Wapi zinapatikana DVD za vikao vya bunge?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wakuu tumeambiwa kua vikao vyote vya bunge haviwezi kuoneshwa live kwa sababu lukuki zilizotolewa na wenye nyumba, tumeambiwa vitarekodiwa na studio za bunge na kurushwa usiku kwenye TV yetu ya kaya.

Kwakua unaporekodi kazi lazima utaisahihisha,kuihariri na kisha kuiruhusu itazamwe. Sasa huu usiku wengine tunakua tumekwisha lala na familia zetu muda hua mbaya kuangalia hizo video za usiku. Naomba kujua kama kuna mahali zinauzwa ama zinahifadhiwa nikazitafute ili angalau nikiwa na muda nitaangalia tu taratibu nafamilia yangu maana huu usiku ni mtihani sana kwangu.

Kuna video za hotupa baba wa taifa zinapatika katika maktaba nyingi kwenye DVD,VHS na CD kwa kuuzwa. Mimi nataka video tu za bunge hili maana ni ngumu kuliona live na video zake kule TV yetu ya kaya zinzwekwa usiku sana.
 
Wanaweza kusema zisiuzwe madukani au wauziwe watu wa chama tu!hii ndo Tanzania mkuu.
 
Nimecheka hadi majirani wametoka Kuja kuniulIZA KUlikoni
Hivi Bunge halijaisha tu maana sijui Hata kinachoendelea.
 
Nimecheka hadi majirani wametoka Kuja kuniulIZA KUlikoni
Hivi Bunge halijaisha tu maana sijui Hata kinachoendelea.
Nafikiri ni fursa kwako wewe na mimi kuungana kutafuta kanda za video kujua kinachojiri mkuu! Tumeambiwa linarekodiwa huenda kanda ziko madukani.
 
Zipo kwenye jengo la ccm nyuma ya msikiti wa manyema ukikosa sogea kweye jengo waliojengewa na wachina karibia na uchaguzi mkuu uliopita wenyewe wanapaita LUMUMBA wale vijana wa jk singida wanakopokelea mpunga ( book 7). Hapo piga ua galagaza hukosi, ukitaka za machinga sogea mtaa huhuo kuna mgahawa mbele yako unaitwa falcon umepata mkuu.
 
Ha ha ha mtoa hoja smart saana..

Angalizo;
Duniani mtafute na kumtegemea Mungu wako maana atakupa uzima wa milele...

Siyo wanadamu...

Asante
 
Zipo kwenye jengo la ccm nyuma ya msikiti wa manyema ukikosa sogea kweye jengo waliojengewa na wachina karibia na uchaguzi mkuu uliopita wenyewe wanapaita LUMUMBA wale vijana wa jk singida wanakopokelea mpunga ( book 7). Hapo piga ua galagaza hukosi, ukitaka za machinga sogea mtaa huhuo kuna mgahawa mbele yako unaitwa falcon umepata mkuu.
Kwahiyo mkuu hili huko ndiko penye CD za vikao vya bunge? Kumbe ni mradi wa chama letu pendwa sasa.
 
Hivi ni muda gani tunapata matangazo ya bunge serikali version huo usiku?
 
Back
Top Bottom