Mturuki kw asababu jeshi kubw ala Nato ni la Marekani linalofuatia ni jeshi la Uturuki nalo ni kubw akatika huo Umoja wa NATO.Sio rahisi kwa NATO kumfukuza uanachama Uturuki. NATO inategemea Jeshi toka kwa Uturuki.
Uturuki inaweza kuwa na wanajeshi wengi lakini haimaanishi kwamba lazima wachangie wanajeshi wengi kwenye missions za NATO, mfano Afghanistan Ujerumani imekuwa ya pili kwa kuwa na wanajeshi wengi baada ya Marekani.
 
Kuna proRussia wanasema Urusi inapigana na mataifa 30 au NATO kisa tu Marekani na baadhi ya mataifa ya Ulaya yanapeleka silaha na fedha Ukraine wakati wanaokufa ni Wa-Ukraine!
West wanapeleka silaha na watu sema wanakwenda tu as Volunteer sio official, pia sioni ufananisho hapa, Uturuki anatetea maslahi binafsi , kukiwa na Vita Mturuki anakua Ulaya ila Kwenye Uchumi Ghafla sio Ulaya huoni kwamba wanataka Tu kumtumia Uturuki kwa Maslahi yao Binafsi?
 
View attachment 2684064
Hili ndio jeshi la Nato ukitoa Marekani, Uturuki anafuatia, ni Uturuki ambaye yupo Syria, Iraq, Katoa Anga lake kwa operation ya Usa Iraq, Apeleke misaada ukraine etc.

Kifupi Mataifa mengi ya Ulaya Yanamnyonya Uturuki Nato, kwanini na yeye asiweke vigezo vyake.

Sababu nyie mpo Brainwashed na mioyo yenu mnatamani nchi zote ziwe vibaraka wa magharibi haimaanishi Uturuki nayo ipo hivyo, wana haki na wao kuangalia maslahi ya Taifa lao.
... mada hapa ni Uturuki kuomba kujiunga EU ambao wanahisiwa ku-support upinde! I thought Uturuki ingekuwa ya kwanza kujitenga vilivyo na nchi za aina hiyo!
 
Si kila Nchi ya EU wanasuport Upinde, Ulaya na West ni wawili tofauti, kuna Nchi Nyingi za Ulaya kati/Mashariki wapo Against.

Mfano Hungary tumeona jinsi wanavyopinga Ushoga.
 
... Hungary ni kisungura tu mbele ya tembo EU; hana influence yoyote ya maana. Soma EU 2020 - 2025 Strategy kuhusu hayo mambo. Uturuki anaona kabisa pale ni pachafu halafu anapakimbilia, tumweleweje?

LGBTIQ Equality Strategy 2020-2025
 
Nimesoma link yako sijaona mahala ambapo Member wanalazimisha na Hio link pia Research inaonesha LGBT Discrimination imeongezeka toka asilimia 37 mwaka 2012 mpaka 43 mwaka 2019.
 
Kwa hiyo unakubaliana na EU kwa kuwa hawalazimishi yeyote kufuata hayo mambo?

Au ni kwa sababu unajaribu kutafuta justification ya Uturuki kujiunga EU? Kesho huyo huyo Erdogan akiituhumu EU kwa ushoga hutabadili kauli?
 
Siasa ngumu sana kuielewa kama hufuatilii nchi na nchi

Turkey walikubaliwa kujiunga NATO kwanini miaka ile ya nyuma?
Kuna nchi hazikuwemo kwa sababu ya udikteta na sio uzkristo au uzungu

Turkey ni rafiki mkubwa wa kwa sababu ya ulinzi wa Dardanelles
Yaani Biden yuko tayari kumpa F-16 nyingi Turkey ingawa anapewa silaha kali na Russia

Hizi sanctions ni blah blah tu alipochukua S-400

Hapa wao ndio wanamuhitaji zaidi kwa jiografia ilivyo
Wanaowaza udini wakasome Dunia inavyokwenda
Wengine tulipitia kwa vitendo na ni hobby yetu na vita nimeiona na kujiunga
 
Kwa hiyo unakubaliana na EU kwa kuwa hawalazimishi yeyote kufuata hayo mambo?

Au ni kwa sababu unajaribu kutafuta justification ya Uturuki kujiunga EU? Kesho huyo huyo Erdogan akiituhumu EU kwa ushoga hutabadili kauli?
Mostly mkuu hizi ni Tuhuma za West, Yes West wana Nguvu EU ila haimaanishi Member wote wa EU wanakubaliana na hilo jambo. Nimekupa Mfano Mzuri tu wa Hungary, na sio Wao tu hata Poland na Nchi nyengine za Mashariki zaidi Ulaya. Hii ramani ya Ulaya ikionesha kukubaliwa kwa Ushoga

230509_IG_AI_RainbowMap2023_EN-xs.png

Jinsi inavyokua Blue ndio jinsi inavykubalika na jinsi Ilivyo red ndio jinsi wanavyokataa. Hapo unaona Nchi za EU kama Romania, Poland, Hungary etc wote wanalimit hizo mambo
 
Back
Top Bottom