Hakuna dawa za kunywa, nimetibiwa tezi dume mwaka 2022!! Nilikunywa kila dawa naambiwa inatibu bila upasuaji na bado iliendelea kukua na kunitesa!!
Nenda Agha Khan wanatumia njia ya Sistoscopy haihitaji kupasuliwa kwa kuchana bali vifaa vinaingizwa kupitia tundu la mkojo!! Sijajua kwa huko kwingine
Afya ni gharama!!
Nimefurahi kupata mtu ana experience ya Kupanuka kwa Tezi Dume. Ukisaga Tezi Dume lina tabia ya kurudia kuvimba baada ya wastani wa miaka 5. Mimi nilisaga mwaka 2017 na ilirudi baada ya miaka 7 (2024).
Kama ulivyosema, hakuna dawa ya kutibu kuvimba bali kuiondoa kwa operation. Madhara wakiiondoa haisimami tena, ni bora ukiwa Padre ila kama umeoa, hapo muziki.
Kusaga kupitia tundu la mkojo, si tiba bali ni kupunguza makali ya Uvimbe na usisahau inapovimba inatoa sumu mwilini. Kwa minajiri hiyo, hata PSA ikiwa ni ndogo 0-4 au volume yake ni kati ya 0-31CC bado itaendelea kutoa sumu mwilini.
Mpaka sasa Wachina ndiyo wanaoweza kutibu bila upasuaji kwa kuipiga sindano, maana uanaambiwa Tezi Dume huwa na mechanism ya kijilinda, hivyo ukinywa dawa haiwezi kuifikia.
Kwa upande wangu nina kawaida ya kupima mwili - Full Body Check-up angalau kwa mwaka mara moja. Tezi langu lilianza kuvimba nilipofikisha miaka 50.
Dawa ya Kichina ambayo inaifanya Tezi Dume lisinyae ni kutoka kwa Dr Song ambaye ameresearch kwa muda wa miaka 30 akapata kiboko ya Tezi Dume. Unaitumia kwa muda wa miezi 4 na unapona. Hii ni dawa maalum kwa Cancer ya Tezi Dume ila na Tezidume lililovimba inatibu tu.
Hii ni ghali sana ila kwa Waswahili na kama haijavimba sana, tumia mabaka ya Mzambarau. Dawa za hospitali hazisaidii maana haziwezi kupenyeza katika Tezi Dume.