Wapi nitapata mtego wa kumnasa mgoni/dawa ya kunasiana?

Wapi nitapata mtego wa kumnasa mgoni/dawa ya kunasiana?

Texas Tom.

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2013
Posts
510
Reaction score
273
Best yangu kaoa miaka 3 ilopita kwa style yake, alikua amekaa kiti kirefu akaona binti (kicheche) anapita akamuita akampa viofa akalala nae.

Wiki 2 baadae akamuona anavinjari na jamaa mwingine , akaniita akaniambia, "unaona kale kakikicheche nimepita nae!!" haijapita hata mwezi jamaa kanipigia simu nimfuate mahali nikamkuta yupo na yule mdada tena.

PAUKWA PAKAWA ...Jamaa hamuiti tena kicheche/cheni/kichaka/mlupo ...anamuita BABY!! na ananinisisitiza niwe na heshima kidogo akiwepo....mara mimba, mara mtoto.

Katika maisha riziki hupangwa na Mungu na kwa kweli huyu mtoto kaja na riziki maana jamaa vihela vinampitia siku hizi.

SHIDA INAANZA, MAMA KAPENDEZA KWELIKWELI Jamaa hapati usingizi kisa mama alikua mama huruma na zile njemba zake za zamani zitakua zinaendeleza.

Ametega mitego yote za kushtukiza hola, ametuma marafiki wakajaribu kutongoza lakini hola (anahisi wanakubaliwa lakini wanaficha),sasa anatafuta dawa za kunasiana ili amtegeshee mkewe.Wapi atapata?? wapi nimuelekeze???
 
He he he he, ana kifua cha panzi? Nimeamini watu huwa wanasake presha wenyewe.

Hajakosewa, anasaka kosa.
 
Haya mateso bila chuki, bora aachane naye kabla hajapata kichaa
 
mwanamke anajichunga mwenyewe sio kuchungwa kama ng'ombe.fanya mamboyako utaumiza kichwa bure
 
Ajiamini kwanza. ni kwa nini anatafuta makosa?
 
Sasa presha za nini? Kumbe anamjua toka zamani kama ni kicheche kayataka mwenyewe amwache binti wa watu anasiane alafu? Aibu yake mwenyewe! Aache ujinga!
 
Mwambie aache kujipa presha isiyo ya lazima na atulie na mke wake kama alivyompenda mwanzo

Aliemwambia mtu huwa habadiriki ni nani???????????

Amewahi kutafiti ni kwa nini huyo Binti aliishi maisha yale????????
 
Back
Top Bottom