GE2025 Wapiga kura ambao wamejiandikisha lakini majina yao hukosekana kwenye orodha ya wapiga kura, ni mkakati wa kuwazuia wasichague viongozi wanaowataka?

GE2025 Wapiga kura ambao wamejiandikisha lakini majina yao hukosekana kwenye orodha ya wapiga kura, ni mkakati wa kuwazuia wasichague viongozi wanaowataka?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Wakuu!

Nimekuwa nikisikia kuhusu dhana hii inayotokana na changamoto ambayo imekuwa ikijitokeza hasa katika Uchaguzi, ambapo baadhi ya Wananchi wamekuwa wakikumbwa na kero ya kutoona majina yao katika orodha ya Wapiga Kura na kuwakwamisha Kupiga Kura.

Hali hii iliwafanya baadhi kususia uchaguzi na kuondoka, jambo lililowanyima fursa ya Haki yao ya Kupiga Kura. Nakumbuka ilitokea mwaka 2024 kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo wakati wa zoezi la ukaguzi na uhakiki wa orodha ya majina ya Wapiga Kura, yaliyobandikwa katika sehemu ya matangazo ya Uchaguzi kuliibua sintofahamu kwa baadhi ya Wananchi kutoona majina yao.

Sasa Uchaguzi Mkuu unakuja Oktoba 2025, na kuna Watu husema kuwa kutokuwepo majina yao kwenye orodha ya majina ya Wapiga Kura ni mkakati wa kuwafanya wasichague viongozi wanaowataka na kuwarahisishia wengine kushinda.
 
MWIZI NI MWIZI TU. KUNA TOFAUTI NDOGO SANA KATI YA KIBAKA WA MANZESE NA YULE WA BOT?
CCM NI WEZI WA KURA WANACHOKIFANYA NI KUBADILISHA MBINU TU
NO REFORMS NO ELECTION
 
Back
Top Bottom