Wapi wanafanya semen analysis Dar?

Mimi sio mtaaluma wa afya ya uzazi ,ila kuwa na korodani moja kusikutie baridi kinyonge mwamba, hiyo hiyo moko inaweza toa mbegu ..nikishauri tu hamia kwenye milo/vyakula vinavyoongeza ustahimilivu wa mbegu na uzalishaji...kama ni mtu wa kula vyakula mwendokasi vya kukaangwa na mafuta achana navyo, piga vyakula vya asili ,gonga mihogo/vianzi/magimbi kula matunda kama mafenesi, mananasi na mapapai (na mbegu zake mapapai)..tafuna mbegu za maboga, almonds, korosho ..kula samaki wa baharini wenye zinc nyingi kama tasi/calamari au ngisi / jodari ..mbogamboga kama biringanya,bamia,ngongwe.. jitahidi pia kama siomtu wa mazoezi kufanya mazoezi ya kutembea au jogging kuruka kamba pull ups na push ups .. ukifanya hivyo consistently miezi mitatu na kuendelea ..ongezea na kumuomba Mungu akutendee kwa wakati wake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…