Wapi naweza pata fundi computer wa kuaminika?

Wapi naweza pata fundi computer wa kuaminika?

EGF

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2017
Posts
387
Reaction score
992
Habari,

Naomba kufahamishwa mahali naweza mafundi bora na wa uhakika kwa hapa Dar es salaam wa computer ukiacha hawa wa machinga complex ambao baadhi yao wamekua sio waaminifu.
 
Habari, naomba kufahamishwa mahali naweza mafundi bora na wa uhakika kwa hapa Dar es salaam wa computer ukiacha hawa wa machinga complex ambao baadhi yao wamekua sio waaminifu.

me nashindwa kukuelewa. unata computer ipone au unataka uaminifu??
 
me nashindwa kukuelewa. unata computer ipone au unataka uaminifu??
Natamani computer ipone ila natamani zaidi uaminifu kwasababu kuna mahala pengine hua wanaharibu makusudi kisha wanakuambia hii haiwezi kupona tuuzie sisi. Lakini hata isipopona ila ikibaki na vifaa vyake kama ilivokuja itakua ni bora zaidi kuliko kupelea vifaa vilivyokuepo mwanzo hasa pale machinga hio tabia imeshamili sana.
 
Mi pia ni funding na Nina wenzangu Kama watatu nao no mafundi, hasa unataka huyo fundi afanye kitu gani hasa job description. na una Aina gani ya computer
 
Habari,

Naomba kufahamishwa mahali naweza mafundi bora na wa uhakika kwa hapa Dar es salaam wa computer ukiacha hawa wa machinga complex ambao baadhi yao wamekua sio waaminifu.

Kabla ya kutamani computer yako irudi kwenye hali nzuri tafakari haya mambo. -:
  • Je, computer yako ipo katika hali gani kwa sasa?
  • Computer ina shida gani?/ unalijua tatizo ? Kwani sio kila tatizo linatatulika kwa 100%.
-Upo tayari kugharimia?
-Computer yako ni moja kati zile zinazotengenezeka?.

Kinyume na hapo utalaumu mafundi , mafundi nao wana ukomo wao. Muonekano wa fundi na ofisi yake haina uhusiano kabisa na uwezo wa fundi kiutendaji.
 
Kuna jamaa aliwahi niletea pc nirekebishe coz haipeleki charger, sasa katika kukagu nikagundua adaptor ndio ina shida pale kwenye pin ikabidi kuchuna wire, kukata na kuunga na solder then kuzungushia insulation tape ile kumrudishia mteja weeh jamaa kawaka haikuwa hivi na ukimuelewesha haelewi.
So mtoa mada kama nawe nijamii ya watu wa hivyo hiyo pc baki nayo tu
 
me nashindwa kukuelewa. unata computer ipone au unataka uaminifu??
Watu wa hivi watata sana!!
Kuna mdada alipeleka samsung flani kwa jamaa arekebishe coz haiwaki.
Jamaa akafanya makeke kuweka kwenye seperator na kucheck fresh. Shida ilikuwa lcd ndio imekufa mashine safi.
Basi akarudishia na kufunga rubber band maana mteja hakuwa na budget, mziki kwenye kumkabidhi sasa mteja akawaka fundi siyo muaminifu keshachomoa vitu maana simu haikuwa vile anaenda polisi na maneno mengine kibao.
Licha ya kueleweshwa rubber iwewekwa kurahisisha kazi wakati wa kureplacement but somo halikueleweka ikabidi jamaa asilibe gundi na kumpa.
 
Ni kweli na sisi wateja tumekua tukikosea sana ila wanasema ni bora uchukue tahadhari zote ili hata ikitokea haujafanikiwa angalau useme kwa nafasi yangu nilijitahidi kuhakikisha kifaa changu kinapona ila imeshindikana maana ni ukweli usiopingika kwa kipindi cha hivi karibuni mafundi wengi wamekua sio waaminifu na hii ndio inapelekea baadhi ya wateja kuingiwa na hofu hasa wanapopata shuhuda kutoka kwa wengine.
 
Back
Top Bottom