Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,782
- 239,461
Kwa siku mbili mfululizo nimeacha gari langu nyumbani na kuamua kutumia usafiri wa umma ( daladala ) kutoka nyumbani kwangu Tandika Mwembeyanga hadi ofisini kwangu kariakoo.
Lengo langu likiwa kufanya ziara ya uchunguzi ili kubaini changamoto za kituo kipya cha mabasi ya mwendokasi na yale yetu ya mwendo wa konokono , hasa baada kusikia sifa nzuri kutoka kwa vijana wangu wa kazi .
Kiukweli kituo ni kizuri ( japo cement iliyotumika kukijenga ilikuwa ikiletwa kwa mikokoteni badala ya kubebwa na malori ) kiasi cha wadau kuutilia shaka ujenzi wake kama utafanikiwa, Mungu mkubwa , ujenzi umekamilika japo si kwa 100%.
Nilichokiona ni kurejea kwa kasi kwa wapiga debe , hasa kwenye mabasi yanayokwenda Tandika na ule upande wa Mabasi ya kwenda Mbagala , taarifa za awali zilionyesha kwamba hakukuwa tena na wapiga debe , sasa wamerejea kwa kishindo .
Naomba sana kwa mamlaka zinazohusika kuondoa wapiga debe hawa , ambao wengi wao ni mateja na wezi , samaki akunjwe angali mbichi , siku si nyingi tutaona mishikaki ikichomwa ndani ya kituo kama walivyokuwa wanafanya stendi ya zamani .
Mwisho - Dustbin ziwekwe ndani ya kituo .
Majuto ni mjukuu .