Hapa karibuni nimefungua pizza and burger shop ila nimejikuta nakwama katika suala zima la packaging, hususani kwenye upande wa pizza.
Maboksi niliyokuwa nayatumia awali niliagiza kutoka Arusha kuja Mwanza ila yalikuwa ni madogo na hayavutii. Na kwa hapa Mwanza kuna wahindi wanauza maboksi ila sio ya square ni ya round na bado hayavutii.
Nilikuwa naomba msaada kwa yeyote mwenye ufahamu na wapi ninaweza kupata maboksi ya pizza meupe au hata printed yawe ya square na kuanzia 14 square inches hadi 18 square inches. Sample ni kama hizi box hapa chini.
Packaging ni muhimu kuwa na mvuto maana ndicho mteja anachokiona kabla ya bidhaa na kisaikolijia mtu yeyote huwa anahamasishwa na muwasilisho wa bidhaa kabla hata ya bidhaa yenyewe.
waone hawa www.Merriam.co.za box zao ni kuanzia tsh 640 mpaka 1120 kwa fedha za kitanzania wapo pretoria ukihitaji naweza kununua na kutuma ntakapokua huko kwa sasa nipo Tanzania sio big deal zipo nyingi tuu kwa mwezi unahitaji kiasi gani au kama una mtu SA angalieni namba ya simu humo anakununulia anatuma tuu mabox hayo kodi yake ipo kidogo tuu ukishindwa nikiwa huko ntakusaidia kuzipata...tukumbushane tuu
shukran kwa msaada wako mkuu ila kwa sasa nilikuwa nahitaji soko la ndani maana niwe na urahisi wa upatikanaji.. nimekwisha fanya research hadi china wanauza box kwa sh 120 tzsh na ni la nch 19 printed, ila wao wanataka order za piece kuanzia 5000.. again thank you sana kwa majibu yako positive mkuu
sawasawa kaka.. ingawa kwa sasa nipo mwanza ila nina jamaa yangu yupo dar nitamjulisha akanitizamie mkuu, nadhani naanza kuuona mwanga kupitia wazo lako mkuu. nashukuru sana