Chilisosi
JF-Expert Member
- Oct 19, 2008
- 3,051
- 747
WAPIGA KURA JIMBO LA IRINGA MJINI WAMSHANGAA MBUNGE WAO
WAKATI mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (pichani )na viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) leo walijitolea kufanya usafi katika eneo la kitanzani mjini Iringa kama njia ya kuhamasisha usafi, wapiga kura wa jimbo hilo wameonyesha kutofautiana na uamuzi huo wa mbunge kufanya usafi huku baadhi yao wakidai kuwa jimbo hilo limemsinda kuongoza na ndio sababu ya uchafu kuzagaa kila kona ya mji .
" Mbunge wetu leo anajitolea kufanya usafi siku zote alikuwa wapi hadi uchafu unazangaa kiasi hiki mitaani .....tunamtaka Msigwa kufanya kazi kama wabunge wengine na kuachana na siasa za kuunga unga na kutafuta umaarufu kwa watu "
Wakizungumza l;eo kwa nyakati tofauti wananchi wa jimbo la Iringa mjini walisema kuwa mji wa Iringa umeendelea kuzidiwa na uchafu na kuwa mbali ya mbunge kujitolea kufanya usafi pamoja na wanachama wa Chadema ila bado hatua hiyo haiwezi kutatua tatizo la uchafu na badala yake uchafu wa Manispaa ya Iringa utaendelea kuwepo .
Juma Husein mkazi wa Kitanzini katika Manispaa ya Iringa alisema kuwa mbunge wao anatafuta umaarufu wa kisiasa na kusahau kuwa yeye ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini na mwakilishi wa wananchi hao bungeni hivyo alipaswa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa uchafu katika jimbo lake badala ya kufanya usafi kwa misingi ya kisiasa huku akitambua kufanya hivyo ni kujichongea mwenyewe kwa wananchi kuwa kumbe ameonyesha kushindwa kuongoza jimbo hilo na ndio sababu ya taka kuzagaa kila kona.
Husein alisema ni vema mbunge Msigwa kwenda kujifunza katika jimbo la Moshi mjini ambalo pia linaongozwa na mbunge wa Chadema na kuona kama mbunge huyo ametumia mbinu kama hiyo kusafisha mji ama kuna mbinu nyingine inatumika badala ya hiyo ya zima moto inayotumiwa na mbunge Msigwa sasa ya kukodi magari ya usafi.
Aidha alisema kuwa kwa kuwa Manispaa ya Iringa inakabiliwa na tatizo la magari ya kusomba takataka na uhaba wa vyombo vya kuhifadhia takataka mbunge Msigwa kwa kutumia mfuko wa jimbo alipaswa kuanza kushughulikia kero hiyo badala ya kukodi magari kwa siku moja ili kutaka kuonekana kuwa ni mchapakazi wakati siku zote yupo mjini Iringa na uchafu huo upo.
Kwa upande wake mbunge Msigwa alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na utaratibu huo alisema kuwa kazi ya mfuko wa jimbo si kwa ajili ya kusafisha mji na kuwa yeye ataendelea kusafisha mji kwa muda wa siku mbili hizi kabla ya kwenda bungeni .
Msigwa alisema kuwa kupitia ofisi yake tayari amekwisha changisha kiasi cha shilingi milioni 16 kwa ajili ya kununua gari ya kubeba taka katika Manispaa ya Iringa ili kupunguza tatizo la uchafu katika mji huo.
Afisa afya wa Manispaa ya Iringa Severin Tarimo alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi ili kueleza mikakati ya Manispaa ya Iringa juu ya hali ya uchafu inayoendelea kuukumba mji huo alidai kuwa kwa sasa yupo likizo hivyo anayeweza kujibia hilo ni yule aliyemwachia ofisi.
"Nazungumza na nani ....sasa mimi nipo likizo bwana naomba uongee na mtu mwingine" alikata simu
MWISHO
Source FRANCIS GODWIN BLOG
My take,
Msigwa kuna mtu anaitwa Chilisosi anakuja hapo hivyo jiandae vyema
CHILISOSI FOR IRINGA 2015