Wapi naweza kupata huduma ya kufunga Music system ya gari

avi.JNR

Senior Member
Nov 17, 2015
139
87
Ni wapi naweza fungiwa system ya music kwa gari lako yenye ubora wa hali ya juu?
Kama kuna mwenye upeo na hiyo sehemu naomba niwasiliane naye ..naomba unipe namba yako
 
Dicky Sound magomen usalama km upo dar ana page yake instagram kwa jina hilohilo mtafute

Huyu dogo jina tu linampa kiburi cha kupanga bei za ajabu.. Mtafute jamaa mmoja anaitwa Ally yupo lumumba pale maeneo ya benki ya Amana ukimuulizia Ally fundi redio za magari utampata
 
Dicky Sound magomen usalama km upo dar ana page yake instagram kwa jina hilohilo mtafute

Kila mtu anasema dogo uyo. JE ni kweli yupo vizurii? ..mawasaliano yake mpaka INSTAGRAM tu?? Poa nashukuru sana mkuu
 
Huko nadhan ndo utampata kirahis au km vp nenda magomen usalama ofsin kwake utampata

Mkuu nimepata namba yake na maelezo mazurii kwa page yake ya INSTAGRAM nadhan kesho namtafuta mapema sana kabla sikukuu hazijaingia...ila vipi naskia bei zake kubwa ..vipi ni ngapi kwa MAXIMUM
 
Yupo reasonable mbona we nenda kachague sound ya maana utuburudishe mtaani. Kamata kinu cha pioneer ama kenwood usumbue mtaa
 
Kova kakataza disco toto sasa ukifunga hiyo pioneer utakamatwa .ha ha ha maana najua mziki wake mnene saana
 
Dicky Sound magomen usalama km upo dar ana page yake instagram kwa jina hilohilo mtafute

Huyu ndio mkali wa Jiji.Amcheki hata kwenye facebook yumo.
Au kama una number ya Sheta,mtafute atakupa.
Maana wasanii wakubwa kibao kawafungie mziki yeye.Bwana mdogo anatisha kama Neymar
Unaweza kumuitaa Neymar Mziki
 
Mkuu nimepata namba yake na maelezo mazurii kwa page yake ya INSTAGRAM nadhan kesho namtafuta mapema sana kabla sikukuu hazijaingia...ila vipi naskia bei zake kubwa ..vipi ni ngapi kwa MAXIMUM

Bei inaendana na Ubora,maana kama mziki hata wewe mwenyewe unaweza kuufunga.

Starehe gharama,Dogo yupo vizuri kupita maelezo,suala la bei inategemea na mfumo wako unaotaka.Ni bora uende ofisini kwake.Humu hakuna jibu la moja kwa moja.
Ubora wa kazi za mtu ni aina ya watu wanaomfuata,ana deal na celebrities wengi saana,sasa hii inaonyesha kwamba ubora wa kazi yake upoje,na hakuna hata mmoja alieenda kwake akasema kazi mbaya.

Ni mshauri mzuri sana katika kazi yake,hakurupuki tu na kuchukua hela yako,lazima akupe somo kwanza kwa ureefu ndio ujue unataka nini na ufanyie vipi
 
Nime prove hilo mkuu.nimefungiwa system bora kabsa na dogo na ni kwa bei affordable kabisa .na speaker za pioneer ni nomaa sana .nashukuru wakubwa
 
Back
Top Bottom